PICHA: Hawa ndio waliomuua mwandishi wa Channel Ten (Daudi Mwangosi) huko Iringa

Ukifungiwa jf hujafungiwa peponi nadhani itakuwa umefungiwa motoni weka baba au ndio hao akina mura hapo juu???


Sawa, nimeziweka lakini nikifungiwa niteteeni

Ok

Wewe ni mod? Wakinifungia mnitetee.

Kuna haja ya kuomba ruhusa.
 
Huyo jamaa aliyemwelekezea bunduki ndio aliyefyatua nini.!! Duh!!, hawa jamaa sidhani kama ni watanzania.
 
Vitendo kama hivi ni vya kulaani, PM sijui inatumwaje. Mimi si mvuta bhangi, nilikuwa eneo la tukio na nimeshuhudia kilichotokea.

Pole sikuwa namaanisha bangi ila moshi wa mabomu. Hiyo picha yako itakuwa ni diffence ya polisi, marehemu anaonekana kakamata silaha ya askari.
 
Yaani naumia mpaka nashindwa kuelewa hivi polisi nyie mtaishi milele jamani?mnajua nyie mtakufanya je?jamani jamani damu ya mtu hiyo mmemwaga inalia mbele ya Mungu hakika atawalipa msipotubu na kubadilika, sio kisa mna silaha basi, mwishoni sasa tutawaogopa hata barabarani, watoto wetu wanadhana nyie ni wauwaji huu uhasama mnaojenga na jamii haufai anayewapa hii jeuri si Mungu, jamani tumwogopeni Mungu.
 
hizo picha huna, ungekuwa nazo ungeweka na kama mods hawatazikubali basi wataiziba thread tusione...wewe huna picha acha kuleta longolongo hapa.
 
Hivi polisi wa Tanzania huwa wanafundishwa human rights na use of force?
 
attachment.php

Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.
naona huyo askar az if anapull trigger at point black range-hawez kosa mtu hapo
 
Duh!!Nao walikuwa wanaua huku wanapigwa picha?Huku ni kujiamini over kujiamini!!!
Hii kwa kweli ni mbaya sana!!!!!!
 
Mods msiifute hii thread wala kuondoa picha,hiyo picha inaonyesha tukio lenyewe,huyo aliyewekewa bunduki tumboni ndo marehemu?tumekwisha!hii haifai,jeshi la polisi halifai!huu unyama huu ndo mwanzo wa kuiondoa serikali.Hakuna uhalali wa kutawalia kwa namna hii!
 
oooh shit jamani kumbe zile damu ni mtu oooh My yaani hao wote inabidi wafungwe duh
 
Vitendo kama hivi ni vya kulaani, PM sijui inatumwaje. Mimi si mvuta bhangi, nilikuwa eneo la tukio na nimeshuhudia kilichotokea.

mkuu ni hiyo moja tu? weka zote tupe na tukio lilivokuwa inaonekana kama walimvutia pembeni!
 
hivi siku hizi limespecialize kuua tu?
Na hakuna ilijualo zaidi ya kuua na kula rushwa?

Inasikitisha sana!

Mkuu kama una picha nyingine zilizo tuwekee..
 
Pole sikuwa namaanisha bangi ila moshi wa mabomu. Hiyo picha yako itakuwa ni diffence ya polisi, marehemu anaonekana kakamata silaha ya askari.
Marehemu anaonekana akimkumbatia askari kiunoni huku kamera yake ikiwa bado mkononi, na si kukamata silaha.Askari wote hao na bado wakamlipuwa?This is too much na huu ndo mwisho wenu!
 
Back
Top Bottom