[PICHA] Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Mara

Highness ametuma salam kwa JK kwamba wanaandamana kwa kuwa watanzania tumepigika.

Wenje:

Mimi ni mtoto wa muuza vitumbua Shirati.

Kufa kwa kiwanda cha Mwatex (Mutex?) kumesababisha kuwa na machinga wengi.

Anamalizia kwa kumwambia JK 'uvumilivu una mwisho'

Shukrani PJ.
Unajua unapokuwa mshiriki siorahisi kupata picha nzuri.Ninazo picha kwenye simu yangu lakini hazina ubora wa kurusha hapa.Tupo na waandishi wa habari na wadau wengine naamini watazirusha kama walivyofanya.

Tupo pamoja.

pole na kazi dada Regia, we hizo picha kama vipi zirushe tu, hamna shida yoyote.

Sasa ni Sugu, anawaomba watu wa Musoma wasusie kazi za wasanii walioibeba CCM wakati wa kampeni 2010

Wenje:

Mimi ni mtoto wa muuza vitumbua Shirati.

Kufa kwa kiwanda cha Mwatex (Mutex?) kumesababisha kuwa na machinga wengi.

Anamalizia kwa kumwambia JK 'uvumilivu una mwisho'

huo mwisho ni lini ndugu yangu? Isije ikawa akitoka jk akaingia lowasa ndio mwisho unaouzungumzia.

Sugu kasema pamoja na kutoka kwenye familia isiyo na jina lkn amekuwa mbunge kwa kupitia CDM

Kasimama Mdee kasema yeye kashinda Jimbo ambalo lina vigogo wengi wa CCM ambao nao pia walimpigia kura.

Wenje:

Mimi ni mtoto wa muuza vitumbua Shirati.

Kufa kwa kiwanda cha Mwatex (Mutex?) kumesababisha kuwa na machinga wengi.

Anamalizia kwa kumwambia JK 'uvumilivu una mwisho'

Mkuu asante kwa kutujuza yanayojili. Endelea kutuhabarisha. Kwa wanaMusoma sina wasiwasi, hao huwa wanafanya kweli. Kuna kata ilimchagua diwani ili hali akiwa amewekwa lupango kwa visa vya kile chama mfilisi.

Vicent Nyerere anasema kuna mjanja kakigeuza kiwanda cha MUTEX kuwa godauni

Vincent anasema huyo mjanja alokigeuza kiwanda cha MUTEX kuwa godown kishamfukuza

Wakuu Salaam!!!

Yale maandamano ya Kanda ya Ziwa leo yanahamia Mkoa wa Mara baada ya jana kuingia Geita, Sengerema, Misungwi, Kwimba na Ukerewe. Maandamano yatakuwa Musoma kuanzia Viwanja vya Bweri mpaka Uwanja Mkendo Musoma Mjini. Msafara wa Vikosi toka Mwanza mjini unatarajiwa kupokelewa na Mbunge wa Musoma Mijini Vincent Nyerere.

Dalili zinaonesha kuwa na leo CHADEMA itaiteka Musoma kwa jinsi ambavyo watu wamejipanga na kujiandaa kwa hamu maandamano haya. Maandamano yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.

Aluta Continua.

Kutoka Kitangiri Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Mutuwekee na kapicha tafadhali....

Vincent kasema atahakikisha mafisadi wanaikimbia Musoma.

Mama Slaa kasalimia, kisha kampisha Dr. Slaa kuongea, anasema ataongea kidogo kwa kuwa muda ni tight ili Mbowe aongee.

Slaa kawashukuru wananchi wa Musoma kwa kumpigia kura na wabunge & madiwani wa CDM

Vincent kasema atahakikisha mafisadi wanaikimbia Musoma.

Mama Slaa kasalimia, kisha kampisha Dr. Slaa kuongea, anasema ataongea kidogo kwa kuwa muda ni tight ili Mbowe aongee.

Slaa kawashukuru wananchi wa Musoma kwa kumpigia kura na wabunge & madiwani wa CDM

Asante kwa updates mzee vipi uwingi wa watu hapo inaweza kulinganishwa na jana kule Mwanza

Watu ni wengi sana hapa uwanja wa Mkendo, nashindwa ku-attach picha via mobile

Slaa anasema 'Kumbe inawezekana kuandamana kwa amani?'

Analiponda Jeshi la Polisi (si JWTZ) kwa uonevu.

Anasema Waziri wa Ulinzi anatakiwa ajiuzulu kuhusiana na tukio la Gongo la Mboto.

Bravo CHADEMA hiyo ndio njia pekee ya amani ya kuikomboa nchi hii kutoka kwa serikali hii ya mafisadi inayoongozwa na Rostam Aziz kwa remote control.

Samahani network wakti mwingine inasumbua bandugu.

Slaa ameongelea DOWANS kwa kirefu, akahitimisha kwa kutaka mitambo itaifishwe.

Kasema kamati ya sasa ya kina January Makamba imeingia mkenge.

Sasa anaongelea kupanda kwa gharama za maisha, anasema kuandamana hakuwezi kukwepeka, wanalazimika kuandamana kutokana na uhalisia wa maisha.

Sasa kaingia Freeman Mbowe

Mbowe:

CHADEMA ni tishio kwa mafisadi, ni chama cha watanzania wote

Mbowe:

Tupo hapa leo watu wa dini mbalimbali, makabila mbalimbali si kwa bahati mbaya, lakini hakuna hata mmoja wetu alomwuliza mwenzake ni dini gani au kabila gani. CDM ni chama cha watanzania wote bila kujali imani na makabila yao

Back
Top Bottom