Picha iliyonivutia leo hii

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
8E9U9910.JPG

Rais Mstaafu awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi akisisitiza jambo wakati alipokuwa katika mazungumzo na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mhe. Benjamim William Mkapa (kushoto), Jaji Mkuu Othman Chande (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadik Meck Sadik (watatu kushoto) pamoja na Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue jana jioni wakati wa futari iliyoandaliwa nyumbani kwa Balozi Sefue jijini Dar es Salaam kwa ajili ya viongozi mbalimbali serikalini. (Picha na Freddy Maro).
 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia upandaji wa miche ya mananasi katika shamba la Koranco kijiji cha Obotweri nje kidogo ya jiji la Accra. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Koranco Farms Ltd. Bw Emmanuel B. Koranteng ambaye amekuwa akilima shamba la matunda kwa miaka 27. Mwalimu Nyerere aliwahi kumtembelea shambani hapo katikati ya miaka ya 1980 kujionea ukulima huo wa matunda. PICHA NA IKULU
 
Mimi nimependa hiyo picha ambapo rais Jakaya Kikwete anakagua mananasi. Sikuipenda kwa vile ni nzuri sana bali inaonyesha Ghana walivyoamua kumsuta, maana kwa wanaojua mananasi pale Chalinze yasivyo na soko wanashangaa ujasiri wa ikwete kukubali kejeli hii. Hili ni suto ingawa kwa Kikwete si somo kwa vile ni mgumu wa kujifunza. Hivi kweli inaingia akilini kumfundisha mgogo jinsi ya kulima karanga? Ningekuwa Kikwete ningekwepa mtego huu ambao ni aibu na suto kwangu. Kwa vile Kikwete si mtu wa namna hiyo anaweza kugeuzwa kituko popote pale na asiipate. Hiyo ya marais wastaafu ni nzuri ingawa nao ni mzigo wa taifa kutokana na legacies zao.
 
Moja ya Magari na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi iliyopewa Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd likiwa limepaki katika Viwanja vya Jangwani kuhakikisha Usafi unazingatiwa Uwanjani hapo wakati tamasha la Dini lililopewa jina la LOVE TANZANIA likiendelea.

Kumbe bongo kuna magari ya kuzoa takataka? Lakini bado mji ni Mchafu?Mkuu Father of All
 
Last edited by a moderator:

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra leo Agosti 11, 2012

Hii ni aibu...au labda usanii! Yaani JK kweli ashangae 'kinanasi' hiki wakati pale jimboni9 kwake tu Kiwangwa na Gongo wanatoa 'mijinanasi' mpingo mikubwa ajabu! Delmonte na Azam wote wamechemsha kununua, watafutie soko hawa sio kushangaa vinanasi vyenye utapia mlo!
 
Mimi nimependa hiyo picha ambapo rais Jakaya Kikwete anakagua mananasi. Sikuipenda kwa vile ni nzuri sana bali inaonyesha Ghana walivyoamua kumsuta, maana kwa wanaojua mananasi pale Chalinze yasivyo na soko wanashangaa ujasiri wa ikwete kukubali kejeli hii. Hili ni suto ingawa kwa Kikwete si somo kwa vile ni mgumu wa kujifunza. Hivi kweli inaingia akilini kumfundisha mgogo jinsi ya kulima karanga? Ningekuwa Kikwete ningekwepa mtego huu ambao ni aibu na suto kwangu. Kwa vile Kikwete si mtu wa namna hiyo anaweza kugeuzwa kituko popote pale na asiipate. Hiyo ya marais wastaafu ni nzuri ingawa nao ni mzigo wa taifa kutokana na legacies zao.

KAKA usikurupuke fuatilia kwanza ndo uzungumze,aina ya mananasi ayo ni tofauti na aya ya kwetu,iyo mbegu inauzika nje tofauti na hii ya kwetu ambayo aina soko nje.
 
Mangimeli unakurupuka wewe au tuseme upenzi wako kwa JK umekuziba fahamu. Kwani umeambiwa kuwa hiyo mbegu ikiletwa Tanzania haioti? Acha ujinga hiyo mbegu gani wakati mananasi yenyewe ni viduchu ukilinganisha na ya kwetu? Kwa taarifa yako unachosema ni kutafuta kulumbana tu ili nawe uonekane umechangia. Tatizo langu si mbegu bali Kikwete na mchango wake kwa wakulima na si kujitia tia anajua kujifunza wakati hakuna anachofanya cha kuonyesha amejifunza. Anapenda kuzurura finito.
 
Amewadangaya wakweree wenzie kuwa atawajengea kiwanda pale Kiwangwa ili wapate soko la kuuzia mananasi yao mpaka leo ziiiiiiiii!! Mkweree anakata mbuga tu kwenda kutalii.
 
Hii ni aibu...au labda usanii! Yaani JK kweli ashangae 'kinanasi' hiki wakati pale jimboni9 kwake tu Kiwangwa na Gongo wanatoa 'mijinanasi' mpingo mikubwa ajabu! Delmonte na Azam wote wamechemsha kununua, watafutie soko hawa sio kushangaa vinanasi vyenye utapia mlo!
Ninafahamu kuwa rais Kikwete analima mananasi. Nadhani na yeye anapaswa kujifunza jinsi ya kuzalisha mananasi mazuri kabla hajapeleka watu wengine kujifunza
 
Mimi ningemwelewa kama angekuwa ametembelea kiwanda cha kisindika matunda kwa maana ya kutafuta soko la matunda yetu
 
KAKA usikurupuke fuatilia kwanza ndo uzungumze,aina ya mananasi ayo ni tofauti na aya ya kwetu,iyo mbegu inauzika nje tofauti na hii ya kwetu ambayo aina soko nje.

hahahahah...kila kukicha una waza nje tu, hujui soko la ndani ni kubwa sana ukipanga.
 
Ninafahamu kuwa rais Kikwete analima mananasi. Nadhani na yeye anapaswa kujifunza jinsi ya kuzalisha mananasi mazuri kabla hajapeleka watu wengine kujifunza

Najua shamba la Kikwete lilipo Kiwangwa, shamba la mwanae Riz2, Said Mwema wa Mwetemo, na shemeji yao Hosea... wote wanatoa mijinanasi mikubwa tu...tatizo la mananasi Bagamoyo (Kiwangwa, Fukayosi, Gongo, Mwetemo, Matipwili, mpaka unakaribia Saadani huko) sio quality ya nanasi...bali soko! Hichi kinanasi alichoshika Kikwete hapo pale Kiwangwa sokoni kinauzwa Tshs 300 - 400! mpingo mkubwa (sio mti, ni aina ya nanasi) linauzwa Tshs 700 - 800...mkulima atatokaje hapo? Delmonte na Azam wanakuja wananunua mananasi shambani kwa bei ya kutupa...mkulima atatokaje hapo?

NB: Najua kwani nami ni mkulima wa mananasi huko!
 
Hii ni dharau kubwa kwetu kama wa TZ,hainiingii akilini na wala sitaki kuamini kuwa huyu nimuonaye ni Rais wangu.Hapo angeweza kupeleka baadhi ya wajumbe tu walioandamana naye ili wajifunze shughuli yote inayofanyika hapo kama lengo ni kuona wenzetu wanavyofanya.
 
Back
Top Bottom