Picha: Bweni lililomliza Naibu Waziri Mahiza Tanga

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
mzee-mwanakijiji-albums-news-worthy-picture463-bweni.jpg

Hili ndiyo Bweni la wanafunzi wavulana wa shule ya Sekondari Zingibar ambalo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza alitembelea ghafla na kutoa machozi baada ya kukuta mazingira yake mabovu, bweni hilo wanaishi jumla ya wanafunzi 25.

Na Dege Masoli ,Mkinga .
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, mwishoni mwa wiki iliyopita alilazimika kutoa machozi mbele ya kadamnasi baada ya kufanya ziara katika shule ya Sekondari ya Zingibari iliyopo Wilayani hapa. Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza ya kukagua shule hiyo ambapo alikuta wanafunzi wakiishi katika hali mbaya ikiwemo uchakavu wa mabweni. Alikuta wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo wakiishi katika nyumba chakavu ya makuti ambayo.

Maoni:
Kwa wanafunzi hawa ukiwauliza ni kitu gani wanakihitaji sasa hivi ili elimu yao iwe katika mazingira mazuri, vitambulisho vya smart card au makazi yenye hadhi na heshima ya mwanadamu. Bila ya shaka watataka makazi ili wawe salama.

Ukiliuliza swali hilo hilo kwa serikali watasema "wanahitaji vitambulisho hivi vya kisasa ili tuweze kujua wako wangapi, afya zao, na ili tuweze kuweka mkakati wa kuwapatia jengo zuri linaloendana na mahitaji yao.".
 
Hili ndiyo Bweni la wanafunzi wavulana wa shule ya Sekondari Zingibar ambalo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza alitembelea ghafla na kutoa machozi baada ya kukuta mazingira yake mabovu, bweni hilo wanaishi jumla ya wanafunzi 25.

Na Dege Masoli ,Mkinga .
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, mwishoni mwa wiki iliyopita alilazimika kutoa machozi mbele ya kadamnasi baada ya kufanya ziara katika shule ya Sekondari ya Zingibari iliyopo Wilayani hapa. Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza ya kukagua shule hiyo ambapo alikuta wanafunzi wakiishi katika hali mbaya ikiwemo uchakavu wa mabweni. Alikuta wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo wakiishi katika nyumba chakavu ya makuti ambayo.

Maoni:
Kwa wanafunzi hawa ukiwauliza ni kitu gani wanakihitaji sasa hivi ili elimu yao iwe katika mazingira mazuri, vitambulisho vya smart card au makazi yenye hadhi na heshima ya mwanadamu. Bila ya shaka watataka makazi ili wawe salama.

Ukiliuliza swali hilo hilo kwa serikali wanaweza kusema "wanahitaji vitambulisho hivi vya kisasa ili tuweze kujua wako wangapi, afya zao, na ili tuweze kuweka mkakati wa kuwapatia jengo zuri linaloendana na mahitaji yao.".
 
Vipao mbele vya serikali hii vina walakini na maswali mengi kuliko majibu.
 
wengi wanaweka hizi priority kwanza , hawajui hali halisi au ndio wanachukulia DSM kama ndio Tanzania, pili wamejaa choyo na ubinafsi, tatu hawana uzalendo kwa taifa hivyo hawajui lipi la muhimu na lipi si la muhimu. Hata huyu waziri katu asingetoka machozi kama asingetembelea huko!
 
Bweni lenyewe hili hapa. Inasikitisha sana.
 
Attachments

  • Bweni.bmp
    446.3 KB · Views: 494
Hiyo ndio Tanga bwana, kuna Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya, Afisa elimu, Waratibu, Wabunge, Wananchi, pamoja na Wizara/Serikali kwa ujumla, NDIO TANZANIA YETU HIYO.
 
Huko Mkinga wazazi je hawana mwamko wa elimu? Nani mbunge wa huko? Maana sehemu zingine kama mkoa wa Kilimanjaro hata mabanda ya mifugo siku hizi hujegwa na tofali na kuezekwa bati!

Ni aibu kwa Tz 2009!
 
Last edited:
Bweni lenyewe hili hapa. Inasikitisha sana
Hivi mpaka lini tutaendelea kulea hawa mafisadi al hali ndugu na jamaa zetu wanakosa hata sehemu ya kulaza vichwa vyao wakisubiri asubuhi kuingia darasani.Na je kama bweni liko hivyo hicho kifungua kinywa kitakuwaje?.Na je darasani kutakalika "umaskini huu,umaskini huu,umaskini huu utaisha lini".
 
...wakulaumiwa pia ni hao wazazi wanaolipa school fees na kutoa pesa ya bweni bila kujali watoto wao wanalala wapi,

...hali isingefikia hivi!
 
At least something alternative to MENGI vs ROSTAM episodes

btw kule Mbagala hali inazidi kuwa mbaya apparently wamekufa wanajeshi wengi kuliko tunavyoambiwa

kuna thread ya Hussein Mwinyi sijui iko wapi nimejaribu kuisearch lakini wapi!!
 
Ninyi mnayoishangaa hii picha mnahitaji reality check...mbona mambo kama haya yapo kibwena hapa bongo?
 
uwiiiiiiii!!!!! Maskini sijui wanasomaje hawa watoto. Sasa mvua ikinyesha si hatari, ndio maana naibu katoa machozi maana inasikitisha mno.
 
Huyo mama naye mimi sijaelewa sababu ya hicho kilio chake. Yaani anathubutu kupretend kwamba hajuwi kuwa hayo ndio maisha ya majority ya Tanzanians? If that is the case then haijuwi tanzania zaidi ya kuijuwa Dar-es-salaam na Dodoma tu. Nyumba nyingi vijijini tena huko Tanga ndio zaidi ziko kwa syle hiyo so cha ajabu nini au kwa kuwa ni bweni? I do not see any difference anyway sielewi kwa kweli. Ile nyumba ya yule bibi kizee jk alimtembelea Tanga maeneo ya Korogwe hakuna tofauti kubwa na hilo Bweni. Mama Mwatum usiishie kulia tu it won't help do something. Hayo ndio maisha ya wale wanaowapaga ushindi wa Tsunami.
 
Back
Top Bottom