PICHA; CHADEMA Yazidi Kuikalia Kooni CCM

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
H1.jpg



H2.jpg


H4.jpg


H5.jpg
Godfrey Chikandawali alipokuwa akitambulishwa rasmi baada ya kuvua gamba na kuvaa gwanda
h6.jpg
John Heche Mwenyekiti wa BAVICHA akihutubia mkutano wa wananchi wa Mwenge wilaya ya kinondoni


CHADEMA Imeendelea kuwatesa wapinzani wao CCM kwa kuendeleza kwa kasi kampeni yake ya VUA GAMBA VAA GWANDA,ambapo jana jioni kabisa Mwenyekiti Vijana (BAVICHA) John Heche aliwapokea wanachama wengi wa CCM walioamua kujivua magamba na kujiunga na M4C.

Anayeonekana na gwanda jeusi pichani akiwa na mwenyekiti heche ni ndg Godfrey Chikandamwali aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa CCM wilaya ya Kinondoni,pamoja naye ni ndugu yake Anna Chikandawali mjumbe wa UWT wilaya, na wengine wengi.

Heche amepokea wanachama hao Mwenge jijini Dar es Salaam

Picha kwa hisani ya Jackson Makala
 
Leo Chadema Yaikalia kooni Ccm, kesho utaskia Chadema yaikalia mapajani CCM tabia hujenga mazoea shauri yenu!
 
Huyu Chikandamwali ameogopa fedhela, kwa vile alikuwa mbioni kutemwa na chama chetu kwa ajili ya UFISADI
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Kamanda John Heche ameendelea kuwa mwiba mkali kwa chama cha mapinduzi. Kwa mara nyingine tena jana amefanikiwa kupokea wananchama zaidi ya 100 kutoka ccm katika mkutano wa hadhara alioufanya jana jioni maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa watu waliorudisha kadi za ccm na kujiunga na Chadema ni pamoja na Bw.Godfrey Chikandamwali aliyekuwa Mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm wilaya ya Kinondoni pamoja na Bi.Anna Chikandamwali aliyekuwa mjumbe wa uwt wilaya ya kionondoni.
 

Attachments

  • Heche1.jpg
    Heche1.jpg
    80.1 KB · Views: 109
  • Heche2.jpg
    Heche2.jpg
    100.1 KB · Views: 135
  • Heche3.jpg
    Heche3.jpg
    104.5 KB · Views: 92
  • Heche4.jpg
    Heche4.jpg
    107.9 KB · Views: 80
  • Heche5.jpg
    Heche5.jpg
    66 KB · Views: 120
  • Heche6.jpg
    Heche6.jpg
    81.2 KB · Views: 91
  • Heche7.jpg
    Heche7.jpg
    76.8 KB · Views: 81
  • Heche8.jpg
    Heche8.jpg
    90.4 KB · Views: 107
  • Heche9.jpg
    Heche9.jpg
    94.1 KB · Views: 95
Ccm nikopo lilo toboka cdm inapokea vitu vinavyo mwagika leo hamtaiyo ila 2015mtakiona kilicho mtoa kanga manyoya
 
Back
Top Bottom