PICHA: Mtoto wa Oscar Kambona ajiunga na M4C, wengi wajiunga

Propaganda kwa maana yake mbaya.

Hapo ujumbe ni kwamba mkiona hata mtoto wa Kambona kajiunga CHADEMA basi mjue bonafide ya hiki chama inakubalika hata katika familia zilizoanza upinzani miaka ya sitini huko. Kwa hiyo wengine pangeni mstari.

It is sad that we are reduced to pedigree instead of focusing on ability. And this is coming from CHADEMA.

Next thing you know Neema anapewa kiti maalum kwa ajili ya jina, culture of entitlement inaanza polepole, tunatengeneza kina Raila wetu.

Halafu kesho CHADEMA watataka kuwablast CCM kwa nepotism ya kuwa fast track kina Makamba and Nchimbi.

I know a photo op is not the same thing, but still, the principle stands. And who is to say what awaits the first CHADEMA administration?

Linapokuja suala la nepotism, hakuna chama cha siasa chenye afueni Tanzania

Chadema viti maalum kumejaa watoto, wake, wakwe, ndugu, marafiki wa viongozi wa chama na walipojivuta nje kidogo ni kwa mwenye kutumia jina la Nyerere licha ya kuwa inasemekana kuwa anaishi Maryland, Marekani

Hili ni muendelezo tu wa trend ambayo ipo tayari kwenye chama

Vyama hivi vinaendeleza dhana ya kibaguzi ya Kikoloni, upwndeleo kwa tabaka maalum
 
Ukweli husemwa:

Siasa za watembezi kutoka bongo bana, kila kitu utapata. swaga, majigambo, mbwembwe na uchakachuaji. Ukizichungulia kwa undani, hakuna kitu chochote cha maana. Si CCM UK wala CHADEMA UK. Leo CHADEMA wanakuja na santuri nyingine mpya yenye kichwa cha habari kinachoweza hata kumfanya kichaa akapona. Kesho ni zamu ya CCM UK.

Kweli kasi ya CHADEMA UK inatisha, kama ndiyo kukutana kwenye pub za East London na kuanza kujadili mstakabali wa taifa baada ya kutandika Guinness foreign extra na Jack Daniel na hapo hapo wengine kuanza kukumbuka kama wanahitaji kuwa na tiketi yenye kitambulisho chenye nembo ya CHADEMA itakayowapa usafiri wa bure kwenye Pub za Wakenya na Wanaigeria za East London. Kweli siasa kwa sasa zimefika kwa wenyewe.

Hata hivyo, bora ninyi mnaopenda tujue kama CHADEMA UK ofisi ziko kwenye meza za Pub. CCM UK wao hata pesa za kutokea nje hawana, achilia mbali ukumbi wa mikutano. Mikutano yao inafanyika jikoni kwenye one bedroom flat.

Kwa nini tusiendelee kufanya kile ambacho tunakiweza (box na kuosha wazee wa kizungu) kuliko kujiingiza kwenye taaluma ambazo hatuna ujuzi nazo.

Watembezi wa Ulaya, ni vizuri ya Kaizari tumwachie kaizari na sisi tuendelee na ya Mussa
Hii inaonyesha CDM ilivyokuwa Chama ambacho hakibagui Dini ama kufungamana na dini yoyote, kumbe kama mtu anakunywa Guiness anywe, tangawizi anywe na hata Kahawa.

Si vinywaji vitakavyoikomboa nchi, maana tunashuhudia hata sasa kumbe ni moyo wa kizalendo na wa kujitoa kuangalia ukweli bila kutumia uzoefu kwamba nimelelewa na chama fulani hata kama kinaonyesha kufikia ukomo, tuziongozwe na mazoea, tuongozwe na uzalendo na ukweli.

Kumbe kama hatuna uzalendo na utayari wa kukubali kuacha kuongozwa na mazoea, haya kama kikao kitafanyika ndani ya Kanisa huku ibada ikiendelea hakitakuwa na maana, kwani PUB ni nini bwana, watu tunajali kinachozungumzwa hapo sio eneo!
 
"Historia inaonesha harakati za ukweli hazifanyikii movenpick wala kwenye hoteli yoyote ya kifahari,hufanyikia chini kabisa kama mashambani,vijiweni huko ndiko walipo watu wenye kiu ya mabadiliko,na ukiwadharau hawa ipo siku utalia na kusaga meno.sehemu unazotaka hizi harakati zifanyikie huko hufanyika harakati za kifisadi kama kutia saini mikataba ya wizi wa rasilimali na dili za wizi"

Hili ndilo tatizo kubwa kwa Watanzania wengi. Kwanza tumejengeka tabia kuwa kila tajiri ni fisadi na mwizi lakini pale tu anapokusaidia katika hali na mali anakuwa siyo mwizi wala fisadi. Hii ni dhana mbaya na potofu kwa jamii endelevu.

Tatizo langu na hawa Watembezi ni jinsi wanavyoendesha siasa zao. Kwa mtu makini, atagundua kuwa uendeshaji wa siasa zao umekaa zaidi kimajungu, kiutaperi na uchakajuaji.

Nani kasema harakati chanya za mabadiliko na mapinduzi ya fikra na utendaji yanafanikiwa kama watu pekee wa vijiweni na mashambani watashilikishwa.

