Picha: Mh:mwigulu nchemba aunguruma kata ya themi jijini arusha kampeni za udiwani.

Mtela Mwampamba

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
537
347
Naibu katibu mkuu akiwasili kwenye viwanja vya kata ya Themi Jijini Arusha kwenye kampeni za Uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Themi.Huu ni mfululizo wa mikutano ya kampeni anayoifanya Mh.Mwigulu Nchemba jijini Arusha kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo na inarejesha kata kwenye himaya yake.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mh.Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM waliofika kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi kata ya Themi Jijini Arusha.

Aliyekuwa diwani wa CHADEMA Bi.Rehema Mohamed ambaye ameamua kujiunga na CCM ilikutimiza ndoto zake za kuwaletea maendeleo ya wanaarusha.Bi.Rehema amesema"Nilikuwa chadema na nimekuwa Diwani kwatiketi ya CHADEMA ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha.Katika kipindi changu chote cha udiwani CHADEMA walizuia kwenda kwenye vikao vya halmashauri kujadili maendeleo ya Halmashauri yetu.Muda wote walikuwa wanasisitiza tusimtambue meya,Kwa hiyo wana Themi hao chadema hata mkiwapa diwani hii leo ajenda yao ni kutomtambua meya,hawana ajenda ya maendeleo hata moja.Hivyo basi nawaomba wana Themi mtumie sanduku la kura kuhakikisha tunaipa ushindi CCM chama chenye sera zinazoonekana na zinazotekelezeka.Mchagueni Victor Mkolwe kwa maendeleo ya Kata ya Themi

Huyu alikuwa ni msaidizi wa Mbunge wa Arusha Mjini jina lake maarufu ni NIKO,Niko amejiunga na CCM baada ya kuchoshwa kuendeshwa kama punda mbele ya Lema.Niko anaeleza kuwa yeye tangu awe CHADEMA hawajawahi kaa chini kupanga namna ya kufanya maendeleo sehemu yoyote ndani ya jiji la Arusha,lakini amekuwa akiongoza vikao chini ya amri ya Lema vya kufanya vurugu,kuandamanisha watu na kuandaa vijana wa kuvamia mikutano ya CCM.Anasisitiza nipo CCM kwa sababu ni sehemu salama,CCM ni chama chenye mfumo uliokamilika lakini sio CHADEMA chama cha mtu mmoja anayetoa amri kama mfalme.Hivyo amewaomba wana Themi kumpigia kura mgombea wa CCM na kuhakikisha kura zinalindwa kikamilifu.

Diwani wa CCM kata ya Monduli Mjini Ndugu Isack Joseph akihutubia mamia ya wananchi kata ya Themi jioni hii ya tar.9/06/2013.Diwani huyu amesema ameshapata taarifa za Lema kupeleka vijana Monduli kwa wamasaai kwenye kata ya Uchaguzi,Vijana hao wa CHADEMA anawarubuni wamasaai kwa sukari na Tsh.10000 ilikununua shahada za kura.Diwani Isack ameonya kuwa CHADEMA wakiongozwa na mbungewao Lema waache mara moja mchezo huu mchafu,sehemu pekee ya kushindana ni kwenye jukwaa na sio kurubuni wananchi.Amewaomba wana Themi kufanya maamuzi sahihi ya kumpigia kura mgombea udiwani kijana Victor Mkolwe

Mjumbe wa Halmashauri kuu (MNEC) alikuwepo kumuombea kura Victor Mkolwe mgombe udiwani kata ya Themi kwa tiketi ya CCM.Mjumbe huyu wa halmashauri kuu amewabeza watu wanaosema CCM ni chama cha wazee,amehoji yeye ni Mzee?Au victor Mkolwe ni Mzee?

Naibu katibu mkuu wa CCM,Mh.Mwigulu Nchemba amehutubiwa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Themi.Mh.Mwigulu Nchemba amesema hakuna sababu ya Wanathemi kumpigia kura mgombea wa upinzani yeyote yule kwa sababu Upinzani hawana sera ya kutekeleza,wanategemea serikali ya CCM kupitia sera zake ndio ifanye maendeleo kata ya Themi.Pia amesisitiza kuwa swala la uchaguzi mdogo kama huu ni matokeo ya siasa za kibabe za CHADEMA,Wamefukuza madiwani kwa sababu za kipuuzi,hekima haikutumika kwa sababu ni Arusha.Mbona mbowe alikimbilia kusuruhisha mgogoro karatu wa ufisadi wa maji?kwanini hakufukuza?Pia amehoji mbona moshi walisuruhisha hawakufukuza?Jibu ni kwamba karatu yupo Dr.slaa,Moshi yupo Mzee Mtei mmiliki wa CHADEMA.Lakini Arusha madiwani walifukuzwa kwa sababu tu Arusha hakuna watu wa kuhoji.je wana Arusha hamuwezi kuhoji?.Diwani alipochaguliwa alikuwa mali ya CHADEMA au wananchi?Mbona walipofukuzwa hamkuombwa ridhaaa ya kuruhusu wafukuzwe?.Hii ni dharau kwenu na kwa wananchi wote.Hivyo tambueni kwamba msipo mchagua diwani wa CCM mtarudi tena kwneye uchaguzi kwa sababu huyo wa upinzani atafukuzwa tena.Sioni sababu ya wana Themi kuendelea kuishi bila Diwani,Jambo jema na la kimaendeleo ni kumchagua mgombea wa CCM kijana Victor Mkolwe.

Mgombea udiwani kata ya Themi jijini Arusha kwa tiketi ya CCM Ndugu Victor Mkolwe,Kitaaluma huyu ni Mwanasheria.Victor Mkolwe amewaomba wana Themi kumpigia kura za ndio kwa wingi iliaweze kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi huu.Amesema atahakikisha anafanya kazi ya kurejesha maendeleo kwa kasi kata ya Themi kwa sababu tangu mwaka 2010 kata imekuwa haina diwani hai.Hivyo yeye ameamua kuchukua nafasi hiyo ilikutimiza ilani ya CCM na sera za chama chake juu ya maendeleo ya kata ya themi na jiji la Arusha.

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania bara Mh.Mwigulu Nchemba akimnadi mgombea wa udiwani kata ya Themi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Ndugu Victor Mkolwe.Mh.mwigulu Nchemba amewaomba wana Themi na wapenda maendeleo wote kumpigia kura mgombea huyu wa CCM.Amesema elimu ya Victor Mkolwe na ujana wake unahadhi ya kuwaletea maendeleo wana themi,Pia kumchagua Victor ni sawa na kuruhusu milango ya maendeleo kufunguka kata ya Themi kwa sababu hawatasikia tena maandamano au vurugu zozote zinazowakera siku za karibuni kutoka CHADEMA.



Mkutano umeshamalizika hapa kata ya Themi jijini Arusha,wananchi wanarejea makwao huku wakiwa na mwamko wa kupiga kura kwaajili ya CCM kwanza.

CCM ni chama cha wazee?Mtoto huyu amehudhuria mkutano wa kampeni kata ya Themi jioni ya leo akiwa ndani ya vazi na bendera ya CCM.(Picha zote na HM)

 
Mwambie Lameki aache uchafu. ndevu kama ---------&*(_*&(__(. au kakosa hela yakwenda kuzinyoa. mwambie huo ni uchafu
 
mbona sijamuona yule jamaa mliye mwagia tindikali kisha mnasingizia wengine ili mpate huruma ya wapiga kura? hahahahahahaaaahahahaa.
 
Umechemsha mdogo wangu mbona picha za wahudhuriaji ni kizungumkuti? A city hakuna mtu wakumsombelea na lory kama kokoto mumshukuru mungu angalau mmewapata hata hao 50 au 80
 
Naona this time umekosa picha za Oblique eeh? kwa tafsiri tumeshajua kilichojiri.
 
Kwetu arusha si wanafki....mtaona mtakachokipata siku hiyo ya uchaguzi...!subirini kipigo kikali....
 
Nimeona CHADEMA kimetajwa mara 11 lakini sijaona ikitajwa sera hata moja zaidi ya maneno ya ujumla eti kuleta maendeleo.Ngoja tusubiri wapiga kura wenyewe watakapofanya maamuzi!
 
"mwigulu"..."nchemba"..."themi".."arusha"....na wewe ni Mwalimu wa Kiswahili kitaaluma,lakn bado hujajua kutofautisha kati ya wapi utumie herufi kubwa na wapi ndogo!Jf ni shule pia..iwe mwisho kufanya udhalilishaji wa maandishi namna hii...Uandishi wako unaakisi nini kilicho kichwani mwako,na ni bora hujaenda kufundisha...nyie ndo walimu mnaofeli hata mkipewa mitihani wanaofanya wanafunzi wenu...Besides:Hakuna kipya ktk bandiko lako..ni maneno yaleyale!!Mwisho:UKOME KUANDIKA "arusha"...wewe n mwalimu wa Kiswahili
 
Tusubiri kipenga kipulizwe maana Nchemba na jeshi lake la vurugu watajifungia ndani kwa aibu
 
Huyo Victor Mkolwe ni rafiki yangu sana na anajulikana kwa jina la mkemia, ni kweli kuwa ni mwanasheria lakini mwenyewe anakiri chadema haishikiki!
Ni kijana wa mkemia mkuu wa tanzania breweries

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Vipi Shonza hajatokea hapa Mwanawane. Matunda ya usaliti yameoneka kwa mwenzio bado wewe. Nye ni kondo kumbe Moyoni Chui. Acha kuganga ganga.
 
Size ya fonts kubwa sana kibaraka Mtela!! mbona unatumia nguvu hivyo??? hivi ndugu yangu Mtela uko CCM gani kati ya hizi???
Sitta....
Edu Lowassa........
Membe........
Wassira........
Nchimbi.........
Wazanzibar........
Ngelejaza........
Sumaye.........
Tafadhali naomba majibu kwani kunafununu kuwa chama kinapasuka rasmi jumamosi ijayo
 
Back
Top Bottom