Picha kwenye uombaji wa kazi

Ma-HR wengine wanatumia hizi picha vibaya, wakishaiona picha ya mtu inavutia (hasa picha za wadada) watachukua no kwenye CV na kuanza kupiga simu ovyo, mara ooh umeomba kazi flani, mi naweza kukusaidia nk. Mwisho utasikia tuonane ili nikupe mikakati nk, ukiulizia pa kuonana utaambiwa hotelini. So bad.
 
Tra nakumbuka walihitaji picha
ni kazi za aina gani hizo?kwa wenye equal employment opportunity under the law tayari kungekuwa na bonge la lawsuit kama sio class-action suit dhidi ya hizo kampuni au mashirika yanayofanya hivyo. Sioni mantiki yoyote katika kuomba picha ndogo ya mtu katika hatua za awali za uombaji kazi. Mtu unaweza ukajenga hoja tena kwa urahisi kabisa kuwa kwa kufanya hivyo wanabagua watu au wanajenga mazingira ya kurahisisha ubaguzi wa watu kwa misingi ya mionekano yao.
 
Hata nafasi zilizotangwazwa wiki jana na tume ya ajira s.l.p 63100 dsm wanataka ubandike ppicha moja na ukathibitishe vyeti nakala za vyeti mahakamani, inakera kwani makarani mahakamani wanadai tshs 2000 kwa kila cheti sasa jumlisha vyeti hivi, shahada, f6, f4, std7, kuzaliwa unapata buku 10, kaaaaaazzzzzi kwelikweli
 
huu mchakato wa kwenda mahakamani tena wanazidi -ku-complicate mambo
 
kitendo cha ku-demand picha, wakati wa kufanya application hiyo sis tunaichukulia kama discrimination on employment; haina logic kuajiri eti kwa kuangalia muomekano wa mtu ktk picha atakama ni atua za awali, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya 2004, kifungu cha 7 kimetamka wazi kwamba ni marufuku mtu yeyote kubaguliwa hasa ktk mchakato huu wa ajira kwa namna yeyote ile.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom