Picha itakayomsuta JK na wabunge wake mamilionea.....

Hii ndio hali halisi kule MBAGALA ..na ndio Tanzania ya 2009

enough with mijadala ya ufisadi...hali halisi on the ground ni hii...
maendeleo.jpg

Wanafunzi wa darasa la saba kutoka Mbagala Kuu jijini Dar es salaam wakiwa katika mitihani yao ya kila mwezi.


-Spika wa bunge letu bwana Samuel Sitta anasema kuwa wabinge wanastahili kulipwa zaidi ya milioni 7 kwa mwezi apart from marupu rupu

-Pesa za kupigana vita Comoro tunazo

-Pesa za mabilioni kwa ajili ya ID cards pia tunazo

-Pesa za kumpa Mattaka na wajumbe wake kule NIC tunazo

This picture shows how out of touch tumekuwa na majority on the ground. Its been 2 years hakuna kinachojadiliwa zaidi ya UFISADI, ile ilani yetu ya UCHAGUZI imetupwa kapuni na mbaya zaidi wapinzani kama CHADEMA nao wako more out of touch kuliko wote on the ground kwani wao bora kukodi helicopter ili kuwakimbia wananchi wakati wa kampeni...

Pesa ya helicopter si wangewanunulia madawati hawa wanafunzi?

anyway nawasilisha.

Tatizo ni kwamba viongozi hawajali na wamesahau kabisa kwamba uongozi ni dhamana na kazi yao ni kutumikia WATU waliowapa dhamana ya kuongoza. Nchi maskini kama yetu inahitaji viongozi waadilifu wanaojua na kujali wajibu wao kwa wananchi. Viongozi wanapaswa kuwa 'watumwa' wenye kukosa usingizi wakiwaza wafanye nini kuwatumikia na kuwanufaisha waliowachagua badala ya kuwaza kujinufaisha wao wenyewe. Matokeo ya hali iliyopo ya viongozi kukengeuka ndio inapofika kwenye Budget matatizo ya wananchi hayakumbukwi na kushughulikiwa kwa kina.

Nchi yenye asilimia 60 ya wananchi wasio na uhakika wa maisha yao ya kila siku; yenye wanafunzi mijini na vijijini wasio na madawati wanaoketi chini wakifanya mitihani yao kama hawa tulioonyeshwa n.k., n.k.; Budget ya mwaka kwa ajili ya maendeleo ya wananchi hao wasio na matumaini, inasheheni kasma za mabilioni ya fedha kwa ajili mambo yasiyo ya lazima kama CHAI maofisini. Wabunge wawakilishi wa watu hao wasio na matumaini, wanaipitisha Budget hiyo kirahisi bila matatizo yoyote. Ndiko tulikofika, hakuna anayeguswa kwa dhati wala anayejali mustakabali wa walalahoi na watoto wao wanaoketi chini darasani! Kila anayepata nafasi ya uongozi ya ngazi yoyote ile anawaza 'pangu pakavu, nitieje mchuzi nifaidi!'
 
i am so angryyyy nikiona hivi especially ukizingania robo nzima ya mahshara yangu inakatwa na hawa watu. basi tu yani
 
Yaani hapo mtu akimuozesha mwanae mnapiga makelele,akimpeleka mwane mgodini mnapiga makelele ,yaani hapo wakitoka lazima wawe wanaenda kama vizee kwa kupinda migongo ,si ajabu wakawa waathirika wa uti wa mgongo baada ya miaka 20.
 
LAKINI HII NDIYO ILANI YETU (ccm)YA UCHAGUZI 2005 KUUA OR SORRY KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KWA ASILIMIA ......

By the way kuna mtu anajua watoto wa hawa wakuu wanasoma wapi?
mkulu JK
Makamba
RA
Sita
EL
Karamagi
Vijisenti
Pinda
mawaziri wate ktk wizara ya elimu
Watoto wa JK wamesoma/wanasoma shule za kawaida tu si zakutisha kivile kama Trust St Patrick, Kifungiro Girls, na Kuna mmoja anasoma Botswana kama sikosei na alipelekwa kule kwaajili ya usalama zaidi..
 
makali tunayo sisi wananchi lakini hivi kweli yupo kiongozi ambaye akiingia madarakani anafuata kanunu na misingi ya uongozi?kama yupo nitajieni! mi nimejenga imani kila aingiae anakula akimalia anasepa zake,hata hao chadema wakichukua ikulu hali sidhani kama itabadilika.
 
Kwa maneno mengine Chadema ni sawa na CCM?

Ndio, Vyote ni vyama vya siasa. Lakini vina sera zinazotofautiana. Wakati umefika inabidi watanzania tubadilike. 1020 tuchague viongozi ambao wana uchungu na nchi hii. Hatuhitaji tena MAFISADI.
 
Hii ndio hali halisi kule MBAGALA ..na ndio Tanzania ya 2009

enough with mijadala ya ufisadi...hali halisi on the ground ni hii...
maendeleo.jpg

Wanafunzi wa darasa la saba kutoka Mbagala Kuu jijini Dar es salaam wakiwa katika mitihani yao ya kila mwezi.



-Spika wa bunge letu bwana Samuel Sitta anasema kuwa wabinge wanastahili kulipwa zaidi ya milioni 7 kwa mwezi apart from marupu rupu

-Pesa za kupigana vita Comoro tunazo

-Pesa za mabilioni kwa ajili ya ID cards pia tunazo

-Pesa za kumpa Mattaka na wajumbe wake kule NIC tunazo

This picture shows how out of touch tumekuwa na majority on the ground. Its been 2 years hakuna kinachojadiliwa zaidi ya UFISADI, ile ilani yetu ya UCHAGUZI imetupwa kapuni na mbaya zaidi wapinzani kama CHADEMA nao wako more out of touch kuliko wote on the ground kwani wao bora kukodi helicopter ili kuwakimbia wananchi wakati wa kampeni...

Pesa ya helicopter si wangewanunulia madawati hawa wanafunzi?

anyway nawasilisha.

Tanzania ni mfano wa kuigwa, mwenye wivu na ajinyonge!!
 
Bravo MwanaJF, we need Dictator at least for five years to clean this uozo vinginevyo huu mchezo wa kupokezana vijiti utatumaliza. Our fellow Tanzanians we have learn the lesson let us make change in 2010 elections!
 
Bwana Game tunashukuru kwa juhudi zako. Ila naona hawa hawahitaji madawati tu bali na darasa kwani naona kama wako nje. Sasa kwa hali hii watoto watafikaje huku tuliko? Kwanza nje kuna mchanga wenye vumbi ambapo linaweza kuwaletea watoto magonjwa. Kazi kwetu 2010.
 
Huwa siharibu kura yangu hata siku moja, nalala napumzika. Hapa sasa hivi hela zimeshaanza kumwagwa mitaani badala ya kutengeneza madawati watoto wakalie. Hakie Elimu ambao wana misaada wanazuiwa kusema ukweli kimatangazo.

Ndiyo maisha ya mbwe mbwe no choice.
 
This time tuna shughuli ya kufanya hasa tunapowachagua hawa watu kutuongoza. Tumuombe Mungu atupe uvumilivu sana vinginevyo kuna hatari.
 
Acheni maneno mengi, kila mtu na afanye analoweza kuokoa nji hii dhidi ya wadhalimu na waloshindwa kwa miaka 48 - uchaguzi unakaribia.....period.
 
Kuhusu helicopter utakua mnachemka kusema zinunulie madawati fedha za kampeni zitumike kwa kampeni.
hayo ndo mambo tunayopetea kila siku donor country wanatupa pesa za mradi fulani (elimu kwa mfano) wwatawala wanakata nusu wanapeleka kwenye account zao uhaibuni zilizobaki zinatumika kinume na mpango wa awali
Kununu madawati ni jukumu la serika sio chama cha upinzania.chama,mtu binafsi au kampuni wanaweza kuchangia kama wanavyofanya voda now(binti wa makamba)
Dispite tunajua ni njama ya kumanda
 
( WE NEED CHANGES )

TUME JIFUNZA NINI KUTOKA KWA WENZENTU WALIOKUWA NA HALI KAMA HII YA NCHI YETU?


Our lives begin to end the day we become silent about things that matter! Martin Luther King, Jr.
 
I told you guys! Hawa viongozi wetu wamekuwa kama mawe, Unajua jiwe linapigwa na jua, linanyeshewa mvua, upepo, n.k lakini halijitingishi, halisikii. Ukitaka lisogee sharti utumie nyundo, koleo, sururu,n.k. Sasa hawa watu maneno tunayoongea hayawafanyi chochote, hawatikisiki, wala hawajitingishi. Hii nchi wameifanya yao. We have to take action, kwa kuanzia ni 2010. Lakini pia nafikiri hiyo haitoshi we need more than uchaguzi.

Watu wanatenga mabilioni ya shs kwa ajili ya vitafunwa? What do u expect from these guys? NOTHING! Angalia leo karne hii watoto wanasomea mchangani, kweli tutafika?

Mheshimiwa hivi ukiona picha hiyo unajisikiaje? Ni kweli umefanikiwa nini katika miaka yako mitano ya Uongozi, Unatushawishi vipi tukupigie kura mwaka 2010? TAFAKARI!
 
Back
Top Bottom