Picha: Ibada ya kumuaga Regia Mtema iliyofanyika Tabata

Special thanks kwako The Finest pamoja na wanaJF wote mliotwakilisha tuliombali.Inaumiza sana kumpoteza Regia,namuonea huruma pacha wake,wazazi wake,ndugu zake wa karibu na hata rafiki zake,najiuliza kama mimi niliyemfahamu hapa JF nimeumia hivi Je hawa watajwa hali ipoje kwao,hapana inaumiza tena inaumiza na uwezo wakumrudisha hatuna basi Regia nenda nasi tutafuata uendako,kazi uliyoifanya ni kubwa na tunaidhamini.RIP Regia
 
Ahsante mkuu,

Nawashukuru kwa niaba ya wadau wenzangu kwa kutuwakilisha...Tunaomba muendelee kutuwakilisha hadi tumalize kazi hii nzito ya kumsindikiza mwenzetu Regia katika safari yake ya mwisho hapa duniani!!

Binafsi na familia yangu tutakuwa na kazi moja kubwa ambayo ni kuwaombea wote muikamilishe kazi hii salama!!


Kila la heri katika safari ya Ifakara......

DC!!
 
SOON.....VERY SOON, Soon-very soon WE are going to SEE the KING, SOON....VERY...SOON WE are going to SEE the King, Halleluya..halleluya WE are going to see the KING......That is all i can write jamani....

RIP SISTER although it is very soon....
 
Asante sana Finest kutushirikisha kilichojiri katika sherehe ile ya mwisho ya dada na mtoto wetu Regia. Kutushirikisha kwako huku kwa habari katika picha kunanikumbusha kwa uchungu mkubwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kutuhabarisha yanayojiri katika harakati za chama chetu. Sisi tulio mbali na wengine nje ya nchi alitusaidia sana kwa kutuhabarisha na hatufahamu baada ya hapa nani atakayekuwa na moyo wa kutusaidia kupata habari kama alivyokuwa ametuzoesha. Binafsi sikupata bahati ya kuonana naye ingawa tulikuwa na mawasiliano kimtandao. Inauma, inasikitisha,inahuzunisha na kusononesha, lakini tuna tumaini moja tu; la kuonana nae tena katika ulimwengu ujao kwani Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.
 
Mkuu finest...nitakua mchoyo kwa niaba ya wengi ambao walikosa fursa ya kufika km sita-appreciate mchango wako huu adhimu!
 
Kwa mara ya tatu mwanaume mimi nikiwa na umri wa kuitwa mwanaume nimetoa machozi tena leo hii....nilitoa machozi kwa wazazi wangu na leo mwanaume mimi nimetoa machozi kwako dada mpendwa Regia,wana Mororgoro tutakukumbuka na kukuenzi daima,wote tu safari moja,ila kwa nini umewahi kutangulia kiasi hiki Regia?ungesubiri basi hata mpaka 2015 uthibistishe kua ni kiasi gani wana Morogoro hasa Kilombero tulivyokupenda...haya nenda dada yetu,nenda....tutaonana tena paradiso.....nio tayari Ifakara kwa ajili ya kukusinikiza Regia,tulikupenda sana,asante Mungu kwa maisha uliyomjalia Regia kua nasi,tunakushukuru sana baba
 
kwa kweli inauma saaaana tu,
Kifo chako kitakuwa chemchem ya ujasili ndani ya mioyo yetu, katika kumkomboa mtanzania mnyonge
mwacheni Mungu aitwe Mungu,
 
naona kama nipo usingizini nipo kwenye ndoto nzito,siamini ninachoendelea kusikiliza,kuona wala siamini machungu niliyo nayo moyoni.natamani iwe ni ndoto nitoke usingizini........eee mungu kama ni ndoto mbona inanitesa na kuniumiza?hapana is not regia
 
Kabla ya siku ya ajali iliyopelekea kifo cha mpendwa wetu nilikuwa namsikiliza Mwalimu Christopher Mwakasege akiwa anazungumzia jinsi watu walivyopata shida kuamini kuondokewa kwa mpendwa wao Fanuel Sedekia wengine wakawa wanasema haiwezekani maana walikuwa wamefunga kwa ajili ya kumwombea apone. Alitoa neno la msaada kwamba Mungu anabakia kuwa Mungu hata kama hakujibu maombi yako kama ulivyotaka. Ni wengi hatukuamini kifo cha mpendwa wetu na ni wengi tulikuwa tunamtegemea na kuona kwamba angekuwa msaada wetu hivyo tungependa kukaa nae zaidi ili kuweze kuchota hekima zake. Lakini niungane na maneno ya mtumishi wa Mungu kuwa Mungu anabakia kuwa Mungu kwa hiyo tumshukuru kwa kila jambo kwani kila analofanya ana makusudi mema. Mungu amlaze Dada yetu mpendwa Regia mahali pema ikimpendeza Mungu tukutane naye siku ile parapanda itakapolia.
 
Bwana alitoa na sasa ametwaa Jina la Bwana libarikiwe! R.I.P REGIA MTEMA! Bwana akuangazie nuru za uso wake.
 
Back
Top Bottom