PICHA: Athari za mvua jijini Dar es Salaam

Kuna wakati aliekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mzee Makamba aliwakemea watu wanojenga kwenye mabonde,namnukuu "hivi nyie watu mnaopenda kujenga kwenye mabonde ya mito mmekuwa vyura?" Tatizo hapa sio CCM, tatizo ni watanzania tumekuwa wabishi, hatuwasikilizi viongozi wetu mpaka maafa yatokee ndo tunaanza kuliaumu serekali! Walishaambiwa siku nyingi hawa lakini wamekuwa viziwi na sasa wanavuna walichokipanda. Ukweli ndo huo na unauma.

who sell those viwanja ni wenyekiti wa vijiji who know the historical background ya maeneo kama si serikali angalia hii kitu kwa upana usiangalie jangwa tu angalia gongo la mboto, mbezi, kimara and ubungo where are the city planners in kimara ,where are the city planner in mbezi
 
Wapangaji wangu hawa toka BANGLADESH kwao mafuriko poa tu......

mafuriko.jpg
 
Wewe ni Mbwa, samahani ila ni kwa sababu huwezi kufikiri kama binadamu wa kawaida ndo maana nimefikia kuhukumu hivyo.
Bahati mbaya kwako ni kwamba , kwa kutojitambua umekuwa mbwa koko toka kuzaliwa, hata kwenye helikopta huruhusiwi kupanda.
 
Nyumba nyingi zimejengwa kwenye mabonde na kwenye mikondo ya maji. Kuna nyingine zimejengwa kwenye "swamps". Pale msasani karibu na nyumba ya Mwl Nyerere kulikuwa ni "swamps" enzi hizo na watu walikuwa wanavuna chumvi. Sasa hivi nyumba zimejaa hivyo mvua kubwa ikija lazima pajae maji.
 
ndani+clip.jpg

Hapa ni sehemu moja wapo ya nyumba zilizo mabondeni ambazo zimezingirwa na pengine kuzama majini kama inavyoonekana hali ambayo hairuhusu hata mtu kuingia au kupita eneo hilo ila kwa mtumwi au mashua.

Binafsi nashindwa kupata picha nani alaumiwe kwa hili, wananchi wenyewe walioamua kujenga mabondeni huku jiji au mipango miji kukosa mipango ya uwazi na sheria za uwazi hali kadhalika usimamizi makini kwa wakazi ambao wanataka kujenga maeneo hayo. Leo kuwapigia kelele ni sawa maana wamechelewa na wengine nguvu zao zote walizimalizia hapo.

Sijambo geni kujenga mabondeni au kando ya mito, nimeshuhudia mafuriko makubwa ambayo yamezikumba nchi zilizoendelea ujuavyo huko majuu ujenzi aina hiyo ndio zao, wanachojali huko madaraja ya kuvukia mito lakini si nyumba za makazi ya watu na majengo ya makampuni. Baada ya mafuriko kulikumba jiji mojawapo kando ya mto mmoja ulio tawi la mto Mississippi, mwaka mmoja baadaye zimeshamiri nyumba nyingi maeneo yaliyokubwa na mafuriko kana kwamba hawakujifunza kitu.

Bora serikali iwaache na yawapatayo shauri yao, maana hata bina ina mipaka yake kwa maafa kama hayo bima hakuna kwa vile mwenye kujenga amejitakia mwenyewe na kama aliyenunua nyumba aliamua kwa kujua na kutaka.

 
Mzigo huu ni wa serikali. Ulishawahi kujiuliza hao town planners wanafanya kazi gani hasa? Kila mahali jiji lina unplanned settlements. Na bado zinaendelea huko kibamba watu wanauziana hatua kumi kwa kumi na tano utadhani enzi za ujima. Na pale wanazuoni wetu waliosomea kupanga miji wanpoona haja wanahamisha watu na kuwalipa fidia kusudi watengeneze 'satelite city'. Umeshawahi kujiuliza kwa nini sateliye city isianzishwe kwenye machka ya kibaha huko tukapunguza msongamano?

serikali imefanya mipango kiasi gani kutengeneza drainage system kusudi maji yapate pa kupita? Umeshaona barabara yetu mpya na pendwa ya morogoro ambayo strabag wanaijenga kimiujiza (manake hawaonekani sijui wanajenga saa ngapi!), jinsi inavyotuama maji? Soon mafuriko yanahamia barabarani, kama wewe unakaa kilimani na unahisi hayakuhusu ngoja siku uchukuliwe na maji ukiwa brabarani ndio utaelewa pa kuto lawama.
 
Msimu huu wanahama mvua ikiisha wanarudi lkn hawa watu walishaambiwa sio eneo la kuishi hapo ila wanataka kupambana tu.
 
mzigo huu ni wa serikali. Ulishawahi kujiuliza hao town planners wanafanya kazi gani hasa? Kila mahali jiji lina unplanned settlements. Na bado zinaendelea huko kibamba watu wanauziana hatua kumi kwa kumi na tano utadhani enzi za ujima. Na pale wanazuoni wetu waliosomea kupanga miji wanpoona haja wanahamisha watu na kuwalipa fidia kusudi watengeneze 'satelite city'. Umeshawahi kujiuliza kwa nini sateliye city isianzishwe kwenye machka ya kibaha huko tukapunguza msongamano?

Serikali imefanya mipango kiasi gani kutengeneza drainage system kusudi maji yapate pa kupita? Umeshaona barabara yetu mpya na pendwa ya morogoro ambayo strabag wanaijenga kimiujiza (manake hawaonekani sijui wanajenga saa ngapi!), jinsi inavyotuama maji? Soon mafuriko yanahamia barabarani, kama wewe unakaa kilimani na unahisi hayakuhusu ngoja siku uchukuliwe na maji ukiwa brabarani ndio utaelewa pa kuto lawama.


well said!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom