Picha: Harambee ya M4C yavuna milioni 323 za kitanzania jijini Dar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
11 August 2012

IMG_0515.jpg

Pichani Juu na Chini ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe akizungumza wakati wa Harambe ya Movement For Change M4C kampeni inayoendeshwa na Chama chake ambapo amesema wana Miaka 3 ya kufanya mabadiliko nchini na kuvitaka vyama vingine vya siasa viungane nao na kuing'oa CCM madarakani mwaka 2015. Jumla ya shilingi Milioni 323 zimepatikana katika harambee hiyo ambapo katika hizo pesa taslimu ni shilingi milioni 70 na ahadi ni milioni 253.

IMG_0506.jpg

IMG_0540.jpg

Wageni waalikwa wakisikiliza sera za CHADEMA M4C kutoka kwa Mh. Freeman Mbowe "(hayupo pichani).

IMG_0575.jpg

IMG_0526.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh.Freeman Mbowe akimtambulisha Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari kwa wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa harambee ya Movement for Change – M4C ya CHADEMA.

IMG_0529.jpg

Mh. Joshua Nassari akitoa salamu kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya harambee ya Movement for Change M4C inayoendeshwa na CHADEMA.

IMG_0608.jpg

Mh.Freeman Mbowe akisalimiana na Jokate Mwegelo aliyekuwa miongoni mwa wageni waalikwa. Katikati ni Sinta.

IMG_06452.jpg

Mh. Freeman Mbowe akipita kila meza ya wageni waalikwa kuwasilimu na kuhamasisha kuchangia chama hicho.
IMG_0616.jpg

Uhamasishaji wa kuchangia ukiendelea kila meza.

Warembo baada ya kuamilisha zoezi la meza kwa meza wakiwa na mabakuli ya mijihela.
IMG_06261.jpg
IMG_0428.jpg

Kushoto ni Blogger Missie Popular, Miss Universe 2012 Winfrida Dominic na Maria Sarungi walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

IMG_0422.jpg

Pichani Juu na Chini ni baadhi ya miongoni mwa wageni waalikwa.

IMG_0432.jpg
IMG_0470.jpg

Mdau Neema Mbuja akitega sikio kwa umakini na yeye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

IMG_0590.jpg

Warembo Jokate Mwegelo na Sinta wakila pozi mbele ya Camera ya MO BLOG.

IMG_0442.jpg

Hapo je imekaa vipi…??? kuamkia leo.

IMG_06851.jpg

People's Power…….Ndio maneno waliyokuwa wakitamka Wafuasi wa chama hicho baada ya kutangaziwa kiasi cha fedha kilichopatikana

.
IMG_0689.jpg

Mh. Freeman Mbowe akiwaongoza wageni waalikwa kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa maalum na chama hicho wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Chadema Movement for Change(M4C) iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam

IMG_0694.jpg

Henry Kilewo naye alikuwepo kwenye harambee hiyo.

IMG_0448.jpg

Hawa ni Baadhi ya Warembo waliokuwa wakikaribisha wageni katika Hafla ya Harembee ya CHADEMA M4C.
 
​london tutakuwa na nyie kwa hali na mali tumewasha moto na hauzimiki mpaka 2015 lazima kieleweke kama noma na iwe noma.
 
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe, pesa zipo nyingi tu tupigishe bakuli nchini ambapo tunapasa misaada ya wenye moyo wa kujenga nchi yetu badala ya kutembeza bakuli linaloshikiliwa na kikwete duniani lenye utaratibu wa mkopo na hivyo kuliongezea taifa mzigo mzito wa deni la taifa kupaa kwa kasi kama ndege angani.
 
Kumbe zilipatikana mil 300 tu??? Pamoja na promo yote, kama wameshinndwa kufikisha lengo la mil 500 walilokuwa wameliweka, vivyo hivyo na 2015 kura hazitatosha!!
 
Kumbe zilipatikana mil 300 tu??? Pamoja na promo yote, kama wameshinndwa kufikisha lengo la mil 500 walilokuwa wameliweka, vivyo hivyo na 2015 kura hazitatosha!!
Nendeni mkamuwekee dhamana Yule mchangiaji mkubwa wa ccm aliyeuwa kwaajili ya kudhulumu Papaa Msoffe hela za watu Kama hao CDM hatuzitaki
 
Nendeni mkamuwekee dhamana Yule mchangiaji mkubwa wa ccm aliyeuwa kwaajili ya kudhulumu Papaa Msoffe hela za watu Kama hao CDM hatuzitaki
Hapa tunaongelea harambee ya CDM, mambo ya papaa msofe yanatoka wapi?

BTW naona kwenye huo mkutano mliwaalika wauza sura wa mjini tu. Sijui mlikuwa mnategea hiyo mil 500 ipatikane vipi.

Ukiangalia kwa haraka haraka gharama za hiyo hafla ni zaidi ya mil.100, then mmepata m.323, most of them ni ahadi za kulipwa within 18 month. Ukiweka provision ya doubtful na bad pledges, unabakiwa na almost nothing. Poor CDM, jipangeni tena kimikakati..
 
