PICHA: Maandamano ya CHADEMA Mwanza

Nimeipenda hiyo iulu chai bure bei ya sukari utaijuaje mjomba???? watu wamechoka kwa kweli
mabango yote yana ujumbe mzito lk hilo la ikulu chai bure ni kiboko huko tunakoenda chai watu watakunywa siku za sikukuu tu.hayo ndo maisha bora wandugu
 
Mimi naamini na nitaendelea kuamini kwamba maandamano yatakayoleta MABADILIKO YA KWELI na ya KUDUMU ni yale yatakayoandaliwa na WANANCHI wenyewe bila kuwahusisha WANASIASA. Vinginevyo tuendelee kufanya hizi sinema zisizo tofauti na FIESTA zinazoandaliwa na CloudsFM.

Safari ya kilometre 1,000 ndugu huanza na hatua moja. Haya ni maandalizi watu watafika huko unakokutaka wewe ipo siku. Haya maandamano yanayofanywa na wanasiasa yanasaidia kutia chachu kwenye mioyo ya watu! Hivyo amini tu kwamba ipo siku watu wataingia mitaani ingawa hilo hatuliombei kwa nchi yetu. Acha haya maandamano ya wanasiasa yawatie watu ujasiri na watafanikiwa!!
 
Baadaye tuwaulize viongozi wetu wa CHADEMA gharama zilizotumika kuandaa fiesta hii. Ruzuku yao ambayo ni kodi zetu imepanda sana baada ya kupata Wabunge, Madiwani wengi na kura nyingi za Urais. Fedha hizi zinapaswa kutumika hivi?
 
Mimi naamini na nitaendelea kuamini kwamba maandamano yatakayoleta MABADILIKO YA KWELI na ya KUDUMU ni yale yatakayoandaliwa na WANANCHI wenyewe bila kuwahusisha WANASIASA. Vinginevyo tuendelee kufanya hizi sinema zisizo tofauti na FIESTA zinazoandaliwa na CloudsFM.

WANASIASA siyo WANANCHI?
 
Limenifurahisha zaidi hilo bango linalosema 'Kikwete nenda Libya, Gadafi njoo Tanzania'
 
WANASIASA siyo WANANCHI?
Ni wananchi ambao kila wanachoandaa ni kwa manufaa na maslahi yao kwanza. Ninachomshukuru Mungu ni kuwa vyombo vyetu vya dola vimeanza kuelewa kuwa maandamano kama haya hayana madhara kwa yeyote. Hakufa Mwananchi wa kawaida MZA.
 
Baadaye tuwaulize viongozi wetu wa CHADEMA gharama zilizotumika kuandaa fiesta hii. Ruzuku yao ambayo ni kodi zetu imepanda sana baada ya kupata Wabunge, Madiwani wengi na kura nyingi za Urais. Fedha hizi zinapaswa kutumika hivi?

  1. Moja wapo ya sabau zilizofanya wananchi wasichague kwa wingi zaidi vyama vya upinzani, ni kwa kuwa HAVIVUMI
  2. Moja wapo ya sababu zilizofanya wapiga kura waipigie zaidi CCM, ni kwa sababu INAVUMA
  3. Mojawapo ya sababu iliyoifanya CHADEMA iongoze katika kura zaidi ya vyama vingine vyote vya upinzani ni kwa sababu ILIVUMA kuliko vingine
  4. Mojawapo ya vitu vitakavyoendelea kuiweka CHADEMA juu, ni kwa kuendelea kUVUMA
 
Nashukuru Sana kwa picha tuliombali tunapata hamasa sana kwa kuona mambo mabalimbali kama haya!! Tumeamua kubadilika
 
Ni Hakika kama Nyerere angefufuka leo angefurahi kuona vijana wenye hari na nchi yao wakidai uhuru wa kweli kama vile yeye alivyo dai kwa wakoloni.

Hongereni Mwanza kwenu hapakuwa na taarifa za kiintelijensia maana mngekiona kama Arusha. Naamini hadi sasa kwa Kanda yote ya Ziwa hapatakuwa na shida! Mungu na Awabariki sana, MUNGU Ibariki Tanzania na watu wake!
 
hapa kwaumbali nahanza kuamini kuwa watanzania wamechoka !!!!!!!ongereni chadema kwakulitambua hilo
 
Baadaye tuwaulize viongozi wetu wa CHADEMA gharama zilizotumika kuandaa fiesta hii. Ruzuku yao ambayo ni kodi zetu imepanda sana baada ya kupata Wabunge, Madiwani wengi na kura nyingi za Urais. Fedha hizi zinapaswa kutumika hivi?

