[PICHA] Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Mara

Wakuu Salaam!!!

Yale maandamano ya Kanda ya Ziwa leo yanahamia Mkoa wa Mara baada ya jana kuingia Geita, Sengerema, Misungwi, Kwimba na Ukerewe. Maandamano yatakuwa Musoma kuanzia Viwanja vya Bweri mpaka Uwanja Mkendo Musoma Mjini. Msafara wa Vikosi toka Mwanza mjini unatarajiwa kupokelewa na Mbunge wa Musoma Mijini Vincent Nyerere.

Dalili zinaonesha kuwa na leo CHADEMA itaiteka Musoma kwa jinsi ambavyo watu wamejipanga na kujiandaa kwa hamu maandamano haya. Maandamano yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.

Aluta Continua.

Kutoka Kitangiri Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

=====================
KATIKA PICHA


122c5g1.jpg

beybnp.jpg

asante
endelea kutupasha,
waambie makamanda wengine watupe habari humu jamvini,
tunataka tuwasikie na wao pia.
 
Chadema ni taasisi sio mtu binafsi hivyo basi mtu yoyote akiyumbisha mustakabali wa chama lazima achukuliwe hatua za kinidhamu regardles who he/she is. Kuhusu kafulira kutoswa sijaona madhara yoyote aliyosababisha kwa chadema. Kwanza kwa jinsi asivyo na msimamo hastahili hata kuchezea chadema.
 
Asante sana mama ila nguvu ya umma balaa! Na hizi hazijachakachuliwa kama zile za chama tawala. Na hawa watu hawajasombwa kwa malori kama wakati wa kampeni za ccm!
 
NIMABADILIKO CCM WAFUNGASHE VIRAGO VYAO SITAWAVUMILIA MIMINA KIZAZI CHANGU WAMETUFANYA MAZUZU nakudidimiza maisha ya watanzania mamilioni kwa mamilioni munguibariki Tanzania mungu ibariki africa !!..
Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
 
Back
Top Bottom