Katika harambee hii kuna ujumbe mzito kwa watu makini! picha zinaonyesha kuwa wageni wengi walikuwa ni vijana na watu wa umri wa kati. Lakini wametoa mali zao kwa moyo wa kimapinduzi jambo ambalo si la kubeza hata kidogo, hii kada ina influence kubwa sana katika jamii hii ndio nguvu kazi inayozalisha, inaendesha maofisi nk salam hizi ccm wazisome kwa makini sana.
 
Hapa tunaongelea harambee ya CDM, mambo ya papaa msofe yanatoka wapi?

BTW naona kwenye huo mkutano mliwaalika wauza sura wa mjini tu. Sijui mlikuwa mnategea hiyo mil 500 ipatikane vipi.

Ukiangalia kwa haraka haraka gharama za hiyo hafla ni zaidi ya mil.100, then mmepata m.323, most of them ni ahadi za kulipwa within 18 month. Ukiweka provision ya doubtful na bad pledges, unabakiwa na almost nothing. Poor CDM, jipangeni tena kimikakati..
Ulitaka hizo hela tukapore kwenye maduka ya wahindi huko mjini Kama mnavyofanya nyinyi ccm kwa kutishia TRA itawafilisi wasipochangia
 
Ulitaka hizo hela tukapore kwenye maduka ya wahindi huko mjini Kama mnavyofanya nyinyi ccm kwa kutishia TRA itawafilisi wasipochangia
Kama unawaza hivyo umepotoka ndugu yangu. Sitegemei comment kama hii kutoka kwa mtu anayejiita Great thinker. Hii ungeifanya vijiweni na kwenye baa za gongo ndio wangekuelewa.

Wananchi siku hizi wana uelewa wa masuala ya kodi, huwezi kumtishia mtu TRA watakufilisi. Watu wanatimiza wajibu wao, kwanini wafilisiwe? Ingekuwa ni kirahisi hivyo, ungekuta Mbowe sasa hivi kesharudi kijijini kwao Machame.
 
Mkuu Hebu usiwe muongo kiasi hicho Hukumbuki dr remmy ongala alijaribu kumpigia Mrema kampeni akambiwa siyo raia achilia mbali wakina jenerali ulimwengu.sasa ni wahindi wangapi wanatishiwa siyo raia wasipochangia ccm Hebu acheni hizo tabia . Askofu Yule muuza madini ya tanzanite Arusha serikali ya ccm ilimfanya nini? Watu wanachangia ccm kwa vitisho vya dola. Mkuu hayo mavyakula ya usiku usiku nafikiri yanalewesha ndio maana huyaoni hayo
 
Nchi itajengwa na wenye moyo!

Chadema ni chama cha wananchi na sio chama cha wenyenchi, watafika tu, hata Mbuyu ilianza kama mchicha.

CCM kama sio pesa za majizi kama kina msofe, mzamili, warabu wenye vituo vya mafuta wa hapa Tanzania ingekuwa imeshakufa siku nyingi, kule Visiwani ambapo watu wana vipato vidogo na ata wale wa mjini wanapikia vifuu mpaka kwenye magorofa CCM inatolewaga makamasi kila chaguzi!

CCM hawatakiwi kutishia mtoto NYAU, wanatakiwa watekeleze ilani na haadi za uchaguzi wanazotuimbia kila uchaguzi,ata CHADEMA na wakija wakaanza kutoa ahaadi ambazo awatozitekeleza pia Wananchi watawachoka, ila mpaka sasa wao wapo makini....iweje Rais atoe ahaadi mpaka azikumbuki?

One day CCM will be no more yes I have a dream that one day watu wataamka na kukuta pale magogoni bendera iliobaki yenye rangi ya kijani ni ya Taifa tu na ya Rais zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa CCM wa mwaka 1977
 
Wajinga wataendelea kubeza hii kazi Kuwa sana, hakuna hela za Wakina barick gold kupitia vibaraka deo mwanyika wala tanzanite one za kibaraka ami mpungwe eti zilizochangiwa mkapa foundation wala za bank m wizi na ufisadi mkubwa, hapa tumeonyeshwa Kuwa inaweza kana bila hao
 
Nimependa hayo makopo yaliyo2mika kukusanyia pesa mezani, hapo lazma kila mtu ajifanye mambo safi. Kumbe baada ya pale hana tena hata ya kupanda bodaboda!
 
Kumbe zilipatikana mil 300 tu??? Pamoja na promo yote, kama wameshinndwa kufikisha lengo la mil 500 walilokuwa wameliweka, vivyo hivyo na 2015 kura hazitatosha!!

mbona zimefika mkuu,tena na zaid
 
Lengo ni kupata bilioni 5 lakini wamepata milioni 70 pamoja na ahadi, kama Dar mlipanga kupata milioni 500 ndio sehemu mliokuwa mnaitegemea lengo limekwama...sasa unakwenda kumualika Sinta na Joketi unategemea nini.
 
Mkuu Hivi Mwenzetu unatumia macho haya tunayoyatumia sisi Kuangalia? Je Baada ya Kuangalia huwa unatumia Ubongo kama Wetu Kuandika hapa?

Poor CCM, M4C Haina Huruma Mkuu
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom