Picha: Mazishi ya Regia Mtema Ifakara

Shukrani nyingi kwako Finest umetuwakilisha kikamilifu. Nasi tunaamini tumeshiriki vyema katika msiba. Ubarikiwe sana. Once again Regia upate pumziko la milele, Uende salama dada yetu, mdogo wetu, mtanzania mwenzetu, mwanetu na zaidi SHUJAA WA KWELI. Hatuna namna ya kukushukuru Regia kwa jinsi gani ulijitolea kuitetea haki ya kila mtanzania ulitamani kuiona Tanzania yenye mabadiliko, Tz. iliyokombolewa lakini bado tunasema asante na TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
 
Finest tunashukuru kwa picha na kazi nzuri hakika ulituwakilisha vyema kwenye msiba huu....Dada yetu mpendwa Regia..R.I.P
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina, kifo cha huyu dada inapaswa tujifunze kitu kikubwa sana kisiasa kwa ile mvua kubwa sana iliyokuwa inanyesha then watu wakaendelea na ratiba ya mazishi bila kukimbia, tena wakiwa wa ccm na vyama vingine ni dhahili kuwa alikuwa ni mwanasiasa aliye komaa na asiyefungamana na upande wowote isipokuwa walipo wananchi, ie bila kujali itikadi za vyama vyao.
 
hawa ccm kila wakikaa wanacnzia hivi huwa wamevimbiwa???cheki ndugai hapo kwenye picha za mwanzo!!!
:yawn::embarassed2::lol:
 
Leo tunapoadhimisha miaka mitano toka ututoke Dada Regia Mtema, nakuombea Mungu akupokee katika makao yake ya milele na ukajumuike na watakatifu wote waliotangulia. Sisi pia tunaomba wakati wetu utakapofika utukute katika hali ya usafi wa moyo na utayari wa kutwaliwa.

Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.
 
Huyu madame ndie aliyesaini kadi yangu ya kujiunga na chadema mungu ampokee na mwanga wa milele amwngazie apumzike kwa amani amina
 
Back
Top Bottom