Picha hii inatoa ujumbe Gani kwenu?

Muungwana anaonekana yeye kwake mambo shwari; hasumbuliwi na kitu. Makamba naye ki-hamnazo yote kwake ni burdan tu. Karume kaja kikazi na ajenda maalum. Mzee ruksa anataka kutoa usemi/methali mpya-naye haoni taab kabisa. Wengine kwa ujumla wapo hapo basi tu wafanyeje? Naona kwa mbali mzee wa vijisenti kama anahuzunika vile. Bila shaka (kwa wenye intelijensi makini) dhamira zao zinawapasha kwamba hapo mahala ni UNAFIKI MTUPU!
 
Halafu mbona mkaa hapa hajavaa sare yao? au hayumo kiroho ila yumo kimwili?
 
Picha ninayoipata ni kwamba tangu nikiwa mtoto mdogo, nimeona picha ya baadhi ya wajumbe kama akina Msekwa, mwinyi Mkapa na wengine wengi, badala ya kutumia taaluma na wataalam wa ndani, kuandaa mambo kwa kutumia utaalam, wanapiga porojo na kujisifia tu wala hamna kinacho zungumzwa. Usishangae wanakuja na hoja ya kilimo kwanza bila kufanya upembuzi yakinifu. Kweli kilimo cha kutegemea mvua! ( hapa mvua isipo nyesha hamna kitu), pia barabara zetu za vijijini!(ikitokea mvua ikanyesha, utashangaa magari hayawezi kupenyeza ili mazao yapelekwe sokoni na hivyo wakulima wanayasomba kwa vichwa vya binadamu. hili lipo mpaka leo). Utaalam wa kilimo duni!(wakulima wanakwenda mashambani kwa mazoea. Mtu amezaliwa kijijijni alipo kua akakuta kila asubuhi anakwenda na jembe la mkono shambani bila hata kunywa chai, nguvu hana "Its a lot of frustrations! you can't finish to explain". Ndo maana mmoja amekaa kama kabanwa mkojo!
 
mmh,wanajua ushindi ni wao lakini bado wanapanga mikakati namna ya kujiibia kura,na kujiibia wenyewe sasa maana sisi washatukamua wametumaliza,kidumu CHAMA CHA MAJ.......:rolleyes:!MAJUKUMU,KIDUMU.
 
mimi nawaona ni viongozi wa chama cha mapinduzi ngazi ya taifa kutoka tanzania bara na tanzania visiwani. baadhi yao wakiwa katika mavazi ya chama, na wengine wakiwa katika mavazi ya kawaida.
tena wapo katika mjadala mkali na hapa wanamsikiliza makamu wa pili wa mwenyekiti mheshimiwa karume.
sasa sioni tatizo lipo wapi viongozi kukaa kwa pamoja na kujadili maswala ya chama chao.
nawashangaa wanaowaita mafisadi.
hapa tukiangalia maana na ya ufisadi kwa maana yake pana zaidi tunaweza kukuta hata anayewaita hawa viongozi kuwa ni mafisadi pengine naye ni FISADI katika ngazi yake ya familia.
CIAO.
8D6U2314.JPG
[/QUOTE]
 
Nadhani kuna jambo zito linazungumziwa na linawezekan linaiuhusu Zanzibar kwa maana Kiranja ameelekeza macho kwa Amani na Vuai na pia nao wanaonekana wako attentive!!
Pia kwenye picha hii inaonensha kuwa Kamati Kuu yote inaongozwa na wazee na hao ndiyo wneye sauti na nadhani wao ndiyo kikwazo kimojawapo wanaoifanya serikali kuwa na kigugumizi katika utatuzi wa mambo mbalimbali yanayolisbu taifa letu. Wao pia yaweza kuwa ni sehemu ya tatizo!!
Taswira nyingine inaonesha kuwa kuna jambo lina uncertainty linajadiliwa!!
 
Wanawake wapo (see attached...)... Japo wachache... Huyo mwanadada aliyepo upande wa kulia ni nani???
 

Attachments

  • CCCCM.jpg
    CCCCM.jpg
    102.4 KB · Views: 51
Hapo mkuu anaonesha kuna kitu anamshauri, au anataka kufahamu kwa Karume, Makamba kwa umbea umbea anaangalia atajibuje! Mwinyi tayari anajua jibu so anatabasamu kinafki, while Msekwa hajui chochote, hana mwelekeo! Mzee Ben anatafakari kama anaweza share uzoefu
 
picha hii inanipa ujumbe kwamba Msekwa amenenepa sana siku hizi, na Malecela mvi zinamnyemelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom