Picha: Mkutano wa CUF Dar wafurika

Na wewe vp? Ikizungumziwa cuf unakimbilia kukiponda cdm badala ya kukitetea cuf! Vichwa vyenu vimekuwa programmed si mchezo!
Si hivyoi bali ni jino kwa jino haiwezekani jino kwa kucha. Kuponda kwa kuponda ndio sera ya JF.
 
Mimimnaona kutofahamu na kutouliza ndio kosa kubwa kuliko hayo ya kutoweka bendera na kutia mikono mfukoni.

Muelewa wa siasa hashangai kuona gestures za nama fulani kwenye hutuba kwani huwa zinaendana na jambo linalozungumzwa.
Hili la Bendera tena ni ujinga ulioje kuliuliza asa far as Seif Sharifu Hamadi Concerned. Hebu tuambie nini Cheo cha huyu Bwana katika Serikali ya Tanganyika AKA Tanzania hata apeperushe bendera wakati akihutubia?

Wewe acha kujifanya ndio una akili sanaaaa. Kuwepo kwake DAR sio kwa shughuli za Umakamu wake wa huo mkoa wenu bali shughuli za CUF kitaifa. CUF taifa ni kwa Tanzania na huo umakamu wake unaishia huko Unguja na Pemba. Huku hatumtambui kwa hiyo bendera aliyokuja nayo bali ya CUF.

Ni jambo lipi linaloendana na kutia mikono mfukoni ndugu mtaalamu wa gestures?
 
Biola shaka tunautaka Muungano na wewe ndiye unatakiwa uwe mwakilishi wa Chadema Zanzibar maanake mna sheria zenu lazima uwe Mzanzibar - Mkandara atakubalika vipi? Hapa penyewe nilipo naitwa chogo na wamakonde leo nikagombee Zanzibar! Hunipendi kweli..haaa! haa! nafanya utani usije nitafuta..
CUF na CCM wote ni Wanzanzibar wenye asili ya nje sasa Chadema wataweza vipi kupenyeza hilo league lenu ikiwa Wazanzibara wenyewe wanatupwa nje..Na vipi naona Maalim Seif kanawir hadi Sigda imeondoka ama kweli Ikulu kutamu weee!

Mkandara! hiyo ndio sisa ya Tanzania, nasikia kuna Chama fulani viongozi lazima watoke kule juu ya Tanganyika.
 
mkuu wangu umeenda sana ndani..mwenye akili zake timamu anawajua hawa jamaa na siasa wanazoziendesha

Hata sisi wenye akili timamu tunajua siasa wanazoendesha chadema; tunajua mna ajenda gani kuhusu zanzibar, tunajua mansukumwa na mna ajenda gani kuhusu uislam na waislam..

msidhani mnawaweza kuficha tena, too late bro
 
Alaa mbona hueleweki mara chadema ni chama cha wakristo hawezi kufika zanzibar etc?? mara mtafika tu ipi ni ipi??

Sasa cha ajabu nini hapo hata CUF itafika kote huko kuanzia mbeya hadi Bukoba; Kigoma hadi Pemba itafika tu..
CUF ifike Bukoba vipi na waliisha ondoka wee vipi.. Mlianza zamani kuondoka Bara ndio maana uchaguzi wa mwaka 2005 mlianza kupoteza Wabunge, mwaka 2010 bara mmebakia na mmoja sasa hizo nguvu ya kurudi huko bara mtaipata vipi ikiwa biashara iliwashinda..

Chadema sio chama cha Wakristu bali WATANZANIA na maadam wewe na kina Jussa mnataka kujitenga kwa sababu ya Uislaam wenu,. mimi sintokuwa nanyi na wala Waislaam wa bara ambao tunaamini Chadema ni chama cha watu wote. Wapo wengi tu Chadema waliosoma madrasa, sio lazima uwaone wewe wala hawana maonyesho!...tutafika tu usiwe na hofu....
 
Acha zako Mgogo angeyasema haya..Na CUf imeshindwa vipi ku penetrate Ugogoni au kwa sababu nako wakristu wamejaa muilsaam wewe tu..
Mkuu usitake sana kuutumia Uislaam maana haupo Zanzibar ila kuna Usultan ambao mnautumia sana kudanganya wananchi kama enzi za utumwa na wakoloni.. Wazo hilo ondoa kabisa, ila baina yao wapo waislaam nao wa kuhesabu kutokana na TOTAL submission to Allah.. Hizi habari za kutoa shahada na kuitana waislaam kwa kuwa kazaliwa mwarabu, mhindi na Mngazija ni ukungu wa ubongo unaotakiwa kusafishwa.

