Photo of the Day - Dar es Salaam 1985

UDA.jpg
Kwa jinsi iyo taa ya duara hapo juu... nadhani hapo ni TAZARA!!!
 
bila shaka mitaa ya posta mpya hiyo.

sijui picha ya mwezi gani, mwenzeni nilikuwa kadogooooooo ka kupakatwa, kama nilikuwa nimeishatinga duniani at all!! dah, nimekuwa mkubwa na mimi siku hizi eeh!

Glory to God
Pole sana Miss Judith wewe ulikuwa kadogo dogo mimi wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 21 Young Man kumbe humu ndani tuna watoto wetu kwenye hii Jamii Forums?
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Population ya Dar ilikuwa ndogo sana wakati huo. Mie nilikuwa Mlimani, tulikuwa tukiletwa mjini na ma-bus ya chuo na kurudishwa saa 6 ili kuwahi msosi. Ukichelewa ma-bus la chuo unapanda UDA na baada ya kama dk 10 umeshafika Havard Cafeteria kuwahi 'NGUIN'. Hakukuwa na foleni ati.
Mimi nilikuwa mtu wa ile cafeteria ya "shimoni" tulikokuwa tunapigania mlo na akina Mwakyembe (1982)! Hiyo picha ya kwanza kama HOMOSAPIEN alivyosema, ni mitaa ya Posta mpya.
 
1985 ndio zamani saana ? duh! ngoja sisi wenye vyeti vya kuzaliwa vilivyoandikwa Tanganyika tunyamaze tu,hivi na sisi kweli ni watanzania ? maana nchi niliyozaliwa haipo tena.
 
Hiyo ni what used to be Agip gas station kwa kulia (hiyo structure nyeupe yenye maandishi ni car wash). UDA limesimama kwenye kituo cha basi, na kushoto ni Posta Mpya.
 
hahahaa binti! kumbe kuna watoto wa miaka ya 80 humu, aisee!!

hahahaaa, kaka, hii sasa ni miaka ya 2010+ so sie wa miaka ya 80 saa hizi si watoto tena, ila si wakubwa kiviiileeee! mpaka hapa, tumeishabanana sana tu na wakubwa humu duniani, teh teh...
 
Pole sana Miss Judith wewe ulikuwa kadogo dogo mimi wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 21 Young Man kumbe humu ndani tuna watoto wetu kwenye hii Jamii Forums?

hahaaaaa, kaka!!!

tafadhari Mzizimkavu usinivunje mbavu, pole ya nini tena badala ya hongera kwa kuwa na mimi nimekuwa mkubwa siku hizi!

yeah, unazungumzia watoto? kuna watu humu sie ni wajukuu kabisa, lolz! na tunakwenda nao sambamba kama magreat thinkers! thats why i always give thanks to my Lord!

Glory to God!
 
i miss you miss Judith ..........:A S-rose: natamani uwe wangu.............................................
 
Mzee hiyo ni Tandamti basi la kwenda Msasani. Mwisho saa 3, Ulikosa hilo unapiga mguu. Linaendeshwa na mzee mmoja ana matusi sio kawaida akifika Namanga anasema shhhhh....nz. Hii kona inanitia ny.....e
 
Mitaa ya posta mpya hiyo kabla hajajenga ile 'sheli' na UDA ya shs 5/= na jengo la IPS kwa mbali.Ilikuwa raha.
Halafu hapo IPS chini kulikuwa na Goethe Institute. Kweli yaliyopita si ndwele...!
 
Kilichonikumbusha mbali ni hilo UDA. Wakati huo tuko wadogo nilikuwa naadmire sana kazi ya kondakta kwa ajili ya kile kimashine chake. Mdogo wangu nyumbani naye alikuwa anaingiza vipande vya karatasi ktk tundu la funguo la kitasa cha mlango halafu mkipita anabonyeza ile handle ikiachia anatoa kikaratasi (tiketi) Ole wako usipokee, analia! Tulikuwa tunatishiwa eti usipolipa nauli unapelekwa kwenye yard ya UDA kuosha ma-UDA matano.

Halafu tulikuwa tunaenda kariakoo sokoni na UDA, tukimaliza kununua vitu shimoni tunaenda mtaa wa Tandamti pale kulikuwa na kituo. Inapangwa foleni pale kwa kila mtu kuweka mzigo wake in a line. Mkifika na nyie mnaweka kapu lenu nyuma halafu mnatafuta kivuli kusubiri UDA. Likija hakuna kugombania, mnafuata ule mstari kwa ustaarabu.

Good old days...

kumbe mambo haya yanawezekana, kwa nini sio siku hiziiii
 
1985 ndio zamani saana ? duh! ngoja sisi wenye vyeti vya kuzaliwa vilivyoandikwa Tanganyika tunyamaze tu,hivi na sisi kweli ni watanzania ? maana nchi niliyozaliwa haipo tena.
ndugu yangu, usishangae sana, wengi humu ni kizazi cha dot com, kwa hiyo hiyo nyekundu, ni zamani sana...hata mei kidogo nilikuwapo .. nilikuwa primary
 
hahahaaa, kaka, hii sasa ni miaka ya 2010+ so sie wa miaka ya 80 saa hizi si watoto tena, ila si wakubwa kiviiileeee! mpaka hapa, tumeishabanana sana tu na wakubwa humu duniani, teh teh...
tena nyie wa wa miaka ya chini ya 80, ndo mpo wachache sana humu, ikipigwa sensa , utakuta ni less that 50%
 
Back
Top Bottom