PICHA: Magari yaliyojaza mkutano wa CCM - Chadema Square (Jangwani)

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Haya ni baadhi ya mabasi yaliyobeba watu leo kuelekea kwenye mkutano jangwani leo.

j2.jpg
 
Attachments

  • MABASI CCM.jpg
    MABASI CCM.jpg
    18.2 KB · Views: 367
sasa ww ulitaka wanachama wake waje kwa mguu?pili tambua ccm ni taifa kubwa na ina matawi mengi hapo mjini wamekodisha magar waende kwny mkutano wao unalalama du wamikumbo bwana.hv unajua dar inapopulation kubwa gani?fikiri kabla ya kukurubuka.
 
Hiyo ndiyo iliyoleta funika mbaya pale Jangwani, kwani huo usafiri ulioonyeshwa ni sehemu ndogo tu ya magari mengi yaliyoleta watu pale Chadema Square.

SAM_2395.JPG

SAM_2396.JPG
 
sasa chama kinachotawala bado mnataka wanachama wake wapate tabu hata ya usafiri? Watakuwa hawana tofauti na migambo sasa
 
sasa ww ulitaka wanachama wake waje kwa mguu?pili tambua ccm ni taifa kubwa na ina matawi mengi hapo mjini wamekodisha magar waende kwny mkutano wao unalalama du wamikumbo bwana.hv unajua dar inapopulation kubwa gani?fikiri kabla ya kukurubuka.

Tunajadili tofauti ya mkutano wa Chadema na CCM. Chadema watu walifika wenyewe kwa usafiri wao na kufanya umati ule. CCM bila usafiri huo je idadi ingekuwaje pale Chadema Square?
 
Nyie mnaoshabikia eti chama tawala wanachama wapewe usafiri, sijui sio migambo nk, kwanini muwasafirishe kipindi hiki? Kipindi cha nyuma wakati wa mwinyi na hata mkapa mlikuwa hamuwasafirishi je walikuwa migambo? Hata wanachama wenu wenyewe hawataki tena kuja kwenye mikutano ni wazi mmefulia na hampendwi na wanachama wenu. Subirini mtaona nguvu ya watu maana yake nini!
 
CCM Mabwe Pande haikubaliki, watu wanateseka na kuishi maisha ya dhiki na taabu, walituahidi kutujengea nyumba, jana wameturuka. Ni nani mwenye hamu na CCM?
Hilo gari halijatokea Mabwepande, wamedanganya umma
 
Walioandika na kutundika hilo bango si wananchi wa Mabwepande bali ni akina Nape
 
Huo ulikuwa mradi wa Nape ili kuonyesha anafanyakazi vizuri, kama kweli wao ni wazalendo waeleze wananchi kiasi cha fedha kilichotumika kufanikisha huo mkutano kama haitakuja bill. kadhaa, wakati umeme ni wa kubahatisha na maji ndiyo usiseme.
 
sasa ww ulitaka wanachama wake waje kwa mguu?pili tambua ccm ni taifa kubwa na ina matawi mengi hapo mjini wamekodisha magar waende kwny mkutano wao unalalama du wamikumbo bwana.hv unajua dar inapopulation kubwa gani?fikiri kabla ya kukurubuka.

Tatizo chama kinalazimaka kukodi magari na bado kinatoa posho kulazimisha watu wapande hayo magari! Hilo ndiyo tatizo, wangekuwa wanachama kwa hiyari yao wanakodi bus na kujilipia wenyewe hilo halina shida.
Ushaidi wa kuletewa bus na kulipwa ni hapa tawini kwangu posho ilianzia 2000 mpaka 5000
 
Back
Top Bottom