Chadema watafika tu Zanzibar Ishaallah maadam tumeisha uvua unafiki wa CUF wapo watu watakuja tuelewa na wala hatuna sababu ya kushindana leo. Leo hii mnajinadi bara mtashindwa na taratibu wananchi wataanza kuziona rangi zetu kutumia dini kama ngao ya unafiki mkubwa mlokuwa nao hao kina Seif na mamluki wake. Na ajabu mmefikia hata kuwafukuza Waislaam wenzanu au HR kabadilisha dini?.. sio Muislaam huyo?

Lawama na Nwato zote hizo zinaletwa dharau yenu kwa wazanzibari na kuhisi kuwa uislamu ni uarabu. Uislamu ni imani na muislamu kama binaadamu mwengine anaasi lakini hatoki kwenye dini.

Dharau na lengo la udini mbadala kwa Wazanzibri ndio linawafanya CHADEMA msipate wanachama. Bila shaka wapo wengi mliowapandikiza kuja kupambana na uislamu, pengine hao watakuwa wanachama wenu. Hata hivyo hebu nikupe somo kidogo.

Siasa kwa Zanzibar si mchezo wa kujifundishia bali ni jambo liliopo ndani ya damu ya Wazanzibari wote. Huwezi kuwadanganya na wanapoona mwenzao anawaendea kinyume dini haiwi kizingiti cha kumtowa kwenye siasa, hatolewi dini,naomba ufahamu.

Sasa Hamadi Rashidi ametolewa kwenye CUF sio uislamu na hivyo anaweza akaenda pengine lakini kama Mzanzibari anaelewa kuwa siasa si mchezo wa mpira kuwa utanunuliwa na mashabiki waendelee kukushangilia.
 
CUF ifike Bukoba vipi na waliisha ondoka wee vipi.. Mlianza zamani kuondoka Bara ndio maana uchaguzi wa mwaka 2005 mlianza kupoteza Wabunge, mwaka 2010 bara mmebakia na mmoja sasa hizo nguvu ya kurudi huko bara mtaipata vipi ikiwa biashara iliwashinda..

Chadema sio chama cha Wakristu bali WATANZANIA na maadam wewe na kina Jussa mnataka kujitenga kwa sababu ya Uislaam wenu,. mimi sintokuwa nanyi na wala Waislaam wa bara ambao tunaamini Chadema ni chama cha watu wote. Wapo wengi tu Chadema waliosoma madrasa, sio lazima uwaone wewe wala hawana maonyesho!...tutafika tu usiwe na hofu....

Ha ha ha

Wewe ndio hujui siasa kweli, kwahiyo Bukoba CUF iliondoka kisa kaondoka Lwakatare?? mistake kupata wabunge ndio kila kitu unadhani uliza kuna wenyevit wa mtaa na kijiji wangapi Tanzania Bara nzima second after CCM..upo?

Chadema ni wimbo mpya na kupata wabaunge wengi safari haina maana CUF haitapata chaguzi zijazo? mistake (or rather wishingfull thinking)

Chadema cha cha Wakristo, hakina hata mwenyekiti wa mtaa maeneo ya waislam na zanzibar? wakristo na ukristo mtupu embu angalia wanavyo sema ovyo kuhusu madai ya waislam wa Tanzania na ku-support matamko ya maaskofu..lol (you can't fool people all the time)

CUF siyo chama cha waislam ni chama cha Watanzania wote; Zanzibar, Pemba, Lindi, Bukoba, Dodoma etc.. pia... kipi kigumu hapo kuelewa??
 
Sasa hili unalouliza ni swali au unatoa jibu? Ukiwa na akili angalau kidogo utajua kuwa CDM hawapo Zanzibar kwa sababu Wazanzibari ni wadini na sio kuwa CDM ni wadini. Kuwa na supporters wengi kutoka seminary za kikatoliki hakuwazuii binadamu wenye akili ya kupambanua mambo kuzipenda sera za CDM. Tungependa kuwa na supporters toka Muslim University of Morogoro lkn kaa ukijua kuwa mpk mtu afikie kuwa supporter wa CDM basi ana dalili za uelewa mkubwa wa mambo.

