PICHA: Mtoto wa Oscar Kambona ajiunga na M4C, wengi wajiunga

Chilisosi

JF-Expert Member
Oct 19, 2008
3,051
747
Binti Wa Oscar Kambona Ajiunga Na Chadema...

Mwenyekiti wa Chadema UK Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Neema Kambona, mtoto wa mwanasiasa mkongwe Mzee Oscar Kambona, shughuli hii fupi ilifanyika Leo Barking baada ya Watanzania wengi kuamua kujiunga na M4C. Picha na Maelezo: Chadema UK
souurce mjengwa blogg
Kutoka Tawi la Chadema Nchini Uingereza:Mtoto wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Mzee Oscar Kambona Ajiunga Chadema

Written by haki | // 0 comments

photo%25281%2529.JPG

Mwenyekiti Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Mchungaji Mathew Juttah

source hakingowi
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

For all I know Kambona's departure was more like a way of calling it quits as his views differed from those of Nyerere in many ways

So I beg to differ from you Kambona wasn't sacked or anything
 
Ukweli husemwa:

Siasa za watembezi kutoka bongo bana, kila kitu utapata. swaga, majigambo, mbwembwe na uchakachuaji. Ukizichungulia kwa undani, hakuna kitu chochote cha maana. Si CCM UK wala CHADEMA UK. Leo CHADEMA wanakuja na santuri nyingine mpya yenye kichwa cha habari kinachoweza hata kumfanya kichaa akapona. Kesho ni zamu ya CCM UK.

Kweli kasi ya CHADEMA UK inatisha, kama ndiyo kukutana kwenye pub za East London na kuanza kujadili mstakabali wa taifa baada ya kutandika Guinness foreign extra na Jack Daniel na hapo hapo wengine kuanza kukumbuka kama wanahitaji kuwa na tiketi yenye kitambulisho chenye nembo ya CHADEMA itakayowapa usafiri wa bure kwenye Pub za Wakenya na Wanaigeria za East London. Kweli siasa kwa sasa zimefika kwa wenyewe.

Hata hivyo, bora ninyi mnaopenda tujue kama CHADEMA UK ofisi ziko kwenye meza za Pub. CCM UK wao hata pesa za kutokea nje hawana, achilia mbali ukumbi wa mikutano. Mikutano yao inafanyika jikoni kwenye one bedroom flat.

Kwa nini tusiendelee kufanya kile ambacho tunakiweza (box na kuosha wazee wa kizungu) kuliko kujiingiza kwenye taaluma ambazo hatuna ujuzi nazo.

Watembezi wa Ulaya, ni vizuri ya Kaizari tumwachie kaizari na sisi tuendelee na ya Mussa
 
Ukweli husemwa:

Wanakera sana na siasa zao ambazo hazina mielekeo mbadala. Katiba ya nchi kwanza haiwatambui kwenye sanduku la kura. Sijui hata kelele zao za mwanzo za diaspora diaspora zimeishia wapi.

Waone nao wana CCM UK

Mkuu naona umeamua kuwavua nguo wote! Hahahhaha! siku nyingine utusaidie kapicha kutoka kila upande ili tujiwekee kumbukumbu!! Kweli 2015 inatafutwa kwa kila mbinu!!
 
Watanzania tutaacha lini siasa za kushabikia majina?

Tunajenga matabaka ndani ya vyama, mtoto wa Kambona ana hadhi kubwa kuliko mtoto wa Kichwabutwa asiyetoka kwenye familia "maarufu"

Hatuoni?
 
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Haukujua kuwa Kambona alirudi NCHINI kwakati wa Msamaha wa RAIS MWINYI na alikuwa na CHAMA chake Hapa Dar? Na

Nyerere alikuwa bado Hai...

Chama Cha Kambona Tanzania kilikuwa kinaitwa TADEA
 
  • Thanks
Reactions: VEO
MsemajiUkweli
Mkuu nimekukubali!! Nadhani kuna haja ya kubadili namna ya kuendesha siasa zetu, tumeegemea mno kwenye siasa badala ya kufanya mapinduzi ya kweli katika sekta za elimu, kilimo pamoja na uzalisha.
 
Last edited by a moderator:
Chilisosi Mkuu hiyo picha mbona inaonesha kana kwamba ukumbi ulikuwa mtupu kwa kuwa viti vi wazi na hata meza kuu mapengo ni mengi!
 
Last edited by a moderator:
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Kwani Mwalimu alikuwa na cheo gani katika CHADEMA? Au mtoto wa Kambona ana uhusiano gani na babake?

1. Abbas Mtemvu je?
2. Teddy Kaselabantu?
3.
 
Watanzania tutaacha lini siasa za kushabikia majina?

Tunajenga matabaka ndani ya vyama, mtoto wa Kambona ana hadhi kubwa kuliko mtoto wa Kichwabutwa asiyetoka kwenye familia "maarufu"

Hatuoni?