Historia ya Tanzania inaonyesha vilevile Mwalimu Nyerere ilibidi asaidiwe na matajiri furani katika kufanikisha harakati za kulikomboa Taifa.
Nchi inajengwa na watu wa matabaka yote katika jamii. Matajiri, masikini, wakulima na wafanyakazi.
 
mtu yuko ulaya,maisha yamemshinda huko anaanza kutafuta namna nyingine ya kutoka,anaona ni bora achague siasa ya tanzania ili akirudi apate lau udiwani.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.
Inaelekea siasa za wakati huo zilikupita au haukuwepo bado. Kambona hakutimuliwa na Nyerere, Kambona aliondoka mwenyewe baada ya kutokubalina naye kuhusu Azimio la Arusha na siasa ya Ujamaa.
Ukiangalia sana yeye alikuwa mtu makini aliyelitendea Taifa letu, changa wakati ule, jambo jema. Maana alipoona hawezi kufuata kitu asichokiamini aliamua kuachia ngazi na kuondoka nchini.
Wakati hayo yanaendelea wapo waliobakia wakimhadaa tu Mwalimu, kumbe hawakuwa waumini wa kweli wa ujamaa.
Ndiyo hawa ambao sasa ni tatizo kwa taifa, mafisadi!
 
Ninakubaliana sana na wewe. Watanzania kwa sasa tuna ugonjwa wa siasa. Kwa sasa hata uvivu tumeanza kuutafutia sababu ya kisiasa. Ninafikili milango ya kisiasa huru ilichelewa kufunguliwa ndio maana Watanzania wengi wanafikiri kila tatizo kwa sasa ni siasa. Wanasiasa nao kwa ubinafsi wao, hawaisaidii jamii ili iweze kujua wajibu wake.

Watu ambao tunafikili angalau wamefunuliwa katika upambanuzi na kujifunza lipi la Kaizari na lipi la Mussa kwa vile wanaishi kwenye nchi ambazo ndiyo waasisi wa demokrasia tunazozifuata ndiyo hawa na picha zao za ajabu kwenye mitandao.

Ama kweli Tanzania bado tuna safari ndefu
Nina uhakika kama mwalimu wa hesabu ataamua kuweka jina lake kwenye kumbukumbu za kweli, mwalimu wa somo la uraia akiamua kuwafungua wanafunzi, daktari akafanya kitu adimu, accountant akakubali kufuata kanuni zake, mhandisi akaamua kutokubali error za kipuuzi au kupitisha pitisha vitu kwa kijinga chini ya usimamizi wa bodi za utaalamu husika tutawapuuza hawa jamaa wanaowafanya watu wawaone kama miungu watu.

Its time to wake up, mapinduzi ya kweli hayawezi kuletwa na siasa bali kwa sisi kuwa na dhamira ya kujiletea mabadiliko katika maisha yetu ya kila siku.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Kah! Radhia!!. Urguement zako nazo!! Kwani mtoto ni sawa na baba? Kila mmoja ana uhuru na matamanio yake. TAFAKARI
 
Mkuu hiyo picha mbona inaonesha kana kwamba ukumbi ulikuwa mtupu kwa kuwa viti vi wazi na hata meza kuu mapengo ni mengi!

Hiyo itakuwa ni Pub kwa vile pub nyingi za Uk huwa zinaonyesha spoti. Ukiangalia vizuri utaona kuna luninga ukutani na projector. Hizo ndizo ofisi za vyama vya siasa ya Watanzania UK
 
Hivi hawa walio nje ya nchi katiba inawatambua kama wapiga kura??
 
Nina uhakika kama mwalimu wa hesabu ataamua kuweka jina lake kwenye kumbukumbu za kweli, mwalimu wa somo la uraia akiamua kuwafungua wanafunzi, daktari akafanya kitu adimu, accountant akakubali kufuata kanuni zake, mhandisi akaamua kutokubali error za kipuuzi au kupitisha pitisha vitu kwa kijinga chini ya usimamizi wa bodi za utaalamu husika tutawapuuza hawa jamaa wanaowafanya watu wawaone kama miungu watu. Its time to wake up, mapinduzi ya kweli hayawezi kuletwa na siasa bali kwa sisi kuwa na dhamira ya kujiletea mabadiliko katika maisha yetu ya kila siku.

You have nailed it. Ukiongea hivi kwa Watanzania wengi wanafikili hii ni nadharia tu kwa sababu macho yao bado yamezibwa na fikra potofu.Tanzania kama nchi, bado tuna safari ndefu. Ndiyo maana nawachukia wana siasa wengi wa Tanzania kwa sababu wametawaliwa na ubinafsi wa hali ya juu.
 
Mpiga picha hakuwambia wafunge mdomo manake inatisha ukiangalia Mara mbili
 
Chilisosi Mkuu hiyo picha mbona inaonesha kana kwamba ukumbi ulikuwa mtupu kwa kuwa viti vi wazi na hata meza kuu mapengo ni mengi!

Mkuu, usishangae, hizo ndizo ofisi za vyama vya siasa ya Watanzania Uk?. Meza za Pub ndiyo ofisi. CCM wao wanafanyia kwenye chumba cha one bedroom flat ambapo hata kwa sheria ya UK ni makosa. Wanahitaji kwanza ruhusa kutoka halmashauri kama nyumba wanaifanya ofisi.

Msidanganyike, Wote ni wababaishaji tu. Si CCM UK wala CHADEMA UK
 
Iwe ni bar, casino, road, airport, chumbani jikoni au sebuleni hatujali we walete tu M4C.... kuna siku tutawatambua tunawahitaji iwe kwa "katiba mpyya" au ya viraka
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Chadema haina uhasama na familia ya marehemu Kambona. Watoto wa familia hiyo sidhani kama wana kizuizi cha kujiunga na chadema.
 
Back
Top Bottom