Naomba niulize swali: Hivi ukimuondoa Lipumba na Seif Sharif Hamad hakuna pair nyingine yenye akili na uwezo wa kugombea urais kwa tiketi ya chama chenu mpk ifikie sehemu mshindwa huyo huyo anayeburuzwa kila siku kuonekana kama ndio chaguo pekee?

Nini kitatokea endapo tukiwapa serikali halafu Seif na Lipumba wakatangulia kwa Allah kunywa wine na mademu? Je, na chama kitakufa na serikali kutawanyika?

Tatizo lako unafikiri siasa ni mchezo kama wa mpira. La hasha kwa Wazanzibari siasa ni nyenzo ya kutumikia maslaha yao. Sasa niambie nyie CHADEMA mna sera gani ambayo itawafanya Wazanzibari wajiunge nanyi?

CHADEMA mna chuki binafsi na Wazanzibari kiasi kwamba walichoamuwa wao nyie mnakibeza halafu mnataka wanachama, huoni kuwa hamna nafasi Zanzibar? Hebu jiulize katika kipindi chenu chote cha mapambano kipi mlichokiwekea sera kwa Mzanzibari?

Nyie wenyewe hamtambui Zanzibar halafu mnalalamika eti udini ndio unaokunyimeni kutambulika Zanzibar. Hivyo kukosa kwa CCM viti kule Pemba kunasababishwa na udini? Jee kuna uislamu wa namna mbili? moja wa Pemba moja wa Unguja?

Ama hili la viongozi hao hao ni uamuzi wa wanachama na iwapo huo ni udhaifu basi na iwe furaha kwenu na sio kulalamika. Unajuwa, ni kichekesho kulalamika mpinzani wako anapokuwa na timu dhaifu huku inakutowa kamasi au tusema kuwa hiyo combination ndio tishio hivyo mnapiga kampeni iondoshwe?
 
Lawama na Nwato zote hizo zinaletwa dharau yenu kwa wazanzibari na kuhisi kuwa uislamu ni uarabu. Uislamu ni imani na muislamu kama binaadamu mwengine anaasi lakini hatoki kwenye dini. Dharau na lengo la udini mbadala kwa Wazanzibri ndio linawafanya CHADEMA msipate wanachama. Bila shaka wapo wengi mliowapandikiza kuja kupambana na uislamu, pengine hao watakuwa wanachama wenu. Hata hivyo hebu nikupe somo kidogo. Siasa kwa Zanzibar si mchezo wa kujifundishia bali ni jambo liliopo ndani ya damu ya Wazanzibari wote. Huwezi kuwadanganya na wanapoona mwenzao anawaendea kinyume dini haiwi kizingiti cha kumtowa kwenye siasa, hatolewi dini,naomba ufahamu.
Sasa Hamadi Rashidi ametolewa kwenye CUF sio uislamu na hivyo anaweza akaenda pengine lakini kama Mzanzibari anaelewa kuwa siasa si mchezo wa mpira kuwa utanunuliwa na mashabiki waendelee kukushangilia.
Mkuu wangu ndivyo wanavyowafundisha hivyo... KUFUR inakuondoa ktk Uislaam na usipokuwa na Total submission kwa Mwenyezi Mungu ktk imani inakuondoa ktk Uislaam. Nimebiashana na watu pale K -Tea shop wakifikiria kama unavyofikiria wewe akaja Ustadh na kuwaambia hapana Dhambi yoyote haikuondoi ktk Uislaam. Kuasi dini haiwezi kukuacha Muislaam hiyo mkuu wangu rudi darasani maana pengine hujui maana ya kuasi..Mtume alisema tofauti baina ya Kafir na Muislaam ni Sala - hili wewe unaitafsiri vipi? -

Chadema hatupambani na Uislaam isipokuwa nyie CUF ndio mnapambana na Uislaam kwa kujaribu kututenga sisi wa bara na kutangaza Uzanzibar wenu mkisahau kwamba Bara wamejaa Waislaam na Wazanzibara. haya alituasa tena Mkristu Nyerere lakini kwa akili zenu mnayaona madogo. Leo mnamwondoa Muislaam mwingine kwa sababu tu kasema Seif ana agenda mbaya. - siri za chama!

Mnapoteza majimbo bara na bado hamsomi alama sasa imebakia kwamba hata Zanzibar kwenyewe intellectuals watawakimbia. Na wawakimbie mara ngapi maana nijuavyo mimi Wazanzibar wasomi wote wako CCM..Walalahoi wanaodanganywa na Udini ndio wamejazana CUF, bara tumeisha washtukia..
 
Wewe acha kujifanya ndio una akili sanaaaa. Kuwepo kwake DAR sio kwa shughuli za Umakamu wake wa huo mkoa wenu bali shughuli za CUF kitaifa. CUF taifa ni kwa Tanzania na huo umakamu wake unaishia huko Unguja na Pemba. Huku hatumtambui kwa hiyo bendera aliyokuja nayo bali ya CUF.

Ni jambo lipi linaloendana na kutia mikono mfukoni ndugu mtaalamu wa gestures?

Sawa kama wewe humtambui lakini naona analindwa na usalama wa Taifa sijui Mbowe nae hufanyiwa hivyo?

Hili la kujuwa utaamuwa wewe kwa kulinganisha hoja zako na zangu!
 
Hata sisi wenye akili timamu tunajua siasa wanazoendesha chadema; tunajua mna ajenda gani kuhusu zanzibar, tunajua mansukumwa na mna ajenda gani kuhusu uislam na waislam..

msidhani mnawaweza kuficha tena, too late bro

tudokeze basi mkuu wetu..binafsi mimi sijui kuwa kina Zitto wana ajenda gani
 
Mkuu wangu ndivyo wanavyowafundisha hivyo... KUFUR inakuondoa ktk Uislaam na usipokuwa na Total submission kwa Mwenyezi Mungu ktk imani inakuondoa ktk Uislaam. Nimebiashana na watu pale K -Tea shop wakifikiria kama unavyofikiria wewe akaja Ustadh na kuwaambia hapana Dhambi yoyote haikuondoi ktk Uislaam. Kuasi dini haiwezi kukuacha Muislaam hiyo mkuu wangu rudi radasani maana pengine hujui maana ya kuasi..Mtume alisema tofauti baina ya Kafir na Muislaam ni Sala - hili wewe unaitafsiri vipi? -

Chadema hatupambani na Uislaam isipokuwa nyie CUF ndio mnapambana na Uislaam kwa kujaribu kututenga sisi wa bara na kutangaza Uzanzibar wenu mkisahau kwamba Bara wamejaa Waislaam na Wazanzibara. haya alituasa tena Mkristu Nyerere lakini kwa kili zenu mnayaona madogo.

Mnapoteza majimbo bara na bado hamsomi alama sasa imebakia kwamba hata Zanzibar kwenyewe interllectuals watawakimbia. Na wawakimbie mara ngapi maana nijuavyo mimi Wazanzibar wasomi wote wako CCM..Walalahoi wanaodanganywa na Udini ndio wamejazana CUF, bara tumeisha washtukia..

Sasa kama CUF wanakimbia na wanachama si ingekuwa furaha kwenu chadema? mbona kila kukicha mko juu kuwaita majina??

Nafikiri wamewashika pabaya that is why mnaota CUF badala ya kuhangaika na CCM, otherwise uniambie mnahangaika na CUF kwasababu ya uislam wao? na nyie na ukristo wenu??
 
Mkandara hebu jiulize Muislamu anatoka mara ngapi kwenye uislamu na kurudi? Jee huyo Ustadhi wako alikwambia kuwa pale anapopita na kuhubiri swala wale wanaomfuata ana washahadiza tena ili kurudi uislamu? Pengine ungemuuliza huyo ustadhi wako kukufuru maana yake nin ni nini?

Tuwache hayo kwani kumbe wewe ndie mdini. Sijibu kwa niaba ya CUF lakini hivyo kwa akili yako iwapo CUF ni chama cha Kidini unafikiri ni rahisi kwa mtu kuacha dini yake?

Hivyo kushindwa CUF Bara si kwa udini kwani dini hazina uchaguzi. Ama kwa CHADEMA kuikosa Zanzibar ni kutokana na sera zao kuenda kinyume na maadili ya Wazanzibari.

Mwenyekiti mpiga Disco na Katibu anatoka Kanisani huku tayari kanisa lishachafua hali ya hewa Zanzibar, unategemea kitu tena?
 
Sasa kama CUF wanakimbia na wanachama si ingekuwa furaha kwenu chadema? mbona kila kukicha mko juu kuwaita majina??

Nafikiri wamewashika pabaya that is why mnaota CUF badala ya kuhangaika na CCM, otherwise uniambie mnahangaika na CUF kwasababu ya uislam wao? na nyie na ukristo wenu??
Mkuu wangu binafsi sina matatizo na CUF hata siku moja bali hawa viongozi wenu kina Seif na Jussa hawa sii waislaam wala Wazanzibar na sintowaheshimu hata siku moja maana nawajua agenda zao kama alivyosema HR.. Na kama unaona tunawafuata kwa uhasama wao ndio wamekwenda funga ndoai na CCM kama alivyofanya Karume halafu Jussa anatukana hadi kesho..

Na historia itamrudi kuna wajinga watasema Jussa na Karume hawakutaka Muafaka isipokuwa yule mkristu Makamba ndiye aliwalazimisha.. hamkosi sababu za kulaumu watu weninge kwa maamuzi yenu wenyewe. CUF kama CUF wana agenda sanwa na Chadema - kuwa na serikali tatu na Zanzibar inazo fursa za kutambuliwa kama sovereign country hatukuwa na tatizo hilo lakini baada ya hawa kina Seif kuona wanazeeka mali hawana, ukubwa wanautaka kabla hawajaingia kaburini wakakubali kukiuza chama.

Na sababu kubwa Chadema walitoa suggestion HR asimame na Dr.Slaa badala ya Seif Hamad..hapo Seif alikuwa mwekunduuu na toka siku hiyo CDM na HR maadui wake..kwani chuki ya Seif na Chadema imeanza leo mkifikiria kwamba HR anautaka ukatibu mkuu?.. tatizo ni Seif ambaye kwa malingo hata bila aibu anakuja na bendera yake mikono mfukoni kutuonyesha yeye ndiye makamu wa rais. Karume wala Shein hawajafanya hivyo hata siku moja leo unamtetea mhuni huyu kwa jina la CUF na Uislaam!..Tema mate chini!
 
Ha ha ha haya mambo ya ndani sasa, embu wewe nidokeza CUF wanaendesha siasa gani kama ulivyo sema hapo juu??
sasa mkuu wangu unaniulizaje swali ili hali hujanijibu swali langu..au nielewe kuwa huna jibu na ulitunga tu ili kunogesha ukumbi?
 
Ngekewa,
Symbolize ya bendera huwekwa menzani pale pembeni au mbele yake na maadam kulikuwa na viongozi wa juu wa chama kutoka BARA ni lazima uweke pia bendera ya bara ktk mkutano wa chama ama huweki zote - inapepea bendera ya chama tu.. Huwezi kupeperusha juu ya jukwaa bendera ya Zanzibar ndani ya nchi nyingine ukasahau kuiweka ya bara ama ukaona hakuna umuhimu. Hawa ni magaidi wa Muungano Na hasa huyo Jussa, na wamefanya hivyo makusudi (habari tunazipata haraka sana kuliko nyie) na ukijumlisha yote haya unapata kile ambacho wengi wanajiuliza hadi wameshindwa kubeba wala kuvaa jezi za CUF..

Mkandara hivyo uliona wapi bendera ya Rais ikawekwa mezani? Na hao Bara nao walileta Makamo wa Rais hata ilazimike nao wawekewe bendera? Kubwa huo ni mkutano wa Kichama lakini wadhifa wa Sefu upo palepale hivyo stahiki zake atapewa.
 
Picha nilizoona hapo juu zimedhihirisha kuwa Hamad Rashid alikuwa sahihi!! Maalim Seif hana mpango na CUF ya Tannganyika, anahitaji CUF ya Zanzibar itakayo mwezesha kuwa Rais au Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Picha hizi zinaonyesha CUF Zanzibar walipofanya mkutano wao pale Manzese. Tusubirie Mkutano wa CUF Tanzania bara utakao peperusha bendera za CUF na Bendera ya Taifa na kuhutubiwa na viongozi wa CUF bara akiwemo Lipumba na HR
Kwani Hamadi wakati ule mlipomnyima uwaziri kivuli mlikuwa hamjuwi kuwa yeye ni CUF wa Bara?
 
Mkuu wangu binafsi sina matatizo na CUF hata siku moja bali hawa viongozi wenu kina Seif na Jussa hawa sii waislaam wala Wazanzibar na sintowaheshimu hata siku moja maana nawajua agenda zao kama alivyosema HR.. Na kama unaona tunawafuata kwa uhasama wao ndio wamekwenda funga ndoai na CCM kama alivyofanya Karume halafu Jussa anatukana hadi kesho..