Propaganda kwa maana yake mbaya.

Hapo ujumbe ni kwamba mkiona hata mtoto wa Kambona kajiunga CHADEMA basi mjue bonafide ya hiki chama inakubalika hata katika familia zilizoanza upinzani miaka ya sitini huko. Kwa hiyo wengine pangeni mstari.

It is sad that we are reduced to pedigree instead of focusing on ability. And this is coming from CHADEMA.

Next thing you know Neema anapewa kiti maalum kwa ajili ya jina, culture of entitlement inaanza polepole, tunatengeneza kina Raila wetu.

Halafu kesho CHADEMA watataka kuwablast CCM kwa nepotism ya kuwa fast track kina Makamba and Nchimbi.

I know a photo op is not the same thing, but still, the principle stands. And who is to say what awaits the first CHADEMA administration?
 
Chilisosi Huyo binti kwa sura ni Kambona ila kachemka mchano wa nywele, angepiga way ningemkubali.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hiyo mikono hawaachani sasa? Halafu kwanini Kambona alitimuliwa na Mwalimu lakini leo Chadema wanamkubalia mtoto wake uanachama kiurahisi hivyo.

Nyerere alimtimua Kambona kwa sababu hakumuunga mkono hasa sera yake ya Ujamaa. Zipo pia sababu nyingine ila nakumbuka hii ni mojawapo. Pia kumbuka watoto wana mtazamo na msimamo wao binafsi. Huwezi husisha maisha ya Kambona na watoto wake ambao kwa sasa ni watu wazima na wana uwezo wa kuchambua pumba na mchele.
 
Ukweli husemwa:

Siasa za watembezi kutoka bongo bana, kila kitu utapata. swaga, majigambo, mbwembwe na uchakachuaji. Ukizichungulia kwa undani, hakuna kitu chochote cha maana. Si CCM UK wala CHADEMA UK. Leo CHADEMA wanakuja na santuri nyingine mpya yenye kichwa cha habari kinachoweza hata kumfanya kichaa akapona. Kesho ni zamu ya CCM UK.

Kweli kasi ya CHADEMA UK inatisha, kama ndiyo kukutana kwenye pub za East London na kuanza kujadili mstakabali wa taifa baada ya kutandika Guinness foreign extra na Jack Daniel na hapo hapo wengine kuanza kukumbuka kama wanahitaji kuwa na tiketi yenye kitambulisho chenye nembo ya CHADEMA itakayowapa usafiri wa bure kwenye Pub za Wakenya na Wanaigeria za East London. Kweli siasa kwa sasa zimefika kwa wenyewe.

Hata hivyo, bora ninyi mnaopenda tujue kama CHADEMA UK ofisi ziko kwenye meza za Pub. CCM UK wao hata pesa za kutokea nje hawana, achilia mbali ukumbi wa mikutano. Mikutano yao inafanyika jikoni kwenye one bedroom flat.

Kwa nini tusiendelee kufanya kile ambacho tunakiweza (box na kuosha wazee wa kizungu) kuliko kujiingiza kwenye taaluma ambazo hatuna ujuzi nazo.

Watembezi wa Ulaya, ni vizuri ya Kaizari tumwachie kaizari na sisi tuendelee na ya Mussa

"Historia inaonesha harakati za ukweli hazifanyikii movenpick wala kwenye hoteli yoyote ya kifahari,hufanyikia chini kabisa kama mashambani,vijiweni huko ndiko walipo watu wenye kiu ya mabadiliko,na ukiwadharau hawa ipo siku utalia na kusaga meno.sehemu unazotaka hizi harakati zifanyikie huko hufanyika harakati za kifisadi kama kutia saini mikataba ya wizi wa rasilimali na dili za wizi"
 
Mkuu nimekukubali!! Nadhani kuna haja ya kubadili namna ya kuendesha siasa zetu, tumeegemea mno kwenye siasa badala ya kufanya mapinduzi ya kweli katika sekta za elimu, kilimo pamoja na uzalisha.

Ninakubaliana sana na wewe. Watanzania kwa sasa tuna ugonjwa wa siasa. Kwa sasa hata uvivu tumeanza kuutafutia sababu ya kisiasa. Ninafikili milango ya kisiasa huru ilichelewa kufunguliwa ndio maana Watanzania wengi wanafikiri kila tatizo kwa sasa ni siasa. Wanasiasa nao kwa ubinafsi wao, hawaisaidii jamii ili iweze kujua wajibu wake.

Watu ambao tunafikili angalau wamefunuliwa katika upambanuzi na kujifunza lipi la Kaizari na lipi la Mussa kwa vile wanaishi kwenye nchi ambazo ndiyo waasisi wa demokrasia tunazozifuata ndiyo hawa na picha zao za ajabu kwenye mitandao.

Ama kweli Tanzania bado tuna safari ndefu
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom