PICHA: Maalim Hamad akutana na Balozi Haji na pia Viongozi wa TIBA Asili Ofisini kwake MIGOMBANI

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akutana na mkurugenzi wa mambo ya nje, Ofisi ya Zanzibar na uongozi wa tiba asilia



%253B.JPG


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
akisalimiana na viongozi wa Jumuiya ya tiba asilia Zanzibar JUTIJAZA,
waliokutana ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kubadilishana mawazo
juu ya maendeleo ya tiba hiyo nchini.


tr.JPG



Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na
Mkurugenzi wa mambo ya nje ofisi ya Zanzibar, balozi Silima Kombo Haji
ofisini kwake Migombani Zanzibar.


4.JPG


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisikiliza kwa umakini maelezo yanayotolewa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Tiba Asilia Zanzibar JUTIJAZA,
Dkt. Haji Juma Msanifu kuhusiana na maendeleo ya tiba hiyo Zanzibar,
huko ofisini kwake Migombani Zanzibar.Picha, Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar


--
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema mabalozi pamoja na idara ya mambo ya nje Zanzibar, wanayo nafasi kubwa ya kuisaidia Serikali kukuza mahusiano yake na nchi nyengine pamoja na mashirika ya kimataifa.

Amesema licha ya suala la mambo ya nje kuwa la Muungano, lakini yapo baadhi ya mambo ambayo Zanzibar inaweza kuyafanya katika kushirikiana na mataifa mengine, kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

Maalim Seif ametoa changamoto hiyo ofisini kwake Migombani Zanzibar, alipokuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa mambo ya nje ofisi ya Zanzibar, balozi Silima Kombo Haji.

Amefahamisha kuwa Zanzibar kama nchi imekuwa ikitembelewa na viongozi mbali mbali wa nchi za kigeni pamoja na mashirika ya kimataifa ambao wamekuwa na hamu na shauku ya kutaka kuendeleza mahusiano na Zanzibar, katika nyanja tofauti zikiwemo za kiuchumi.

"Wakuu wa nchi mbali mbali wanakuja hapa Zanzibar pamoja na viongozi wa mashirika ya kimataifa, na huwa na shauku kubwa na kutaka kuendelea mahusiano baina yao na nchi yetu",alieleza.

Amempongeza mkurugenzi huyo kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo, na kwamba serikali tampa mashirikiano ya kutosha katika kutekeleza majukumu yake, na kusifu kazi nzuri inayofanywa na ofisi hiyo. Hata hivyo Makamu wa Kwanza wa Rais amemtaka mkurugenzi huyo na ofisi yake kwa ujumla, kuongeza umakini wakati wanaposhughulikia safari za viongozi wakuu wa nchi, ili kuondosha usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kwa upande wake balozi Silima ambaye alikwenda kujitambulisha kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni, amemuhakikishia Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa ofisi yake itafanya kazi kwa karibu na serikali katika kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata fursa zinazostahiki.

Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais amekutana na uongozi wa Jumuiya ya tiba asilia Zanzibar JUTIJAZA, na kubadilishana mawazo juu ya maendeleo ya tiba hiyo nchini.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Haji Juma Msanifu amesema jumuiya yake ina mpango wa kuanzisha vitalu maalum vya miti asilia, ili kurahisisha upatikanaji wa dawa hizo.

Dkt. Msanifu amesema wamefikia uamuzi huo kufuatia kuendelea kwa vitendo vya ukataji wa miti ovyo, hali inayotishia kutoweka kwa miti inayotumika kwa ajili ya upatikanaji wa dawa asilia.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo bi Zahra Hassan amesema jumuiya yao bado inakabiliwa na tatizo la ofisi za uhakika pamoja na usafiri, na kuiomba serikali kuangalia namna ya kuisaidia ili kuondokana na matatizo
hayo.


Amesema tiba asilia ni muhimu na zimekuwa zikitumika kitaalamu na kujipatia umaarufu mkubwa katika nchi za Afrika Mashariki na dunia kwa ujumla, jambo ambalo linapaswa kupewa msukumo kwa maslahi ya wananchi na taifa
kwa ujumla.

Maalim Seif kwa upande wake amewataka wanajumuiya hao kufuatilia upatikanaji wa hati miliki za viwanja walivyonavyo kwa ajili ujenzi wa ofisi na kituo cha utafiti, ili waweze kufanikisha matarajio yao kwa uhakika.

Kuhusu ukataji wa miti, Maalim Seif amesema bado ni changamoto inayoikabili ofisi yake, lakini wanaendelea kuifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata elimu ya kutosha juu ya uhifadhi wa miti na mazingira
kwa ujumla.


Na Hasssan Hamad

Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar.
 

Ni kweli HAMAD kama kuna njia ya Serikali ya Zanzibar kuongea na NCHI MARAFIKI zake kupata MISAADA kwa ZANZIBAR, Hiyo Ingesaidia na

kama wakati Zanzibar imefikia wakati wa kuamua kuwa hawautaki MUUNGANO wawe tayari wameisha JIZATITI wenyewe kwenye Masuala ya

KIMATAIFA...
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom