Picha - Design ya apartment iliyotulia India, nakunwa kichwa

Kwani nani amesema akiishi humo atamsahau Muumba wake? Kama binadamu wote wangekuwa na mawazo kama yakwako, Dunia ingekuwa bado inagaragara kwenye karne ya kwanza kimaendeleo.

Umesema kweli tupu.

Aliyefanya yote hayo yafikie yalipo katika maendeleo ni Mungu, na ni Mungu huyo huyo atakaya kuhukumu kwa kutotumia akili aliyokuwa kuendeleza ulimwengu.
 
Nimekusoma mkubwa Kwapa, ni jazba tu ya watu kudharau wataalamu wao wa ndani. Uchumi wetu ni mdogo sana kufikia point ya kujenga majengo kama haya.

Mkuu coby, asante kwa mchango wako hapa!

Awali naweka wazi kwamba mimi ni mtaalamu mmojawapo wa ujenzi!

Mkuu kuna watu wengine wanatoa mawazo yao bila hata ya kushirikisha bongo zao!
Hivi tunasema madaktari wa Tanzania ni viazi kwa kua hatuna hospitali kubwa ya moyo?
Au tuseme wasomi wetu wa TEHAMA ni viazi mbatata kwa kua hatuna kiwanda cha Sony au Dell Tanzania?
Au tuseme hatuna wanasheria kwa kuwa kuna wafungwa wengi? na wizi wa EPA?
Au wahasibu ni pumbavu kwa kuwa kuna wizi wa fedha za umma?
Au walimu wote ni maboga kwa kua hatuna shule nzuri?
Kwamba kuna fani isiyo na matatizo hapa Tanzania kwa umaskini huu???

Hivi wanajua kwamba wasanifu wengi tu wa majengo na miji ya uarabuni sio waarabu?
Hivi wanajua ugumu wa kusanifu jengo (au chochote) kwa 'Client maskini'? Kwamba hana hela za kutosha lakini anataka nyumba bora! Mnaelewa lakini??? Au mnajua tu kufungua midomo bila kutumia bongo zenu??
 
Last edited by a moderator:
Mimi ni Mhandisi wa umeme (Electrical Engineer),Ngoja niwape shule kidogo sio mnaropoka ropoka tu kama majuha;
1. Jengo hubuniwa na Msanifu majengo (Architect) kulingana na mahitaji, matakwa na uwezo wa mteja wake ili mradi sheria za miji zinaruhusu; jengo unaloliona hapo ni matokeo ya kazi ya Msanifu majengo ambaye hubuni na kuliweka katika taswira inayoeleweka wazi kwa mteja wake (3D view) kama linavyoonekana hapo juu

2. Baada ya jengo kubuniwa Mhandisi ndio anaanza kazi yake. Hapa kuna wahandisi wengi lakini muhimu sana ni Structural Engineer (nimeshindwa kiswahili chake). Huyu ndiye anayeweza kusema hili jengo linawezekana kujengeka au la. Kumbuka Architect anaweza kubuni umbo lolote analoona linampendeza lakini je linaweza kujengeka likafaa kwa matumizi au la hiyo ni kazi ya huyu Mhandisi.

Huyu ndiye atakayesema kulingana na umbo hili la jengo basi linatakiwa liwe na chuma au nondo au mchanga au saruji au kokoto gani, kiwango gani na kiasi gani katika kila sehemu ya jengo hilo ili kuliwezesha umbo hilo litokee na matumizi yanayokusudiwa yawezekane pamoja na kuhimili changamoto mbalimbali kama uzito, upepo, mafuriko na matetemeko.

3. Mjenzi (Contractor). Huyu ndie anayelijenga jengo. Huyu kazi yake yeye ni kujenga kila kitu kulingana na matakwa ya Engineer na Architect. Kama kaambiwa weka nondo sita za zaizi flani ataweka hivyo tu na si vinginevyo hadi jengo linaisha.

Baada ya kukupa shule hiyo nadhani utakua umehamishia kejeli kwa Architect. Tambua kwamba hakuna jengo liloshindikana kubuniwa na kujengeka Tanzania kwa wataalamu wa Kitanzania. Tatizo ni Mteja gani anayeweza kumudu ghalama ya kulijenga hilo jengo Tanzania? Au mnadhani wataalamu ndio wenye hela za kujengea kila aina ya jengo!

Nakumbuka kuna Mwalimu alipoambiwa umeme unaozalishwa Tanzania hautoshelezi mahitaji akadakia harakaharaka eti "sasa nynyi Wahandisi wa umeme kwa nini hamjengi mitambo ya kutosha"! Ikabidi nimuwahi kwa kumuuliza swali hilo yeye "sasa nyinyi walimu mnaona shule hazitoshi kwa nini hamjengi shule za kutosha"!

Tuache kudharauliana bila sababu.

Hongera kwa kazi ya kuwaelimisha hawa watu. Wameimbishwa vibwagizo na wanasiasa sasa kila kitu ni kejeli tu na ujuaji mwingi wa kukurupuka. Uhandisi si imani ya dini ukiombea pepo anatoka. Leteni pesa watu wawafanyie vitu na wanasiasa wakae mbali
 
unatumia kinywaji gani please coz umenikuna, na umewakuna wengi pia maana kwenye huu mtandao watu wanaropoka tu kama wawezavyo.
 
Mkuu coby, asante kwa mchango wako hapa!

Awali naweka wazi kwamba mimi ni mtaalamu mmojawapo wa ujenzi!

Mkuu kuna watu wengine wanatoa mawazo yao bila hata ya kushirikisha bongo zao!
Hivi tunasema madaktari wa Tanzania ni viazi kwa kua hatuna hospitali kubwa ya moyo?
Au tuseme wasomi wetu wa TEHAMA ni viazi mbatata kwa kua hatuna kiwanda cha Sony au Dell Tanzania?
Au tuseme hatuna wanasheria kwa kuwa kuna wafungwa wengi? na wizi wa EPA?
Au wahasibu ni pumbavu kwa kuwa kuna wizi wa fedha za umma?
Au walimu wote ni maboga kwa kua hatuna shule nzuri?
Kwamba kuna fani isiyo na matatizo hapa Tanzania kwa umaskini huu???

Hivi wanajua kwamba wasanifu wengi tu wa majengo na miji ya uarabuni sio waarabu?
Hivi wanajua ugumu wa kusanifu jengo (au chochote) kwa 'Client maskini'? Kwamba hana hela za kutosha lakini anataka nyumba bora! Mnaelewa lakini??? Au mnajua tu kufungua midomo bila kutumia bongo zenu??

Mkuu RR maswali yako yote ni ya msingi sana. Imefikia wakati Watanzania hatutaki kabisa kufikiri, siasa imetuharibu fikra na sasa kila tatizo letu ili kulitatua tunaanzia kisiasa na tunajikuta hatufikii hata kwenye utaalamu na mbaya hata zaidi utatuzi wa kisiasa ni wa kuiga walichofanya au wanachofanya wenzetu bila kufikiria tupo wapi kiuwezo na tufanye nini ili tuweze. Watu hawatambui kwamba hata hilo jengo linaloonekana hapo kuna uwezekano mkubwa kuna mkono wa Mtanzania, tunaishia kudharauliana tu. Inasikitisha kwa kweli kuona tuna akina Kova wengi kweli in my beautiful Country,TZ
 
Hongera kwa kazi ya kuwaelimisha hawa watu. Wameimbishwa vibwagizo na wanasiasa sasa kila kitu ni kejeli tu na ujuaji mwingi wa kukurupuka. Uhandisi si imani ya dini ukiombea pepo anatoka. Leteni pesa watu wawafanyie vitu na wanasiasa wakae mbali

Umenichekesha sana mkuu Sorrow to Joy, nikakumbuka na speech ya Mch. Msigwa Bungeni, "...We don't pray for this..."
 
Hili jumba ambalo lingali katika ujenzi (under construction) huko Mumbai - India lina mvuto pekee na wa aina yake.

Poor us...we are always trying to create 'heaven' on earth, it wont happen..hata ukilala humo bado haitakuwa pepo kwako, as you will always feel that something is missing...and too bad that you will never figure out what is it!
 
Kwa kauli yako unapingana mwenyewe, kwani una mengi tu uyafanyayo kwa ajili ya kujenga maisha yako. Kwa nini ufanye hayo wakati unasubiri hadi uende peponi ambako utapata raha iliyokamilika? Muumba katupa akili tuzitumie kwa ajili ya kuutengeneza ulimwengu uonekane mzuri.
 
Back
Top Bottom