Elections 2010 PICHA: Dr. Slaa in Singida today

Nimefurahiswa na habari za Sinhgida kwa sbb huko ndio nyumbani kwa CCM na umaskini ,kama wameamka hongra sana ,baba,mama,kaka ,wajomba ,wadogo zangu SAA YA UKOMBOZI IMEWADIA
 
TBC wameonyesha mkutano wa Dr. Slaa akiwa Singida. Picha ya mkutano huo wameichakachua na wala hawakuonyesha kama kulikuwepo na umati wa watu mkubwa namna hii. Jamani wenye uwezo hakikisheni picha hizi zinayafikia magezeti ya kesho ili zitumike na kuondoa dhana kwamba mkutano ule haukuwa wa watu.

CCM wanatumia kila kilichoko mbele yao kuchakachua na kuonyesha kuwa Dr. Slaa hakubaliki wakati yeye ndiye kipenzi cha watanzania kwa hivi sasa.

kumbe uliona. Tbc wa ajabu sana na wanatia hasira. Niliona huo umati kupitia star tv. Tbc walichoonyesha ni pamoja na dk slaa kukataa jukwaa na kutumia gari
 
inatia moyo kwa kweli, inazidi kunipa moyo wa kupiga kura coz nilikuwa nimeshajikatia tamaa
 
hawa watu wanvipicha vyao viwili vitatu, ndio watapongezana humooo mpa asubuhi. Sehemu nyingine ni chafu tu, hawana kitu.

Kama mimi nadanganya waambie waonyeshe zile za mtwara, lindi, songea na mbeya ni aibu tupu.

Kwenye mtandao nyie ushindi chukueni, lakini mitaani waachieni ccm no 1.



craaaaaaaaaaaaaaaaaa ..
 
[inatia moyo kwa kweli, inazidi kunipa moyo wa kupiga kura coz nilikuwa nimeshajikatia tamaa ]
NYAMAYAO!Ulikata tamaa kwa nini?kweli tupo pamaja kwenye msafara huu?Hakuna kulala mpaka kieleweke!
 
hAWA WATU WANVIPICHA VYAO VIWILI VITATU, ndio watapongezana humooo mpa asubuhi. Sehemu nyingine ni chafu tu, hawana kitu.

Kama mimi nadanganya waambie waonyeshe zile za Mtwara, Lindi, Songea na Mbeya ni aibu tupu.

KWENYE MTANDAO NYIE USHINDI CHUKUENI, LAKINI MITAANI WAACHIENI CCM NO 1.

Jamaa utakuwa hujui ukweli wa mambo,l na sio lazima kila mkoa watu wengi watauzulia mikutano ya kila mgombea, lakini tunaangalia what the big picvture tell us, mikoa mingapi Dr.Slaa anakubalika, huko lindi na mtwara kama hakubaliki doesnt mean Mbeya, iringa, Arusha etc hakubaliki, mwaka tena CHADEMA tunashinda kwa kishindo, tuna mfrash mkuu wa kaya inayotaka kuzama.

So jiandae kuwa na broken heart, make nafikiri wengine mna mapenzi tofauti kabisa na ya kawaida ambayo kila mctu anayaona.
 
Huyo anayesema kuwa ya Tunduma yalimsikitisha kwa taarifa ni kuwa hakuna mgombea aliyewahi kukusanya watu wengi zaidi kama alivyofanya Dr. Slaa pale Tunduma. Shughuli zote zilisimama na watu wanaoonekana kuchoshwa na maisha magumu yaliyotengezwa na CCM walikuwa wakimsikiliza kwa makini mtetezi wao.
Mwendo ni huo huo Dr. Slaa mpaka kieleweke hata kama siyo mwaka huu tutapambana hadi 2015 tuhakikishe CCM inazikwa na haitafufuka tena.
 
Soma gazeti la Tanzania Daima la tarehe 6 Oktoba 2010 ili kuona jinsi alivyovuta watu wengi zaidi pale Tunduma. Sehemu ya gazeti hilo inasomeka hivi:
"... MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa ametoboa siri ya mahusiano ya karibu kati ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, na mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.

Alisema uhusiano wao wa karibu, ulimfanya Luteni Jenerali Shimbo apate zabuni tata ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) na ndio sababu ya kiongozi huyo wa jeshi kutoa kauli ya kuwatisha wapiga kura ili kulinda maslahi yao.
Dk. Slaa, alifichua siri hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma, kwenye uwanja wa michezo katika mkutano huo mkubwa unaoelezewa kuwa umevunja rekodi ya mahudhurio tangu kuanza kwa kampeni za urais.
Dk. Slaa ambaye amekuwa akivuta hisia za wengi kwenye mikutano yake ya kampeni, alisema Shimbo yuko kwenye mtandao wa Rais Kikwete, aliojiunga nao mwaka 2005 na ndio sababu ya kuamua kutoa kauli ya vitishio ili kumlinda Kikwete ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asing'oke madarakani. Akifafanua madai dhidi ya Luteni Jenerali Shimbo, Dk. Slaa alisema aliingizwa kwenye mtandao wa Rais Kikwete mwaka 2005, hivyo alimtaka afafanue kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuhusu usalama wa nchi ni ya JWTZ au yake binafsi inayolenga kulinda mahusiano yake na Kikwete..."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom