Picha matukio: Ziara ya BAVICHA Mkoani Mpanda iliyomliza (PM) Pinda

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kupitia viongozi wa Baraza la VIjana Taifa la chama hicho (BAVICHA) kimefanya ziara ya kichma katika mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe na Katavi ambapo pamoja na mambo mengine, ziara ilipofika Mkoa wa Rukwa iliweza kuamsha wananchi kwa kiwango cha kumshitua Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama alivyonukuliwa Bungeni akijibu swali la Mbunge wa Same, Mama Anne Kilango alietaka kujua Serikali inakauli gani kuhusu mikutano ya CHADEMA hasa jimboni.

Ziara hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa Mwenekiti wa BAVICHA, John Heche na Katibu wake, Deo Mushi. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio mbalimbali ya mikutano ya hotuba, mazungumzo na wananchi na kujua kero zao, kufungua matawi n.k
View attachment 60448
Hapa Heche anaonekana akipokea maelezo ya wananchi kuhusiana na tatizo la maji linalowakabili. Picha ya kwanza na ya pili ni shida ya maji ndani ya Jimbo la Waziri Mkuu
View attachment 60449

View attachment 60454

View attachment 60458

View attachment 60459

View attachment 60456

View attachment 60460
View attachment 60463
 
Yaani badala ya Pinda kuhangaika na maji anahangaika kuwatafutia maisha bora AGRISOL!!! Aibu!
 
Ushindi wa viongozi wa CCM unategemea umasikini wa sehemu walipo wananchi. Hapa Pinda anategemea 2015 ataenda kuwapa wananchi wa jimbo lake t-shirt ya njani na kijani wamchague tena.
 
Ushindi wa viongozi wa CCM unategemea umasikini wa sehemu walipo wananchi. Hapa Pinda anategemea 2015 ataenda kuwapa wananchi wa jimbo lake t-shirt ya njano na kijani wamchague tena. Waziri mkuu, mbunge miaka, wananchi wake hawana maji eti yeye ni mtoto wa mkulima
 
Ndugu wanJF,
Hivi karibuni Viongozi wakuu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa, Kamanda John Heche(Mwenyekiti) na Kamanda Deogratias Munisi(Katibu) walifanya ziara katika mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini katika muendelezo wa M4C.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya mikutano mbalimbali iliyofanyika katika mikoa hiyo kuanzia Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na Iringa.
Pamoja na mikutano ya hadhara pia kulikuwepo na shughuli za uzinduzi wa ofisi mbalimbali za Chadema katika maeneo mbalimbali walikopita pamoja na kupokea wanachama wapya.

Mikutano hii ndiyo iliyowatisha waziri mkuu Pinda, Spika Makinda pamoja na wabunge kadhaa wa ccm hadi kufikia hatua ya kulalamika. Wananchi wa Mpanda, Sumbawanga mjini, Tunduma pamoja na Njombe walijitokeza kwa wingi sana kuwasikiliza makamanda hao wa Bavicha, na kujiunga kwa wingi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Wananchi wakiwa wanasikiliza kwa utulivu na umakini viongozi wa Bavicha wakimwaga sera.



Mwenyekiti wa Bavicha Taifa Kamanda Heche(kushoto) akikata utepe kuzindua moja ya ofisi za Chadema zilizozinduliwa katika ziara yao, kulia ni Katibu wake Munisi.


Kamanda Heche akiwahutubia wananchi kwa hisia kali sana.

 

Attachments

  • h1.jpg
    h1.jpg
    154.1 KB · Views: 2,453
  • h2.jpg
    h2.jpg
    91.6 KB · Views: 2,067
  • j1.jpg
    j1.jpg
    66.6 KB · Views: 2,043
Hadi huu mwaka uishe watakuwa washapata presha sana hawa magamba manake ukombozi upo katika spidi ya ajabu sana na hakuna kiumbe wakuweza kuzuia hili kiukweli kabisa
 
MMh Vijana wa Bavicha kweli wamekomaa kama wanaweza kukomandi audience kubwa hivyo duh wananchi wameanza kuelewa sanaa tuu ukombozi ni sasa
 
OMG!
Mbona watamuua Mfipa wa watu kwa presha!!?
Ogopa mtu kimbaumbau akipata pressure!!
 
Nimemuomba invisible anisaidie ku-upload picha ili wadau muweze kuona ni kiasi gani vijana wa Chadema wameweza kukusanya mamia ya wananchi kuwasikiliza.

Bila shaka mtashuhudia kuanzia Mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe na Iringa.
 
Mnawachanganya wananchi. Pinda ni mkatoliki na cdm chama cha kikatoliki. Waache lipi wafuate lipi?
 
Hivi yule kibaraka wa Shibuda,makamu mkiti Bavicha Juliana Shonza yuko wapi siku hizi? Tangu siku ile amesoma Tamko lililoandaliwa na Shibuda naina kapigwa PIN ya nguvu.Chezea CDM wewe...
 
Hivi yule kibaraka wa Shibuda,makamu mkiti Bavicha Juliana Shonza yuko wapi siku hizi? Tangu siku ile amesoma Tamko lililoandaliwa na Shibuda naina kapigwa PIN ya nguvu.Chezea CDM wewe...

Hata mimi sijamsikia tena tangu siku alipotoa tamko la shibuda. Lakini yuko busy kwenye mafesibuku si unajua kule ndiko kimbilio la wengi wasioweza mikiki mikiki.
 
Back
Top Bottom