Picha: BAVICHA wakiwa mjini Morogoro

Kweli Bavicha mnatupa matumaini vijana wenzenu. Hongereni kamanda Munishi (Katibu mkuu) na Heche (Mwenyekiti)

Naamini hamtatuangusha Vijana tulio nyuma yenu. Ila itakua vema tukajua sumu mliyomwaga huko Morogoro.

Jamaa walikwenda kufungua matawi ya vijana na taarifa iliyopatikana ni kwamba wamefungua matawi manne yenye wanachama 187, wamefungua ofisi ya kata, wamehutubia mkutano wa hadhara na wamechangisha pesa taslimu kwa ajili ya shughuli za chama huko Morogoro.

Munishi aliwashambulia vijana wa Morogoro kwa kukubali kusababisha hali ngumu ya maisha kwa vijana wengine Tanzania kwa kukubali kuikumbatia CCM na kuifanya kama dini yao. Pia aliwaambia ugumu wa maisha unaowakabili ni makosa yao wenyewe na hivyo ni kujiunga na CDM ili kuunganisha nguvu zao na vijana wengine Tanzania kuiondoa CCM iliyokosa dira, mipango, na mikakati thabiti ya kuliongoza taifa. Aliendelea kuishambulia CCM kuwa imeoza kiasi kwamba hata malaika ashuke kutoka mbinguni kuiongoza Tanzania kupitia chama hicho ni lazima atafail tuu. Aliwataka kutambua kuwa hatma ya taifa hili liko mikononi mwa vijana. Wakizembea tu watakua wanawanyanyasa wazazi wao, wadogo zao, watoto wao na hata wajukuu wao na laana itakua juu yao.

Kamanda heche alitetemesha Morogoro kwa kuwataka vijana kuiunga mkono CDM kudai katiba mpya ya ukweli na sio ya kihuni huni. Katiba ambayo itapunguza mamlaka ya raisi, katiba itakayoweka ardhi mikononi mwa wananchi, katiba itakayoilazimisha serikali kuwapatia wananchi huduma za kijamii kama elimu na afya ili ikishindwa watu waweze kuishtaki. Katiba itakayoweka mamlaka ya nchi mikononi mwa umma tofauti na ya sasa iliyokaa kinafki nafki hivi.

Aligusia swala la mgomo wa madaktari na kuitaka serikali kuweka wazi madhara yaliopatikana kutokana na uzembe wake wa kutokushulikia madai ya madaktari.

Haya ndio niliyorushiwa na kamanda mmoja ambaye ni mwandishi wa habari huko Moro wazeiya!
 
Duu, Kweli huu ulikua ni mkuki wa moyoni. Ukweli mtupuuuuuuuuuuuuuu! Nawavulia kofia kwa mistari yenu yenye vina. tunafurahi kusikia mnaunganisha nguvu za vijana makamanda wetu. Heko Munishi, Heko Heche.
 
Hadi Morogoro wameitika kiasi hiki,hz ni dalili za siku za mwisho kwa gambaz

Hakuna anayeweza kuhimili mziki wa CDM. Kila mtu na kiu ya kuwasikiliza si Dr slaa, si Mbowe peke yao bali hata vijana kama hawa.
Kwa hali hii inaonyesha kuna Mwenyekiti na katibu mkuu wa Chama kwa miaka ijayo ndani ya CDM taifa.
 
BAVICHA wanawashinda kwa mbali sana UVCCM....kwa organaizesheni....wanafanya vema kazi ya siasa......unaona kabisa ni vijana ambao wamejiandaa kushika dola.....ukiangalia vijana wa ccm ..huoni wakiwa na vishen ya kuendelea kushika dola......kutwa ni kulalamika kuwa wazee wanataka kuwapa wapinzani nchi..vijana wa ccm wamekata tamaa...na wanayo haki ya kuwa hivyo...

Kwanini mnafanya kazi kwa kujilinganisha na fulani na fulani?
Ni sawa na uko mbele kwenye marathon afu kila baada ya mita100 unaangalia nyuma for what?
Mna iogopa sana CCM?
Maana kila mnacho kifanya mnalinganisha na UVCCM,au CCM,....au akifanya kitu Mnyika mna mlinganisha na Nape
damn.
Jiamini bana.
 
Mimi nafurahi sana huku kwenye madrassa zetu CHADEMA CHONDE CHONDE HAWA BAVICHA MUWATUMIE VIZURI WAINGIE MIKOANI WANAHITAJIKA SANA KILA KONA HASA HUKU TANGA,SONGEA,PWANI, MH MBOWE HEBU WEKA MSUKUMO BAVICHA IIKIWA NJE YA BUNGE NA WEWE UKIWA NDANI YA B UNGE KM TUKO SERIOUS KUCHUKUA NCHI 2015 BASI SILAHA ZA KUTANGULIZA MBELE TUNAZO WAPEWE UWEZESHO WAENDE MIKOANI NA KILA CHAMA KINAPOHITAJIKA AHSANTE MH HECHE WANAOSEMA HUWEZI SASA WAMEONA,MUNISHI PANGA MIKAKATI KAZI IPIGWE WATUMIENI SANA WABUNGE VIJANA KM LEMA,SUGU,MNYIKA,SILINDE,WENJE,MAchemli,lissu,msigwa sambazeni ujumbe huo ni utume Viva Chadema
 
Kwanini mnafanya kazi kwa kujilinganisha na fulani na fulani?
Ni sawa na uko mbele kwenye marathon afu kila baada ya mita100 unaangalia nyuma for what?
Mna iogopa sana CCM?
Maana kila mnacho kifanya mnalinganisha na UVCCM,au CCM,....au akifanya kitu Mnyika mna mlinganisha na Nape
damn.
Jiamini bana.

Wewe mwenyewe ulivyoandika hapa hujiamini na ndio maana unaona wenzako hawajiamini? Chadema ni lazima ijilinganishe na CCM kwa sababu ndio waliolididimiza taifa hili na kama chama mbadala lazima kijiepushe na ugoro huo wa masaburi likewise BAVICHA Vs UVMasaburi. Fungua akili yako!
 
vijana hawa wananikumbusha enzi tunatafuta uhuru wa nchi hii nimeipenda sana muundo wao wa harakati ni mzuri sana chama kazi kwenu vijana mnao muwatumie
 
Kazi nzuri kabisa, wacheni viwavi wa Nape waendeleze ***** wao kwenye mitandao nyie twangeni kote kote, kitaeleweka tu, watanzania siyo wajinga kihivyo, wakielemishwa wanaeleimika.ELIMU YA URAIA NI MUHIMU SAAAAAAAAAAAANA.
 
Kwanini mnafanya kazi kwa kujilinganisha na fulani na fulani?
Ni sawa na uko mbele kwenye marathon afu kila baada ya mita100 unaangalia nyuma for what?
Mna iogopa sana CCM?
Maana kila mnacho kifanya mnalinganisha na UVCCM,au CCM,....au akifanya kitu Mnyika mna mlinganisha na Nape
damn.
Jiamini bana.

Kwa msomi unapofanya uchambuzi lazima ulinganishe mambo mawili au matatu kabla ya kuhitimisha. Ndiyo maana tunapojivunia mafanikio ya miaka 35 ya CCM tunatazama nyuma, kule tulikotoka. Hali ya sasa na ya nyuma inapokuwa tofauti ndipo tunaposema tumefanikiwa au tumeshindwa. Hawa jamaa wanafanikiwa kwa sababu ya kupenda kujilinganisha na wanasiasa wenzao. Mimi nafurahia mbinu hiyo na tunatakiwa kuwatia moyo ili wasonge mbele walikomboe taifa kutoka kwenye ufisadi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom