picha gani unapata miaka mingine mitano katika utawala wa CCM

inols

JF-Expert Member
Sep 22, 2010
283
95
Miaka mitano iliyopita ilikuwa ni miaka ya mapambano na mafisadi, kuvunja baraza la mawaziri mara kwa mara, safari zisizokwisha, kupanda kwa bei ya bidhaa, kushuka kwa thamani ya shilingi ya kitanzania. Ni miaka ambayo tumeona na kusiakia ya ajabu, kilimo kwanza kwa ajili ya makampuni ya kifisadi kuweza kufanya biashara kwa kumnyonya mkulima wa kipato cha chini, watanzania kutapatiwa vyandarua kwa ajili ya kupambana na mbu katika kampaeni ya malaria haikubaliki. Kwa kweli inasikitisha, sasa hivi tujiandae na shilingi kuwa 2500 kwa dola moja ya kimarekani, tujiandae kwa kodi za ajabu ajabu kurudisha pesa zilizotumika kwa manufaa ya CCM. Tujiandae kwa kilo moja ya unga wa sembe kuwa Sh 2500 na sukari kilo moja kuwa Sh 2800, Nyama 1K=Sh 6000, nauli ya daladal kuwa Sh 400. Kwa kweli tujiandae kufanga mikanda, tujiandae kwa maandamano ambayo hatujawai kuyaona tangia uwepo wa nchi inayoitwa Tanzania. Natamani hii miaka ijayo mitano ipite kwa kasi ya mlio wa sauti 3*10^8 m/s.:A S cry::A S cry::A S cry::A S cry:
 
Back
Top Bottom