Picha: Chadema warudisha fomu Igunga

Mbona sura zao hazioneshi matumaini? Yaani ni kama watu waliokata tamaa hata kabla ya mchezo. Kuna umuhimu gani kuingiza timu wakati unayetaka kucheza naye ni klabu bingwa milele? Je huku si kujitafutia kilio?

Hapo pekundu: Elimu yako ni darasa la ngapi vile? Try 2 use your small brain properly brother. Hao raia wana machungu ya hali mbaya ya maisha na hawako kwenye kinyang'anyiro cha kugombea miss vodacom kuwafanya watabasam bila sababu. Halafu unapotolea mfano wa timu unaniudhi kwani unanikumbusha kiwango cha soka Tanzania kwa miaka 50 ya uhuru na Taifa Stars chovu. Klabu bingwa milele ni ipi kwa mfano wako? Rushwa, Ufisadi, Umasikini, Njaa, Ukimwi, au Maji taka badala ya Maji salama?

Mbona sura zao hazioneshi matumaini? Yaani ni kama watu waliokata tamaa hata kabla ya mchezo. Kuna umuhimu gani kuingiza timu wakati unayetaka kucheza naye ni klabu bingwa milele? Je huku si kujitafutia kilio?

Kilio mara ngapi???!!! Nchi nzima inalia mfano hakuna!!!.. na chanzo cha kilio unakijua!!!... halafu unaongea habari za kujitafutia KILIO??!!!... Nafikiri.. kajipange upya.....

Big up sana Easyfit,

Haya ndiyo mambo tunayotaka ili kina Rejao, Mwita25 na FaizaFox wajue watanzania wako wapi. na wanataka nini

Mbona sura zao hazioneshi matumaini? Yaani ni kama watu waliokata tamaa hata kabla ya mchezo. Kuna umuhimu gani kuingiza timu wakati unayetaka kucheza naye ni klabu bingwa milele? Je huku si kujitafutia kilio?

Acha mambo ya kitoto, nyie ndio mlioifikisha nchi hii kwenye hii taabu ya maisha, Huna jipya hata kidogo. Onyesha hao wa CCM walio na furaha labda wewe unayekula na kunywa pasipo kufanya lolote.

Na wasi wasi wewe hadi leo hii unajua Kuku wanafugwa kwenye friji, nyanya na Mchicha unalimwa kwenye friji.

Eti kila siku unawauliza watu hivi njaa ikoje?

Acha mbwembwe hizo.

Shime wana Igunga tuondokane na chama ambacho hakiguswi na matatizo yetu ya Msingi hasa umaskini,elimu duni,miundo mbinu duni,huduma za afaya na jamii duni.
Mwana igunga tafakari na uchukue atua

Nina hoja tofauti; Philosophy inasema ukimfundisha mtoto kwamba nyumba inaitwa daraja, na mayai yanaitwa bahari, basi mtoto huyo atakuamini ila tu atatofautiana na wewe kama atakuwa mdadisi na mwenye kutaka kujua kwa nini majina hayo yanaitwa hivyo.

Uwingi wa watu sio guarantee ya ushindi na wala kuvaa mavazi ya chama sio kuunga mkono mgombea, lakini sana kuunga mkono mgombea sio kumchagua kwa kuwa kura ni siri ya mtu kulingana na utaratibu ulivyo. Cha msingi hapa ni kuhakikisha kila anayeshabikia mgombea wa cdm ana kadi ya kupiga kura na ana kadi ya chama na ni mzalendo. Hilo litafikiwa kwa kufanya kampeni kwa ukaribu sana na wapiga kura, maana yake zaidi ya kupanda jukwaani ama kuporomosha muziki wa densi mikutanoni.

Haina ubishi kwamba cdm sasa watanzania wanaiamini sana lakini ni wangapi wana nia ya kuipa dola? No hapo ndio tunarudi square 1 kwamba tuna kazi ngumu mbele yetu. Sina haja ya kutoa sifa kwa kitu nisichokijua kwa kuwa hakuna ajuaye kesho, ila ninashauri na kuwazua kulingana na mazingira, tunahaitaji wapiga kura na sio kujaza watu bila maana, Mrema analijua hili na gari lenye kutumia watu ili litembee matokeo yake hata 50% hakugusa.

Cdm, lazima isiishie kuona watu wakijibu 'Powerrrr; bila kujua hiyo power nini maana yake na inaishia wapi; sasa kama power mbona mambo kwa sasa ni mzobemzobe halafu hatuoni maana ya power? Daima tutashauri na kutoa maono yetu ili 2015 tuchukue dola na sio kuleta picha ambazo hazina vithibitisho kwamba zina maana yeyote kwetu.

JF, Napenda kutoa hoja.

mkuu hapo umenena!

quote_icon.png
By Mwita25 Mbona sura zao hazioneshi matumaini? Yaani ni kama watu waliokata tamaa hata kabla ya mchezo. Kuna umuhimu gani kuingiza timu wakati unayetaka kucheza naye ni klabu bingwa milele? Je huku si kujitafutia kilio?
Unataka wawe kama hawa,,

ROSTAM.jpg

Back
Top Bottom