Photo of the Day - Dar es Salaam 1985

Jamani yaani nikiona hivi nakumbuka enzi hizo nilikuwa kijana mbichi ndiyo nimeanza tu "kutoa mbegu" tu. Duuu ama kweli humu JF tunakumbushana mbali sana. Natamani nirudie ujana wangu.

Mmh! imekula kwako hiyo mkuu....sasa ni zamu yetu dot com generation
 
Ukienda mjini jumapili kila mtu wa tatu unayemuona unamjua, mnasoma wote, mmecheza mpira, mmeenda kusali pamoja etc.

Enzi hiyo kabla machinga hajaingia mjini, ukikutwa unazubaa zubaa mjini unapigwa "uzururaji" watu wanakutia kwenye lori wanakupeleka Gezaulole au Kibugumo.

Hahahahahah lol! Weye sasa inabidi ugombee ubunge maana unajulikana sana jijini :) :) :)
 
Teh teh teh, ndo nilizaliwa kipindi hicho, macho yanafunguka naona ustaarabu, miguu na akili inakomaa nakaexperience unyama ama ushenzi. Nakumbuka nakua mitaa ya shule ya uhuru, mama alikuwa mwalimu, kukiwa na ugeni wa kitaifa unapita Uhuru road, anamtuma mwanafunzi mmoja anakuja kutuchukua nyumbani kutupeleka kuwapungia mkono Raisi na Mgeni wake.
Roads zilikuwa zinajaa kuwapungia viongozi! Leo ni kuwazonea na kiwapiga mawe.
Nakumbuka ujio wa papa tulikaa road more than 3 hrs huku tunasikilizia kwenye radio Tanzania!
 
Ukienda mjini jumapili kila mtu wa tatu unayemuona unamjua, mnasoma wote, mmecheza mpira, mmeenda kusali pamoja etc.

Enzi hiyo kabla machinga hajaingia mjini, ukikutwa unazubaa zubaa mjini unapigwa "uzururaji" watu wanakutia kwenye lori wanakupeleka Gezaulole au Kibugumo.

Hii nimeopenda! Nakumbuka ilipita kampeni ya NGUVU KAZI mwaka 1983 enzi hizo Sokoine Waziri Mkuu, walisombwa watu wasio na kazi maalum wakapakiwa kwenye treni kurudishwa mikoani kwao.
 
3091805970_81fd31281e_b.jpg
Nani anakumbuka haya mabasi?
 
Jama mnakumbuka lile basi la kamata lililopinduka pale mtaa wa mgombani asubuhi? Lilikua limebeba wanafunzi wengi wa forodhani. Dreva alilipindua maksudi kwasababu ya kutukanwa na wanafunzi.
 
Teh teh teh, ndo nilizaliwa kipindi hicho, macho yanafunguka naona ustaarabu, miguu na akili inakomaa nakaexperience unyama ama ushenzi. Nakumbuka nakua mitaa ya shule ya uhuru, mama alikuwa mwalimu, kukiwa na ugeni wa kitaifa unapita Uhuru road, anamtuma mwanafunzi mmoja anakuja kutuchukua nyumbani kutupeleka kuwapungia mkono Raisi na Mgeni wake.
Roads zilikuwa zinajaa kuwapungia viongozi! Leo ni kuwazonea na kiwapiga mawe.
Nakumbuka ujio wa papa tulikaa road more than 3 hrs huku tunasikilizia kwenye radio Tanzania!

hapo kwenye bold umnikumbusha mbali sana mkuu,................. nakumbuka niliwahi kusimama sokine drive masaa kibao kuwasubiri mwinyi na gen. babangida wa nigeria niwapungie mikono!!.............. ila siku hizi, ukisimama barabarani na hao waheshimiwa wanapita huku jiwe liko karibu unaweza kupata kesi ya bure aisee.............. siku hisi magadhabu dhidi ya hawa wakoloni weusi yako nje nje...................... kweli mambo yamebadilika sana.............
 
View attachment 34147

Mitaa ya wapi hii, wadau mnakumbuka mlikuwa wa wapi na mnafanya nini mwaka huu wa 1985?

Mwaka huo mie ndio naoa na kuchukua kimwari kipyaaa!!
Picha imepigwa kituo cha mafuta Agip, na hilo jengo kulia lilikuwa Benki Kuu(baada ya benki kuu ya awali kuungua)
Tanzama saa hizo za magharibi, hakuna watu kabisa Dr es salaam, maana enzi hizo niu mashirika ya umma tu na kila shirika lina mabasi yake.
Mimi nilikuwa nafanya kazi shiika fulani la umma ghorofa ya tano hapo IPS , hilo jengo refu katika background.
 
...
Mimi nilikuwa nafanya kazi shiika fulani la umma ghorofa ya tano hapo IPS , hilo jengo refu katika background.
Unakumbuka kijiwe cha Coffee Bar mtaa wa Samora? Halafu hapo nyuma ya IPS kwa chini kulikuwa na mgahawa unaweza kupata supu ya kumalizia hangover. Mishe mishe za ulanguzi zilikuwa zimetapakaa na minoti tulikuwa tunaiweka kwenye soksi!
 
Hakukuwa na kitu kama hicho mzee, nakumbuka tulikuwa tunakaa kunduchi magari ya huko yalikuwa ni hizi COASTER, kama utakumbuka vizuri kwa wale waliokuwa wapenzi wa DISCO hizi ndo zilitumika sana pamoja na magari madogo kama pick up n.k,

Tena hizo Coaster nazikumbuka kwa majina kama,
  1. Apolo Eleven
  2. Scaba Scuba
  3. Nyanza Express
  4. Akachube One
  5. The Storm
 
Unakumbuka kijiwe cha Coffee Bar mtaa wa Samora? Halafu hapo nyuma ya IPS kwa chini kulikuwa na mgahawa unaweza kupata supu ya kumalizia hangover. Mishe mishe za ulanguzi zilikuwa zimetapakaa na minoti tulikuwa tunaiweka kwenye soksi!

Ha ha haa!
Mzee mwenzangu
Ile sehemu ya supu ya hangover ilikuwa inaitwa Georges Grill, nafikiri bado ipo.
Siku hizo ukipatikana na dola, wewe ni lupango na hakuna dhamana-mhujumu uchumi.Dola zote ilikuwa mali ya serikali.
Lakini miaka hiyo poa, nikitoka kazini hapo IPS jumamosi aidha unaishia Embassy Hotel au New Africa open restaurant. Jioni hapo hapo New Africa ngoma za maghorofani-MK Beats.
 
Hapo ni maeneo ya posta Mpya na hicho kibanda cheupe palikuwa ni carwash kwenye hiyo petrol station (Agip) ilikuwa mkabala na AISCO na kwa upande wa pili kuna YWCA ambayo inapakana na lile kanisa ambalo lilikuwa mkabala na Mawenzi Hotel, Jengo la Nyuma ya hicho kibanda Cheupe ilikuwa ni benki kuu ya Muda baada ya ile ya dhamani kuungua, nadhani ni jengo la iliyokuwa BENKI YA USHIRIKA NA MAENDELEO VIJIJINI, hilo jengo refu la nyuma ni IPS pale kwenye mzunguko wa sanamu la Askari, ambalo linapakana na Phillips house (bank ya posta) na idara ya Maelezo iliyokuwa inapakana na Empire cinema

Dar ilikuwa murua na iliyostaarabika, namkumbuka sana yule Mama pekee aliyekuwa anaendesha hayo mabasi UDA, utaratibu ulikuwa mzuri sana na kulikuwa na urataibu wa kuknunua kitabu kizima cha tiketi cha mwezi mzima na ukiwa nacho wewe upangi foleni UDA ikisimama wewe unapandia mlango wa mbele
 
Ha ha haa!Mzee mwenzanguIle sehemu ya supu ya hangover ilikuwa inaitwa Georges Grill, nafikiri bado ipo.Siku hizo ukipatikana na dola, wewe ni lupango na hakuna dhamana-mhujumu uchumi.Dola zote ilikuwa mali ya serikali.Lakini miaka hiyo poa, nikitoka kazini hapo IPS jumamosi aidha unaishia Embassy Hotel au New Africa open restaurant. Jioni hapo hapo New Africa ngoma za maghorofani-MK Beats.
Dah, umenikumbusha mbalii!
 
Back
Top Bottom