PICHA: Dr. Slaa atoa pole kwa familia ya marehemu Mwangosi

Duh! Hizi picha zinasikitisha sana.

Ndicho hata mie kinachoniuma moyoni hadi kutoa chozi, kwani wauaji hawaoni hata mtafaruku wa familia yake na hatima yao katika mazingira ya leo ya hali ngumu ya maisha. They are just playing game like bao, it pain.
 
Hapo kwenye huo mti iwe ni sehemu ya kumbukumbu,panatakiwa pawekwe jiwe la msingi la kumbukumbu pakiwa na jina lake na maelezo ya kilichompata "briefly".May he rest in Enternal Peace.

Niko pamoja nawe, jmushi1 jaribu kufikisha suala hili kwa wahusika hasa Kamanda Mnyika atalifanyia kazi, he is very active.

Sehemu aliyouliwa nayo ni muhimu kuenziwa kwa namna hiyo hiyo, kwani hizi ni kumbukumbu muhimu za historia ya nchi yetu yenye kuwatambulisha wajao historia ya wapigania demokrasia ya kweli baada ya ukoloni.
 
Chadema kama chama wachukuweni hao watoto muwasomeshe mpaka chuo kikuu, pamoja na kumuangalia mjane, mzazi wao kafa ndani ya harakati za kisiasa za Chadema
Sawa ila elewa kuwa Marehemu hakuwa CDM. Ingependeza kama ungesisitiza IGP, RPC wajihudhuru kwanza kwa uzembe, then mambo mengine yafuate, kwani kwa mazingira ya picha inaonesha bunduki ilifyatuka kwa uzembe na ushabiki wa askari ili waonekane wamefanya kazi mbele ya RPC aliyekuwepo wakati wanamkata na kumpa kashikashi marehemu.
 
Asante Dr kwakutu wakilisha. Naamini Dr soon atasema yaliyo moyoni kuhusu ili tukio na hatua za kuchukua!

Policcm wameamua kutumia nguvu baada ya kuona wananchi wanazidi kufunguliwa na kujua ukweli.

R.I.P Mwasongwe
Mkuu hapo ulimaanisha au kidole kiliteleza? Sisi tunaomboleza kwa Mwangosi.
 
Inasitisha jamani...Poleni wanafamilia na wote mlioguswa kwa namna moja au nyingine. Mungu awatie nguvu familia yake katika kipindi hiki kigumu. So sad....kwa kweli sisi wote ni wamoja adui yetu namba moja CCM na police wao.
 
Hawathamini kabisa uhai wa Watanzania na athari kubwa kwa familia husika iwapo uhai huo utamalizwa bila kutarajiwa.
 
Huyo mtoto hataipenda CCM Tena na hatawapenda mapolce mpaka anakufa, Ebu mwangalie Alvyofumba macho kwa uchungu mwangalie mikono yake alvyomkumbatia slaa dah
 
RIP Mwangosi!

Hivi viongozi wa wauaji (Said Mwema & Nchimbi) wanajisikiaje? Halafu lile tango pori la magogoni bado liko kimya tu?
 
Niko pamoja nawe, jmushi1 jaribu kufikisha suala hili kwa wahusika hasa Kamanda Mnyika atalifanyia kazi, he is very active.

Sehemu aliyouliwa nayo ni muhimu kuenziwa kwa namna hiyo hiyo, kwani hizi ni kumbukumbu muhimu za historia ya nchi yetu yenye kuwatambulisha wajao historia ya wapigania demokrasia ya kweli baada ya ukoloni.
Hopefuly ataiona kwasbabu huwa anapita hapa.
 
Marehemu ameuwawa kikatili sana,jinsi unavyozidi kuangali vipande vya nyama ya mwili wa marahemu unapata roho ya kisasi maisha yako yote, wakati mwingine auwaye kwa upanga ni vema na yeye akafa kwa upanga.!
 
sikatai chadema kusaidia kwa rambirambi. . . Lakini sio kweli kwamba amekufa kwenye harakati za siasa za chadema.
Your observation is rather skewed and wrong in many ways.

Waue polisi, chadema wachukue jukumu la baba mlezi?

Mdau mwenzetu Bigirita maarufu hapa JF, nipengependa tu kukujulisha kuwa huyu Daud Mwangosi licha ya kuwa kiongozi wa wanahabari Iringa, ni kati ya wanahabari wachache nchini tulio nao ambao hawayumbishwi kwa woga au kuficha habari.

