Photo of the Day - Dar es Salaam 1985

tototundu

Senior Member
Jul 29, 2009
198
40
dar 1985.JPG

Mitaa ya wapi hii, wadau mnakumbuka mlikuwa wa wapi na mnafanya nini mwaka huu wa 1985?
 
bila shaka mitaa ya posta mpya hiyo.

sijui picha ya mwezi gani, mwenzeni nilikuwa kadogooooooo ka kupakatwa, kama nilikuwa nimeishatinga duniani at all!! dah, nimekuwa mkubwa na mimi siku hizi eeh!

Glory to God
 
Mitaa ya Posta mpya nikuwa kazini tena serikalini katika jengo la Lehmans building.
 
UDA linanikumbusha mbaaali, enzi hizonilikuwa naamsaidia kondacta kugonga bodina shilingi kama dereva hajasikia/kengele haifanyi kazi
 
Kilichonikumbusha mbali ni hilo UDA. Wakati huo tuko wadogo nilikuwa naadmire sana kazi ya kondakta kwa ajili ya kile kimashine chake. Mdogo wangu nyumbani naye alikuwa anaingiza vipande vya karatasi ktk tundu la funguo la kitasa cha mlango halafu mkipita anabonyeza ile handle ikiachia anatoa kikaratasi (tiketi) Ole wako usipokee, analia! Tulikuwa tunatishiwa eti usipolipa nauli unapelekwa kwenye yard ya UDA kuosha ma-UDA matano.

Halafu tulikuwa tunaenda kariakoo sokoni na UDA, tukimaliza kununua vitu shimoni tunaenda mtaa wa Tandamti pale kulikuwa na kituo. Inapangwa foleni pale kwa kila mtu kuweka mzigo wake in a line. Mkifika na nyie mnaweka kapu lenu nyuma halafu mnatafuta kivuli kusubiri UDA. Likija hakuna kugombania, mnafuata ule mstari kwa ustaarabu.

Good old days...
 
Population ya Dar ilikuwa ndogo sana wakati huo. Mie nilikuwa Mlimani, tulikuwa tukiletwa mjini na ma-bus ya chuo na kurudishwa saa 6 ili kuwahi msosi. Ukichelewa ma-bus la chuo unapanda UDA na baada ya kama dk 10 umeshafika Havard Cafeteria kuwahi 'NGUIN'. Hakukuwa na foleni ati.
 
Da! Hilo 'Bayankata' limenikumbusha mbali hasa! ukitaka kwenda Gongolamboto lazima unapitia airport ya zamani ndio mwisho wa UDA toka kariakoo kisha unapanda lingine linaanzia pale hadi gongolamboto!
Kuna makonda eti na mainspekta! Jamaa wanapandia tu popote alafu wanauliza tiketi randomli!
 
UDA, nakumbuka ndio ulikuwa usafiri wa jumapili mchana, wakati ule jumapili baada ya saa nane magari yalikuwa hayaruhusiwi kutembea; kwa anayekumbuka, ilikuwa ni suala la ku-save mafuta tu au ilikuwa na siesta ya lazima?
 
umenikumbusha mbaliiii, kile kimashine cha konda pale mlango wa nyuma kilikuwa kinanikosha sana, hakuna kusemeshana sana, "kond: Wapi? Abr: Manzese msufini"
 
Mtaa wa Azikiwe... Wakati huo hailkuwa Dual Carriage naona Posta Mpya,Car & General,Embassy Hotel,Jengo la IPS,Benki ya CRDB. Azikiwe,Agip(Oryx),New Africa Hotel wing mpya ikiwa inajengwa na Crane juu na kali zaidi UDA. Enzi hizo kulikuwa hamna Billboards... Old Good dayz...
 
bila shaka mitaa ya posta mpya hiyo.

sijui picha ya mwezi gani, mwenzeni nilikuwa kadogooooooo ka kupakatwa, kama nilikuwa nimeishatinga duniani at all!! dah, nimekuwa mkubwa na mimi siku hizi eeh!

Glory to God
hahahaa binti! kumbe kuna watoto wa miaka ya 80 humu, aisee!!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom