Picha: Mkutano wa chadema huko Karatu...

Huyu kijana matata sana, Ana mvuto wa ajabu kwenye kujieleza, dr. Slaa was good ila baada ya kumpata Huyu mama aliyenae binafsi naanza kupata wasi wasi na uwezo wake wa kuhimili unyumba na kazi za chama katika Muda huu, heko zzk msaidie slaa mjenge chama.

kama wewe ni kamanda naomba umuheshimu dr. Slaa, uheshimu na kutambua juhudi zake na mchango wake mkubwa ktk kukiimarisha cdm tafadhali!
 
Ushauri kwa Wapenzi na Wanachama wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo CHADEMA nimefurahi sana kuona vingozi wetu wanafanya juhudi kubwa kukitangaza chama Tanzania nzima ushauri wangu wa bure kwa muda huu Tanzania ni kubwa ssana Kijiografia kuifikia hadi uchaguzi mkuu 2015 ambapo watazania tuliokata tamaa tunategemea CHADEMA kuchukua Dola na kuwakomboa wanyonge ambao kwa miaka 50 tunaishi maisha ya kubahatisha,Viongozi wangu wa chama muda huu tufanye yafuatayo
1.Tujaribu kuitembelea Tanzania kuna maeneo makubwa sana wakati huu wanahitaji kuwaona viongozi wao wakuu ambao wamejiandaa kuwakomboa.
2.Mikoa kama Arusha,Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Mara, Kigoma, tupunguze safari za huko na mikutano ya hadhara kwavile huko tayari tumeisha pata Uungwaji mkono tujaribu kuitembelea mikoa mingine ambapo watu wanashauku ya kuwaona viongozi wao ambao wanaweza kuwaondoa kwenye minyororo ya CCM viongozi mnapopenda kila siku kufanya mikutano ambapo tayari chama kina mtaji basi tutambue ya kwamba hasimu wetu atawkumbatia hao ambao hatuwafikii na kujitambulisha kwao. Nawaomba chonde chonde Dr, Slaa,Mbowe na timu yako zingatia ushuri huu.
 
Shukrani kwa picha. Picha inatoa ufafanuzi zaidi kuliko maneno.
Hapana mkuu, tumeshuhudia mikutano ya CCM ambayo ilitkuwa inahutubiwa na Mwigulu, Lusinde, NAPE inakuwa na umati mkubwa wa watu lakini unakuta kilichoongelewa hapo ni Matusi, vijembe na maneno yasiyofaa na kuwa na tija na maendeleo ya taifa hili ndo maana nashauri unapoweka picha ni vizuri ukaweka pia na kilichoongelewa katika mikutano na hapo taarifa yako itakuwa kamili.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom