PICHA hii tafakari - Hivi huyu OMBAOMBA kazalishwa na nani?

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
01_12_uub790.jpg


Saada King'ombe akiwa na watoto wake chini ya mti karibu na Viwanja vya Gymkhana, Upanga jijini Dar es Salaam. Nimeiangalia hii picha na kutafakari sana hivi huyu Omba omba amezalishwa na kina nani na je nani anawahudumia hawa watoto kweli Mungu mkubwa tumshukuru kwa kila jambo.

JIBU: Ombaomba huyu kazalishwa na Serikali yetu! Mwembe hauwezi kuzaa nanasi! Serikali ombaomba inazaa ombaomba! - By Marejesho
 
"Wanaonekana" kuwa na afya njema, na mavazi mazuri tofauti na ombaomba tuliozoea kuwaona mitaani. (au kwa kuwa yuko maeneo ya Upanga?)

Saada hapaswi kuwa "ombaomba" wa style hiyo, pamoja na matatizo ya kiuchumi yanayomkabili....kuna jambo limejificha!
 
Huyo omba omba ameshajadiliwa katika thread moja inayosema Mwl Dar ageuka Changudoa sijui?
 
Anafanya makusudi huyu, hana lolote! Ina maana hizo mimba anapata bahati mbaya? Tz huduma ya uzazi wa mpango ni BURE! Mie huwa simuonei huruma kabisa, nna ndugu vijijini wana watoto, wanalima na mvua hainyeshi, hao wanapata huruma yangu!
Uko sawa sawia King'asti kula tano. Uje utembee ukerewe uone wadada wana watoto kama yeye hawajaolewa, hawana kazi. wao ni shamba tu na watoto wanapiga shule ya msingi wanafaulu kwenda sekondari ya kata. Kuna mmoja kule zanzibar yeye anabadili watoto kila siku. leo utamkuta na mtoto mweupe kesho kablack, keshokutwa kamekua kidogo, au kachanga zaidi. Nafikiri huyu akiwa dar angekuwa ameshachezea kichapo kidogo. niliskia tu kuwa huwa anakodi mtoto wa kwenda kuzunguka nae kutwa mjini!!!
 
Anafanya makusudi huyu, hana lolote! Ina maana hizo mimba anapata bahati mbaya? Tz huduma ya uzazi wa mpango ni BURE! Mie huwa simuonei huruma kabisa, nna ndugu vijijini wana watoto, wanalima na mvua hainyeshi, hao wanapata huruma yangu!

si huduma ya uzazi wa mpango tu, hata elimu ya msingi ni BURE kabisa (licha ya tumichango twa hapa na pale)..................... huyo mama kama si mgonjwa wa akili, mi namwita malaya na mjinga tu................. tena anatutia aibu sana watanzania............ na serikali imnyang'anye watoto.................... hafai kuitwa mama................... anawaharibia sana maisha hao watoto wake.....................
 
Kama taaluma yake ni ualimu na ana uzoefu na kazi yake ningetegemea wasifu wake ni soko tosha kupata ajira sehemu nyingine hata iwe shule binafsi au kujiajiri kwa kutoa bonge la tuition. Kuna dalili za kufukuzwa kwake kazini kana kwamba walitafuta weak point kutokana na sifa ya utendaji wake kazini. Mambo ya misiba yanaeleweka na wengi tu wanafiwa na kwenda misibani mikoa ya mbali kisha wanarudi makazini, iweje yeye pekee aonewe na kukataliwa kurudi kibaruani??????????
 
Mimi humshangaa sana mtu mwenye kuzaa namna hiyo kama bata. Sasa huyu ambaye amededicate maisha yake kukaa pembeni ya barabara akiomba na watoto wote hao anastahili viboko. Kama kuna mtu anamfahamu tafadhali akamuondoe pale na kumrudisha kijiji alichotoka, anatuchafulia jiji pale.
 
01_12_uub790.jpg


Saada King’ombe akiwa na watoto wake chini ya mti karibu na Viwanja vya Gymkhana, Upanga jijini Dar es Salaam. Nimeiangalia hii picha na kutafakari sana hivi huyu Omba omba amezalishwa na kina nani na je nani anawahudumia hawa watoto kweli Mungu mkubwa tumshukuru kwa kila jambo.

Huyu mama ni mlezi tu wa watoto hapo hapo anapiga round mjini kwa kigezo cha kuwatembeza kumbe ndiyo anachukua nafasi ya kupigia mizinga pia, kwahiyo analipwa kwa kulea na kuombea. Ni mlezi mzuri kwani anatembeza watoto mpaka mjini. Na unaweza kuta ana nyumba nzuri tu sana.
 
Naomba nijibu swali la ET hapo juu!Ombaomba huyu kazalishwa na serikali yetu!
Mwembe hauwezi kuzaa nanasi!Serikali ombaomba inazaa ombaomba!!!
 
Lol! Soon tutaona kwenye tv mtu anasema naomba serikali initandikie kitanda kama sio kunifagilia uwanja! Tz bwana! Halafu kufukuzwa kazi toka mwaka gani sijui ndo anaona sababu ya kujitembeza bila haya! Kama ana case ya kubakwa aombe msaada wa kisheria. Kuliko nimsaidie omba omba, wale wamama wanaofagia barabara nikikutana nao nawapa buku ya kununua maji ya kunywa! Najua mwajiri wao anawanyonya!
Naomba nijibu swali la ET hapo juu!Ombaomba huyu kazalishwa na serikali yetu!
Mwembe hauwezi kuzaa nanasi!Serikali ombaomba inazaa ombaomba!!!
 
hakuna ombaomba hapo,kwa nini wavue viatu na kuvificha kwa nyuma?
huyu anatafuta wanaume na atawapata.
mi namshauri akakae karibu na ofisi ndogo za ccm pale lumumba hapo labda atawapata walimzalisha.
 
Huyu mama tatizo lake ni kubwa,nadhani anahitaji matibabu ya akili na msaada wa kiroho pia
wakati mwingine utamkuta ana smoke huku anazungumza mwenyewe English na anaongea English nzuri sijui ni nini kilimtokea.
 
munu muondolee kizazi ili maisha aliyonanyo ayamudu..

maisha magumu ila kuna vitu vingi tunavifanya viendelee kuyaongezea maisha kuwa magumu..

ded song Tamaa Mbaya by 20%
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom