Picha: JK kwenye ghorofa liloloporomoka

Tatizo siyo ufundi wa ujenzi, bali ni quality ya vifaa vyetu vya ujenzi hapa nchini. Nondo zinazotumika si za kiwango takiwa, wala simenti yenyewe ni siment feki. Tusilaumu wahandisi, tuangalie pande zotezote. Nchi yetu ni usanii pande zote na siyo upande mmoja. Jiulize, kwa nini wachina wakati wanajenga uwanja wa taifa walitumia nondo zao na simenti yao????? Hii ni kwa kuwa vifaa vyetu havikidhi kiwango cha kimataifa. Hivyo majengo kuanguka ni tukio lililo tegemewa. na bado tutaona mengi.

Mkuu mbona unachanganya madawa. Wewe ni injinia, unaletewa nondo feki na simenti feki na unakubali kujengea halafu unasema usilaumiwe!!!! Ufundi ni pamoja na kujua vifaa bora vya ufundi wako
 
utawala wa sasa ni makamasi matupu
kweli zana za uokozi za kisasa hatuna
watu wanapiga sururu na kuokota matofali kwa mikono????

afu wanakuja kuuza sura apo?nyambafu
 
Mkuu mbona unachanganya madawa. Wewe ni injinia, unaletewa nondo feki na simenti feki na unakubali kujengea halafu unasema usilaumiwe!!!! Ufundi ni pamoja na kujua vifaa bora vya ufundi wako
Samahani kwa hasira mkuu, Nilikuwa na maana ya kuwa tujifunze na kutokukubali kuwa dampo la materials of lowest quality. Vifaa vyote vya ujenzi, kwa maana ya nondo, siment, hata bati, haviko kwenye viwango. Hata nchi jirani achilia mbali kenya, uganda zambia, bali hata burundi, rwanda na drc, wanatuzidi. Sikutarajia kukuudhi hadi uwe mkali, but it was just a point of discussion.
 
Makampuni ya nje yakipewa kazi tunalalamika siyo wazalendo.
 
Mnalalamika wakat kuna wakaguzi wanalipwa lakin ndo ivyo kifuc kinaönekana mchanga tupu hakuna sement
 
Waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa aliwahi kumtimua kazi Kurugenzi wa Halmashaur Bwana Idd Nyundo kwa issue hii hii ya kupolomoka jengo
 
Waziri mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa aliwahi kumtimua kazi Mkurugenzi wa Halmashaur Bwana Idd Nyundo kwa issue hii hii ya kupolomoka jengo
 
Hii nchi inapitia ktk kipindi cha laana, tusubiri matamko na kuundwa tume kuchunguza then kimyaaaaaaaaaaaaa
 
Nashindwa kuelewa ni kwa nini NHC wanaingia ubia na wahindi kujenga hayo magorofa wakati hela yote inakuwa ya mkopo. NHC ilianzishwa na marehemu Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere kwa ajili ya watu wa kipato cha chini wapate nyumba za kuishi, lakini cha kushangaza ni kwamba shirika hii limekuwa la MA--------- na ndio faida yake hii ya kuanguka kwa jengo. Nashauri hata huyo mkurugenzi wa NHC Nehemia Msechu achukuliwa hatua na huyo --------- aliyeingi ubia na NHC.
 
Labda safari hii anaweza kuwa mkali kidogo! Tusubiri.

Hapa ndipo kwenye tatizo letu watanzania tunafikiti ukali ndio unaonyesha utendaji kazi. Hii imefanya viongozi wetu 'kupiga kelele nyingi, kufukuza watu n.k.' Mbele ya kamera za waandishi wa habari. Uongozi ni zaidi ya ukali.
 
Mheshimiwa Rais JK amezuru eneo la maafa pale kulipoporomoka ghorofa leo asubuhi.

attachment.php
Picha imeeditiwa hii, mbona sijaona akicheka?
 
Akina Mchechu, Mndolwa na timu yao ya NHC mpya wapo kiulaji na kibiashara zaidi. Mtakapowashtukia watakuwa tayari ni matajiri wazawa. Hata lile jengo lililopo Samora opposite na Twiga BanCorp wataalamu wanasema lina kasoro nyingi sana. Ni suala la muda tu.


Mchechu na timu yake waachwe kabisa katika hili. Kumbuka jengo hili lilianza kujengwa mwaka 2008 wakati Mchechu akiwa haijui NHC kwa maana ya utendaji! Alipoingia alikuta kuna mikataba ya kipuuzi mingi mno. Akafuta mikataba 64. huu ni mmoja wa mikataba iliyoingiwa na watangulizi wake ambao hawakuwa na chembe ya uzalendo. kwa hiyo kumshutumu yeye na timu yake ya kina Mndolwa, Suzy na wengine wengi, ni kuwaonea. Tuwe wakweli.
 
Nashindwa kuelewa ni kwa nini NHC wanaingia ubia na wahindi kujenga hayo magorofa wakati hela yote inakuwa ya mkopo. NHC ilianzishwa na marehemu Baba wa Taifa Mwl J.K.Nyerere kwa ajili ya watu wa kipato cha chini wapate nyumba za kuishi, lakini cha kushangaza ni kwamba shirika hii limekuwa la MA--------- na ndio faida yake hii ya kuanguka kwa jengo. Nashauri hata huyo mkurugenzi wa NHC Nehemia Msechu achukuliwa hatua na huyo --------- aliyeingi ubia na NHC.


Mkataba wa jengo hili uliiingiwa mwaka 2008 Mchechu akiwa bado hajaingia NHC. Lawama zimwendee mtangulizi wake aliyelimaliza shirika. Akauza viwanja vingi sana vya NHC.
 
Mi yangu macho na msikio kwani kifuatacho ni mizengwe wahusika wanaeleweka
 
Back
Top Bottom