PICHA: Dr. Slaa atoa pole kwa familia ya marehemu Mwangosi

Pale walipopanda mti, nyumba ndio iwe na jina la marehemu, hao CCM watautoa huo mti, kama mawe ya msingi yaliyowekwa na Mrema waliyatoa, sembuze mti
 
Hapo kwenye huo mti iwe ni sehemu ya kumbukumbu,panatakiwa pawekwe jiwe la msingi la kumbukumbu pakiwa na jina lake na maelezo ya kilichompata "briefly".May he rest in Enternal Peace.

Mawazo safi sana, ningependekeza uje na action plan ya utekelezaji hapa JF tuijadili na kuanza utekelezaji, ikiwezekana kwa kuwasupport CDM au sisi kama wadau wa Mabadiliko.
 
Chadema kama chama wachukuweni hao watoto muwasomeshe mpaka chuo kikuu, pamoja na kumuangalia mjane, mzazi wao kafa ndani ya harakati za kisiasa za Chadema

harakati za chadema kivipi?kwani marehemu alikuwa mwanachama wa chadema?na je chadema kilikuwa chanzo cha kifo chake? Fikiria kiumakini kwani kutokana na taaluma ya uandishi hutakiwi kuwa mwanachama wa chama cha kisiasi unless unaripoti taarifa ya chama na hushughuliki na kazi nyingine kama mnyika yeye ni mwanahabari wa chama
 
Ukombozi una changamoto na majribu mengi sana!!R.I.P Mwangosi,wewe ni dira na daima utakumbukwa!!!
 
Hakika hakuna chozi litakaloenda bure Mungu awape moyo wa kishujaa upendo amani na mwongozo watoto wa marehemu .
 
It will also come to pass!! Haya ni maagizo ya mkweree kwa jeshi la polisi kuwa waanzishe vurugu kwenye mikutano ya CHADEMA ili wapate sababu ya kukifungia chama!! Sumaye was right kuwa hawa wakipata madaraka kwa staili waliongia magogoni watamwaga damu za wananchi wasio na hatia; utabili huo sasa unatimia. R.I.P. Kamanda Mwangosi.
 
Kamanda Precise Pangolin
Kwanza nitumie vipimo na saizi ya viatu nataka nikutumi pamba ya nguvu; na boot kali upendeze achana na kakhi za kushonesha kwa fundi John; makamanda hamuelweleki serikali ikiwashtaki wahujumu uchumi kelele isiposhtaki kelele, na kuhakikishia kama raisi angetaka Mahalu awe jela leo hii angekuwa jela, lakini ni kwasababu ni mtu anayeheshimu misingi ya demokrasia.

Chama
Gongo la mboto DSM
kwi! kwi! kwi! kwi! teh! teh! Mkuu chama lakini Gwanda lisiwe la kijani naweza nikatapika kila nikilivaa. Nitakutumia kabla hujarudi
 
Wana Jf,msafara wenye majonzi kuelekea itete nyumbani kwao marehemu Daud Mwangosi kwenda kumzika,kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr W. Slaa akiwa na makamanda wa m4c wameambatana na wafiwa kwenda kuzika.Huzuni imetawala kwa wana-rungwe. Source:mimi mwenyewe
 
Wana Jf,msafara wenye majonzi kuelekea itete nyumbani kwao marehemu Daud Mwangosi kwenda kumzika,kiongozi mkuu wa upinzani nchini Dr W. Slaa akiwa na makamanda wa m4c wameambatana na wafiwa kwenda kuzika.Huzuni imetawala kwa wana-rungwe. Source:mimi mwenyewe

Mungu amlaze mahala pema peponi Ameni!
 
Dr.Slaa mnafki sana mikono yake imejaa damu,vurugu zote anaanzisha akafu analala mbele,msala anawaachia wengine,tunasubiri zamu ya mkoa gani damu kumwagika.
 
attachment.php

Mkuu chama ona walichokuwa wanafanya CCM siku hiyohiyo CDM waliyokuwa wanataka wafanye mkutano mwandishi akauliwa na CCM hawakufanyiwa chochote huu ni uonevu
 

Attachments

  • bubuuu.jpg
    bubuuu.jpg
    64.6 KB · Views: 105
nimemsikia muandishi mmoja wa Chanel ten akisema msafara umefika mbeya .... je umeshaondoka hapo .... tuwekee na picha mkuu
 
Najaribu kuvuta taswira, unaona mzazi wako utumbo umesambaratika vile kama siyo binadamu. Mke ambaye 'honey' wake aliyempenda na kumthamini kafumuliwa utumbo, dah, machozi yanatoka.

Hakika Mungu wetu siyo kiziwi. Japo Mungu alisema tutii mamlaka zimetoka kwake, hii ya JK imetoka kuzimu hii, na inabidi irudi kuzimu.
Ni kweli, CDM wanatakiwa kuwaangalia hawa wajane na yatima kwa stahili yake.

RIP MWANGOSI
 
Mweyezi Mungu awatangulie na awape faraja wafiwa wote! RIP Dav
 
Hata kama watauwa watu wote walio ndani ya harakati naamini watazaliwa wengine watakao endeleza harakati na kustawisha mbegu ya mabadiliko.

Mabadiliko yangekuwa yanazuilika kwa mtutu wa bunduki hosein mubarak angefaulu na sasa angekuwa yu ngali madarakani. Ifike hatua ccm wajue kuwa kuwatumia polisi waue hakuta weza kuwaokoa na anguko maana hasira ndio zinazidi kwa wananchi wa kawaida. Huyo mtoto wa marehemu pamoja na mama yake naamini hawawezi kupigia kura serikali iliyo uwa kiongozi wa nyumba (baba).
Kwani huyu muandishi na yeye alikua kwenye harakati zenu?
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom