PICHA: Mtoto wa Oscar Kambona ajiunga na M4C, wengi wajiunga

Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Why do you always ask silly questions? Sasa wataachana vipi hiyo mikoni ilhali hii ni ''still'' picture? Na Mwalimu kumfukuza Kambona ndio uzao wake sio WATANZANIA?
 
Hivi hawa walio nje ya nchi katiba inawatambua kama wapiga kura??

Mkuu Katavi niliwahi kuuliza hili swali sikupata majibu. Siku hizi kila Chama kinawafuata diaspora lakini sijui kama watakuwa na maamuzi wakati wa uchaguzi. Watu badala ya kwenda Nyangoto na Kewancha ama Uzogole wao wanang'ang'ania UK, USA! Naona kama ni matembezi kama matembezi mengine!
 
Last edited by a moderator:
Hili ni swali la kijinga kwa mtu mwenye akili timamu!
Ni mtazamo wako tu. Yalisemwa haya enzi hizo. Na hata Kambona mwenyewe aliporudi nchini akaanzisha chama cha TADEA( nadhani?) yalisemwa pia. Namshangaa huyu binti kukiacha chama ambacho baba na mama yake ni waasisi wake na kukimbilia waliko Wajomba.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Mwalimu was not an SI Unit in everything, naye kama mwanadamu wa kawaida alikuwa na mapungufu yake, anyway mwana/binti hatahukumiwa kwa dhambi ya mzazi wake
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Sweetie kwani kama Mwl. hakumkubali Kambona vivyo ndivyo yawapasa CHADEMA kumkataa mwanae Kambona?
 
Linapokuja suala la nepotism, hakuna chama cha siasa chenye afueni Tanzania

Chadema viti maalum kumejaa watoto, wake, wakwe, ndugu, marafiki wa viongozi wa chama na walipojivuta nje kidogo ni kwa mwenye kutumia jina la Nyerere licha ya kuwa inasemekana kuwa anaishi Maryland, Marekani

Hili ni muendelezo tu wa trend ambayo ipo tayari kwenye chama

Vyama hivi vinaendeleza dhana ya kibaguzi ya Kikoloni, upwndeleo kwa tabaka maalum
Kwa hiyo ulitaka chama kiwe na wanachama gani manake sasa kila kitu kikifanywa mnakosoa ,
Leo mnasema mwenyekiti anavaa koti moja kesho majina makubwa yakianza kujiunga mnasema wanataka ubunge ,... tutafika kweli???
 
Ni mtazamo wako tu. Yalisemwa haya enzi hizo. Na hata Kambona mwenyewe aliporudi nchini akaanzisha chama cha TADEA( nadhani?) yalisemwa pia. Namshangaa huyu binti kukiacha chama ambacho baba na mama yake ni waasisi wake na kukimbilia waliko Wajomba.
Kma alivyosema Nyerere, CCM SIO BABA WALA MAMA
 
Binti Wa Oscar Kambona Ajiunga Na Chadema...

Mwenyekiti wa Chadema UK Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Neema Kambona, mtoto wa mwanasiasa mkongwe Mzee Oscar Kambona,
shughuli hii fupi ilifanyika Leo Barking baada ya Watanzania wengi kuamua kujiunga na M4C. Picha na Maelezo: Chadema UK

Kwa hiyo katika watanzania wote waliojiunga siku hiyo mtoto wa kambona ndiye aliyedeserve kupigwa picha?
 
Kwa hiyo katika watanzania wote waliojiunga siku hiyo mtoto wa kambona ndiye aliyedeserve kupigwa picha?
HAYA PICHA ZAIDI HIZO MKUU, SHINDWA MWENYEWE
[h=1]Kutoka Tawi la Chadema Nchini Uingereza:Mtoto wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Mzee Oscar Kambona Ajiunga Chadema[/h]

Written by haki | // 0 comments

photo%25281%2529.JPG

Mwenyekiti Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Mchungaji Mathew Juttah

Kma alivyosema Nyerere, CCM SIO BABA WALA MAMA
Mimi nilidhani angekuwa kama yule binti wa Zulfikar Ali Bhuto wa Pakistani. Hivi TADEA yenyewe ipo kweli? Kambona alirudi kwa kishindo kidogo akaishia kuungwa mkono na akina John Lifa Chipaka tu. Wote waliomuasi Mwalimu hawakufanikiwa KISIASA hata baada ya kuwa ameacha madaraka. Angalau akina Hans Pope wanafanya vizuri huku kwenye malori na kwenye Simba na Yanga hasa suala la Twite(r)!
 
Wazamani sana wewe! una bado zile fikra za zidumu fikra za mwenyekiti na una akili za kupatiliza makosa ya baba kwa mwana

bila shaka utakuwa na maisha ya ajabu sana, Mwalimu hakuwa malaika naye alikuwa na makosa yake kadhaa na hatuwezi sasa kumuhukumu Makongoro au Madaraka kwa makosa ya Baba yake

Kambona naye alikuwa mwanadamu na alikuwa na makosa kadhaa kama wengine na hatuwezi binti yake kwa makosa ya baba yake huo ni UBAGUZI

Na hiyo unayoona ni picha ilipigwa wakiwa wameshikana mikono, baada ya picha waliachana mikono au wewe unadhani wameendelea kushikana mpaka sasa??
 
Hhahahahaha,
Mkuu huyu jamaa anazania bado wameshikana mikono.
Kwa hiyo kama baba yake alikuwa anavuta sigara basi na mtoto naye lazima avute sigara????
 
Back
Top Bottom