Na historia itamrudi kuna wajinga watasema Jussa na Karume hawakutaka Muafaka isipokuwa yule mkristu Makamba ndiye aliwalazimisha.. hamkosi sababu za kulaumu watu weninge kwa maamuzi yenu wenyewe. CUF kama CUF wana agenda sanwa na Chadema - kuwa na serikali tatu na Zanzibar inazo fursa za kutambuliwa kama sovereign country hatukuwa na tatizo hilo lakini baada ya hawa kina Seif kuona wanazeeka mali hawana, ukubwa wanautaka kabla hawajaingia kaburini wakakubali kukiuza chama.

Na sababu kubwa Chadema walitoa suggestion HR asimame na Dr.Slaa badala ya Seif Hamad..hapo Seif alikuwa mwekunduuu na toka siku hiyo CDM na HR maadui wake..kwani chuki ya Seif na Chadema imeanza leo mkifikiria kwamba HR anautaka ukatibu mkuu?.. tatizo ni Seif ambaye kwa malingo hata bila aibu anakuja na bendera yake mikono mfukoni kutuonyesha yeye ndiye makamu wa rais. Karume wala Shein hawajafanya hivyo hata siku moja leo unamtetea mhuni huyu kwa jina la CUF na Uislaam!..Tema mate chini!

Kama unge- declare mapema kwamba huna shida na CUF except Maalim Seif na Jussa ningekuelewa; lakini ulipoanza kuwakandia CUF eti wanakumbatia dini, kama ambavyo chadema inavyokumbatia wakatoliki mbona mjadala ungeshaisha zamani?? kwani kwangu mimi mtu yeyote anayeleta dharau na uislam na waislam hana nafasi hata kidogo kwenye maisha yangu..

Mkuu hata mimi sina shida na chadema isipokuwa viongozi wake Dr. Slaa na kina JJ Mnyika ambao kutwa kucha kazi kuchangisha harambee za kanisani as if wamechaguliwa kueneza ukristo...

Tuko pamoja kama ni matatizo ya viongozi na si chama ..tchao
 
Mkandara hebu jiulize Muislamu anatoka mara ngapi kwenye uislamu na kurudi? Jee huyo Ustadhi wako alikwambia kuwa pale anapopita na kuhubiri swala wale wanaomfuata ana washahadiza tena ili kurudi uislamu? Pengine ungemuuliza huyo ustadhi wako kukufuru maana yake nin ni nini?
Tuwache hayo kwani kumbe wewe ndie mdini. Sijibu kwa niaba ya CUF lakini hivyo kwa akili yako iwapo CUF ni chama cha Kidini unafikiri ni rahisi kwa mtu kuacha dini yake? Hivyo kushindwa CUF Bara si kwa udini kwani dini hazina uchaguzi. Ama kwa CHADEMA kuikosa Zanzibar ni kutokana na sera zao kuenda kinyume na maadili ya Wazanzibari. Mwenyekiti mpiga Disco na Katibu anatoka Kanisani huku tayari kanisa lishachafua hali ya hewa Zanzibar, unategemea kitu tena?
Kushahadia pekee haikurudishi ktk Uislaam ni sawa na kukubali (shahada) ulipotoka na sasa unarudi ktk njia ongofu..Lakini kama hutajisalimisha kwa mola wako kwa kufuata njia ongofu ati kwa sababu tu ulishadia unajidanganya mwenyewe..

Lazima ufuate Uislaam unavyotakiwa hakuna excuse zaidi ya zile zilizoorodheshwa... hao Wa Libya na Wasyria utawaita waislaam walioasi wakati wanafanya kufur kubwa tuuite ati uasi.. Huwezi kuacha ibada kubwa ukisema kesho nitarudi ktk Uislaam Mwenyezi Mungu sii wa kuchezea kama unaingia kuoga maji ukichafuka. Na ndio maana mtume akasema kama wewe husali huna tofauti na Kafir ikiwa na maana zipo sifa zinazokufanya wewe uwe Muislaam na neno Total submission lina maana kubwa zaidi ya kutoa shahada. huapishwi uraia mkuu wangu hii ni imani ya Mungu, dini sio uraia.

Pili maana ya shahada ni kushuhudia na kukubali kwamba hakuna Mola apaswaye KUABUDIWA kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na usipomuabudu shaha yako haina kazi maana huyo Ustadhi ni shahidi tu wa kwamba uliukubali Uislaam kama hutautuafata hiyo ni kesi yako na huyu siku ya siku atakuwa shahidi dhidi yako wewe. Hakuna sababu ya huo Ustadhi maana hawa watu hawakuniamini mimi hivyo wewe chukua darsa kutoka kwangu. Bongo mambo mengi sana mnadanganyana..
 
Back
Top Bottom