Kwa taarifa yako mmoja ambaye alikuwa anaanika habari live za vyama vyote bila kigugumizi ni Mwangosi tofauti na wanahabari wengine ambao huchagua na hata wanapolelekewa habari naye walikuwa wanazichakachua.

Nikupe mfano mmoja kati ya wanablog maarufu mji wa Iringa ni Mjengwa na Francis Godwin. Mwangosi alikuwa kiungo mojawapo chao cha habari, lakini katika mitandao hiyo miwili unaweza kuona mmoja ulikuwa unajitahidi kuziweka habari hata za Chadema bila kigugumizi, lakini mtandao mmoja sitaki kuutaja kati ya hiyo miwili anaonekana wazi alikoegemea, na hata habari ya tukio hili amejitahidi kuchakachua sana kama ilivyofanya Habari leo.

Kati ya wapigania haki katika ukombozi wa kifikra, demokrasia, uchumi, elimu na mengineyo, katu huwezi kuweka kando vyombo vya habari. Huyu ameuawa akiwa katika kumpigania mwanahabari mwenzake wa IPP ambaye alikuwa anapigwa na Polisi. Asingekuwa na uchungu wa kweli wa demokrasi asingethubutu kumfuata kiongozi wa polisi na kuuliza kulikoni mnamtesa na kumnyanyasa mwanahabari ambaye yuko kazini kama polisi wenyewe.

Historia inajirudia wazi Daud Mwangosi ni mmoja wa kukumbukwa katika kumbukumbu za ukombozi wa kifikra na demokrasia nchi, na ndivyo hata nilichokiona kwenye CNN katika habari zao. Lets united together to deal with them.

Jaribu kutalii katika ulimwengu wa wapigania haki, utakutana na wanahabari ambao katika kuungana na wananchi kupigania haki walifikia yaliyomsibu Mwangosi. Kama si kupigania haki na demokrasia, wakati akijua hatari zilizoko katika mikutano hyo kwa nini alijitosa kumfuata RPC kujua uhakika wa ratiba ya mikutano ya Chadema? Alipozungushwa bila kupewa jibu na RPC aliamua kufuata msafara wa mikutano hiyo hadi kukumbana na yaliyompata, nini tena tukuhakikishie mdau kwamba amekuwa mpiganaji katika kuungana na wapenda mabadiliko nchini?
 
wamebaki yatima kivipi wakati mama yao yupo!!! Inamaana siku hizi akifa mzazi mmoja watoto wanakuwa yatima?????

Unataka kusema kwa sababu mama yao yupo basi watoto sio yatima, na kwa maana hiyo mama yao sio mjane...??
 
I think kwa sababu za kiafya napaswa kulog out kwenye hii thread inaweza kunisababishia matatizo makubwa ya kiafya, kipimo cha kuvumilia unyama kama huu kimefikia kwenye maximum level, i can not handle this.
 
Mimi nimesikitika sana jamani. Hivi jamani lile bomu ni la machozi kweliiiiiii???? Nakumbuka hata kule Dodoma katika kijiji cha Njedengwa watu walipigwa risasi za moto na mabomu ya moto kama hili lililomuua ndugu yetu Mwangosi. Tusiishie kusema R.I.P we have to do something more abt these Police and their government.
Ukatili wa Jeshi la Polisi Njedengwa - YouTube
 
I think kwa sababu za kiafya napaswa kulog out kwenye hii thread inaweza kunisababishia matatizo makubwa ya kiafya, kipimo cha kuvumilia unyama kama huu kimefikia kwenye maximum level, i can not handle this.

Wengi yametupata yanayokupata mwenzetu, ndio hali halisi ilipo, tunatakiwa kutokata tamaa kwani unapoona magumu ujue ndio ngazi ya kupandia kwenye ushindi, ushindi hauji kwa ulaini.
 
Mkuu Ritz
Angalia picha utaona wenye majonzi ya kweli na wanafiki waliokwenda kutafuta picha za magazeti; Dr. Slaa anaona hata aibu kuingalia kamera kwasababu ya dhambi unafiki inamsuta, masikini kama watoto uyatima kwa tamaa za kisiasa inasikitisha sana. R.I.P Mwangosi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom