[PICHA] Maandamano ya CHADEMA Chato na Katoro

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
863
Wakuu, Salaam!

Jana nilikuwa kwenye maandamano katika Wilaya ya Chato nyumbani kwa Maghufuli ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Maandamano yalikuwa ni ya Kilometa nane yaliyoshirikisha magari,pikipiki na waendao kwa miguu. Baada ya maandamano kama kawaida ulifanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Leo wakati tunarudi Mwanza tukafanya maandamano madogo na mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro jimboni Busanda ambako nako watu walijitokeza kwa wingi. Hakika watanzania wameamua kuunga mkono mabadiliko. Kama tungeanza mapema vuguvugu hili nadhani saa hizi tungekuwa tunazungmza mengine kabisa.

Maandamano Kanda ya Ziwa ndio yamehitimishwa na baadhi ya Viongozi wamesharejea kwenye Makazi Yao. Wengine bado tupo hapa jijini Mwanza tunakula Sato. Tumehitimisha kwaajili ya kufanya tathmini na kujipanga upya kwaajili ya Kanda zingine.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Kutoka Jijiji Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.

============================

P030311_15.jpg

P030311_16.jpg

chato3.jpg

chato1.jpg

chato.jpg

chato2.jpg

chato4.jpg

chato5.jpg
 
Hongereni sana kwa kazi nzuri na poleni kwa misusuko ya wale wanaoogopa vivuli vyao. Tunawaombea mrudi kwenu salama. Hakuna kulala hadi kieleweke.
 
Ukifanya analytical analysis inakuwa vigumu sana kuelewa CCM walishinda vipi Urais na idadi kubwa ya wabunge only 4months back??? The only conclusion ni Uchakachuaji wa hali ya juu, na kama uchaguzi huru ukifanyika TZ hata kesho CHadema ni RULING PARTY.

Kila la heri Dada Regia, lakini nadhani sasa uongozi mzima wa chadema ukae chini na wanasheria ili kucover all the bases, ili kila matamshi yawe ndani ya sheria, maana JK na serikali wamepigwa na hofu na kitakachofuata ni mabavu ya dola. Ni muhimu sana kwa sasa hivi kuwaelimisha wananchi matumizi mabaya ya serikali, upotevu wa pesa za umma na mambo mengine bila kusogea hata kidogo kwenye gray area yoyote kisheria, sababu hamna haja MAPENZI YA WANANCHI KWA CHADEMA YANAKUWA NATURALLY sababu ya upuuzi wa serikali.

May God Bless Tanzania.
 
Wakuu, Salaam!

Jana nilikuwa kwenye maandamano katika Wilaya ya Chato nyumbani kwa Maghufuli ambako kulikuwa na umati mkubwa wa watu. Maandamano yalikuwa ni ya Kilometa nane yaliyoshirikisha magari,pikipiki na waendao kwa miguu. Baada ya maandamano kama kawaida ulifanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Leo wakati tunarudi Mwanza tukafanya maandamano madogo na mkutano wa hadhara katika Kata ya Katoro jimboni Busanda ambako nako watu walijitokeza kwa wingi. Hakika watanzania wameamua kuunga mkono mabadiliko. Kama tungeanza mapema vuguvugu hili nadhani saa hizi tungekuwa tunazungmza mengine kabisa.

Maandamano Kanda ya Ziwa ndio yamehitimishwa na baadhi ya Viongozi wamesharejea kwenye Makazi Yao. Wengine bado tupo hapa jijini Mwanza tunakula Sato. Tumehitimisha kwaajili ya kufanya tathmini na kujipanga upya kwaajili ya Kanda zingine.

Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

Kutoka Jijiji Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli- Kazi na Ajira.

============================

P030311_15.jpg

P030311_16.jpg

chato3.jpg

chato1.jpg

chato.jpg

chato2.jpg

chato4.jpg

Hizi picha ndizo zinawafanya CCM waanze kuruka kimanga khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Safi sana CDM mmemaliza mzizi wa fitna CCM watakiona cha mtema kuni kilichomtoa kanga manyoya!
 
Hongereni sana, kweli saa ya ukombozi wa mtanzania imeshawadia hakuna kulala!!!!!!!
 
I wish na CCM nao wafanye maandamano lakin without Entertainment or free transport (Ili waende wale tu ambao huwa wanaenda kwa dhamira yao) sijui watahudhuria wangapi...(
 
While we are @ it, lazima sasa techniques za hali ya juu zitumike kuwa isolate viongozi wa juu na mafisadi. Hapa nina maana ASAP Chadema waongeze wafanyakazi wa chini wa serikali kama watu ambao chadema inawatetea ukijumlisha na vijana maskini na wananchi maskini kwa ujumla. Kwa kuanzia Chadema waweke wazi kuwa wanataka watu muhimu kama walimu, madaktari walioajiriwa kwenye hopsitali za serikali, Polisi wa chini, wanajeshi wa chini, manurse na wafanyakazi wengine kwa ujumla waboreshewe mishahara. I believe ili litaiweka serikali kwenye wakati mgumu na hapohapo kwafanya hao polisi ambao hawafikirii kutoka na ufinyu wa elimu kupiga wananchi na viongozi wa chadema wakati hiyo cake inaliwa na hao viongozi wa juu na mafisadi.
 
Wape wape eeeeeeeeeee vidonge vyaoooo wapewape vidonge vyaoooooooooo,kudadeki hapo ni masikani washikaji awajaniangusha. Hiiiiii ni sombamsomba abaki mtu hadi uvunguni Treni himemsoba PM kwenda BKna bado
 
Ukifanya analytical analysis inakuwa vigumu sana kuelewa CCM walishinda vipi Urais na idadi kubwa ya wabunge only 4months back??? The only conclusion ni Uchakachuaji wa hali ya juu, na kama uchaguzi huru ukifanyika TZ hata kesho CHadema ni RULING PARTY.

Kila la heri Dada Regia, lakini nadhani sasa uongozi mzima wa chadema ukae chini na wanasheria ili kucover all the bases, ili kila matamshi yawe ndani ya sheria, maana JK na serikali wamepigwa na hofu na kitakachofuata ni mabavu ya dola. Ni muhimu sana kwa sasa hivi kuwaelimisha wananchi matumizi mabaya ya serikali, upotevu wa pesa za umma na mambo mengine bila kusogea hata kidogo kwenye gray area yoyote kisheria, sababu hamna haja MAPENZI YA WANANCHI KWA CHADEMA YANAKUWA NATURALLY sababu ya upuuzi wa serikali.

May God Bless Tanzania.

Mkuu analysis gani tena hapo wakati picha zinajionyesha. Watoto kibao hawapigi kura. Pia vijana kibao ambao kelele nyingi lakini hawapigi kura. Unawaona wazee wangapi kwenye hizo picha? Wazee wengine ndio huwa wanapiga kura, ila wapo wachache sana kwenye picha ambazo nimeziona so far.
 
Chadema ina wafuasi wengi,mashabiki wengi ila ina walalamikaji wengi pia wasio weza kuchukua hatua,........kati ya wengi wanao ishabikia chadema,wachache sana wanaopiga kura...

Ni ukweli ambao wengi wataupinga humu
 
Back
Top Bottom