Ni sawa Kabisa na hii ndiyo elimu kwa umma, watu wajue haki zao, nakumbuka Dr aliahidi kuzunguka Nchi nzima akitoa Elimu ya Uraia watu wajue haki zao za msingi. Unajua Ukienda kule kwetu masaini utakuta tunalalilia Ngozi ya Ng'ombe na hatuoni kuwa ni shida na hayo ndo maisha ya Umasaini kwa sababu hakuna aliyekuja kule masaini na kuleta Godoro la TANFOAM, ikiwa mtu atalileta ndipo tutaacha Ngozi na kujua kuwa tulikuwa tunateseka, lakini wewe ukipewa Ngozi ya Ng'ombe huwezi lalilia sababu unayo elimu na unaifahamu TANFOAM na utamu wake. Kwa maandamano kama haya ni wengi wanaerevuka na kujua kweli na kweli itawaweka huru!
Mbarikiwe na Bwana na usiwe mtu wa kutapika hadharani!
 
Eeh, Tanzania, akili za watu zimefunguka, Hongera sana watu wa mwanza.

Mwaka huu usiishe, tuing'oe ccm kwa nguvu ya umma, tumechoka chama kimoja kinaongoza nchi na kufichiana ma-dhambi mpaka lini.

Pipooooz...
 
  1. Moja wapo ya sabau zilizofanya wananchi wasichague kwa wingi zaidi vyama vya upinzani, ni kwa kuwa HAVIVUMI
  2. Moja wapo ya sababu zilizofanya wapiga kura waipigie zaidi CCM, ni kwa sababu INAVUMA
  3. Mojawapo ya sababu iliyoifanya CHADEMA iongoze katika kura zaidi ya vyama vingine vyote vya upinzani ni kwa sababu ILIVUMA kuliko vingine
  4. Mojawapo ya vitu vitakavyoendelea kuiweka CHADEMA juu, ni kwa kuendelea kUVUMA

Tabu yao ni moja, wanachagua kuvuma kule ambako tayari wanavuma sana. Arusha, Mwanza nadhani baadaye watakwenda Moshi?
 
mwanza ooooh mwanza... u gotta luv that city!

asanteni ndugu zangu wa mwanza:hug:
 
Baadaye tuwaulize viongozi wetu wa CHADEMA gharama zilizotumika kuandaa fiesta hii. Ruzuku yao ambayo ni kodi zetu imepanda sana baada ya kupata Wabunge, Madiwani wengi na kura nyingi za Urais. Fedha hizi zinapaswa kutumika hivi?

Na jamaa zako wa CCM je?
 
chadema%2Bmwanza.14.JPG
chadema%2Bmwanza.5.JPG
chadema%2Bmwanza.4.JPG
 
Kwa yaliyotokea Mwanza,naona kama CHADEMA kwa sasa hivi kina sifa zote za kuwa de facto Chama Tawala kwa sababu:-
(1) kina watu makini kwa hoja na mitazamo ya kubadili hali ya wananchi kama
chama tawala kinavyopaswa kuwa.
(2) kinajali kwa dhati matatizo ya watu na kina hoja madhubuti za kuondoa ma
tatizo hayo.
(3) kinasikilizwa sana na watu wengi kila kinapotoa miito yoyote ile kama maa
ndamano.
(4) Kiko upande mmoja kikipingwa na vyama vingine vingi. Kwa kawaida
chama tawala kinakuwa upande wa peke yake kikipingwa na vingine kama
hali ilivyo kwa "Chama Tawala" CHADEMA sasa hivi kinavyoshambuliwa na
"Vyama vya Upinzani" vya CCM,CUF,NCCR Mageuzi,UDP,TLP nk.
Kutokana na nguvu ya ushawishi ya CHADEMA kwa wananchi,CCM inapaswa ikichukulie chama hicho kama taasisi kubwa na nyeti katika mustakabali wa maendeleo na amani ya nchi yetu. Wawe wanazitafakari kwa utekelezaji agenda mbali mbali zinazotekelezeka za chama hicho zinazolenga maslahi ya umma. Wasiichukulie CHADEMA kama kichama fulani hivi cha wababbaishaji kama kile cha jimbo moja na mbunge mmoja! CCM wakitangaza vita na CHADEMA kupinga hoja za maslahi ya umma, kuna hatari kubwa inaweza kutokea kama CHADEMA kitatumia nguvu yake ya ushawishi dhidi ya serikali ya CCM. Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom