PICHA: Mtoto wa Oscar Kambona ajiunga na M4C, wengi wajiunga

Uanachama wa huyu mama na wengine waliojiunga wakiwa huko UK ni batili. Katiba ya CHADEMA hairuhusu mambo haya kufanyika nje ya matawi yao ambayo yako ndani ya TANZANIA tu.

Mkuu heshima mbele.

Sasa ingekuwa ni jambo jema kama ungeleta vielelezo ukichambua hicho kipengele kwenye katiba ya CHADEMA kuhusu matawi nje ya TANZANIA, ili mapungufu yaonekane.

Maana wengi labda hatufahamu hilo.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Walitofautiana kisiasa na siasa za zamani ilikuwa ukienda tofauti na wengi (ukabaki unaonyesha msimamo wako) unaonekana adui wa Taifa na ndio maana jamaa akasepa
 
Uanachama wa huyu mama na wengine waliojiunga wakiwa huko UK ni batili. Katiba ya CHADEMA hairuhusu mambo haya kufanyika nje ya matawi yao ambayo yako ndani ya TANZANIA tu.

Je ukiwa na kadi wakati upo nyumbani alafu ukaenda nje ya nchi hapo inakuaje, mie nadhani hawa walioko ulaya ni kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanachama pindi wanaporudi nyumbani waendeleze libeneke
 
Mkuu heshima mbele.

Sasa ingekuwa ni jambo jema kama ungeleta vielelezo ukichambua hicho kipengele kwenye katiba ya CHADEMA kuhusu matawi nje ya TANZANIA, ili mapungufu yaonekane.

Maana wengi labda hatufahamu hilo.
Sura ya 7, toleo la 2006 la KATIBA ya CHADEMA ambayo ipo kwenye website yao itakusaidia katika hili. Hakuna Tawi la CHADEMA lililo nje ya NCHI.(7.2.1). Shughuli hii iliyofanyika UK ni batili tangu mwanzo wake.
 
Chilosisi,

Kimaadili ulitakiwa uandike source ya habari na picha hiyo. Imetoka Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
Mkuu unajuaje kama aliitoa huko huenda na yeye ameitoa wewe ulipoitoa (kama hutaki picha zako zitumike ni vema ukaweka watermark) au ulitaka aweke source : sony camera
 
Je ukiwa na kadi wakati upo nyumbani alafu ukaenda nje ya nchi hapo inakuaje, mie nadhani hawa walioko ulaya ni kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanachama pindi wanaporudi nyumbani waendeleze libeneke
Hakuna tatizo kama unakidhi vigezo vya kuwa mwanachama. Sura ya 5. Sifa( 5.1.1 hadi 5.1.8). Kinachotakiwa hapa ni taratibu zifuatwe kikatiba ili kama mwanachama uwe na haki(5.2), wajibu(5.3). Tundu Lissu anapowakomalia wengine kufuata KATIBA yeye na chama chake wawe wa mfano hata ukiwatazama tu.
 
Binti Wa Oscar Kambona Ajiunga Na Chadema...

Mwenyekiti wa Chadema UK Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Neema Kambona, mtoto wa mwanasiasa mkongwe Mzee Oscar Kambona, shughuli hii fupi ilifanyika Leo Barking baada ya Watanzania wengi kuamua kujiunga na M4C. Picha na Maelezo: Chadema UK
souurce mjengwa blogg
Kutoka Tawi la Chadema Nchini Uingereza:Mtoto wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Mzee Oscar Kambona Ajiunga Chadema

Written by haki | // 0 comments

photo%25281%2529.JPG

Mwenyekiti Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Mchungaji Mathew Juttah

source hakingowi
yap! tunajua uchaguzi ukija atakuja bongo kuwapigia kura halafu ndo arudi UK! hahaaaa!
 
Sura ya 7, toleo la 2006 la KATIBA ya CHADEMA ambayo ipo kwenye website yao itakusaidia katika hili. Hakuna Tawi la CHADEMA lililo nje ya NCHI.(7.2.1). Shughuli hii iliyofanyika UK ni batili tangu mwanzo wake.

Mkuu sawa umeona hili.

Lakini vipengele hivi vya 7.2.1 na 7.2.2 havijatanabaisha kwamba ni lazima tawi lianzishwe ndani ya Tanzania tu na ndio maana vimeeleza kwa ujumla.

Kwahi kwa kuelewa hivyo basi tawi linaweza kufungliwa mahali popote pale nje ya mipaka ya Tanzania.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.
Mabint wengine bana mara kule unauliza machozi hujayaona hapa unauliza mikono haijaache; ok hiyo PC yako inamatatizo ama ni uwezo mdogo wa kufikiri.
 
Mkuu sawa umeona hili.

Lakini vipengele hivi vya 7.2.1 na 7.2.2 havijatanabaisha kwamba ni lazima tawi lianzishwe ndani ya Tanzania tu na ndio maana vimeeleza kwa ujumla.

Kwahi kwa kuelewa hivyo basi tawi linaweza kufungliwa mahali popote pale nje ya mipaka ya Tanzania.
7.2.1 Tawi litaundwa katika eneo la kijiji, mtaa au shehiya ya kiutawala katika mamlaka ya serikali za mtaa.
 
7.2.1 Tawi litaundwa katika eneo la kijiji, mtaa au shehiya ya kiutawala katika mamlaka ya serikali za mtaa.

Sawasawa kabisa ikimaanisha kwamba tawi litaundwa kwa kufuata sheria ya kiutawala za mamlaka ya serikali za mtaa.

Hivyo kwa wale walio nje wanatumia haki yao ya kukusanyika kuunda chama bila kufunja sheria ya "public order" ambayo ni kufanya vurugu.
 
nadhani amekuelewa sasa
 
Karibu sana mtoto wa Kambona. Aluta Continua Mapambano yanaendelea na hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Nimefurahi sana watu wengi wanavyojiunga na mageuzi,kweli nimeamini huwezi kuzuia mabadiliko ambayo muda wake umefika.
 
samahani bro nilikuwa nataka kumjibu mtu mwingine

Nilikuwa najaribu kutafuta kwamba kwanini mkuu Wild Card anataka CHADEMA ifuate katiba ya CCM inavoeleza kuhusu matawi ya nje ya nchi.

Anasahau kwamba katiba zinatofatiana na hata manifesto pia.
 
Nilikuwa najaribu kutafuta kwamba kwanini mkuu Wild Card anataka CHADEMA ifuate katiba ya CCM inavoeleza kuhusu matawi ya nje ya nchi.

Anasahau kwamba katiba zinatofatiana na hata manifesto pia.
Mkuu magamba tumewashika kuliko ndio maana wanapagawa.
 
Ni uamuzi sahihi wa dada Neema Kambona kujiunga na wanaharakati kupitia chama mbadala cha CHADEMA.

Kuwepo kwako CHADEMA UK kutaleta tija kwenye maeneo ya upangaji mikakati na hasa eneo la "public affairs" maana naona una uzoefu fulani katika eneo hilo.

Niliona mchango wako kuhusu "online movement" kwa bbc kupitia kipindi cha Stephen Sackur alipomhoji raisi wa Bebo Joanna Shields.

Hongera sana.
 
Back
Top Bottom