Phiri apanga mashambulizi Mazembe

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KOCHA wa Simba Patrick Phiri amesema kikosi chake kitatumia mfumo wa kushambulia kwa kasi lakini kwa tahadhari mno ili kuepuka wapinzani wao TP Mazembe wasipate bao katika pambano lao la Jumapili.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Phiri alisema kuwa watalazimika kutumia mfumo huo ili waweze kupata mabao mengi na ikiwezekana mapema zaidi.

"Tunahitaji kushinda mabao zaidi ya mawili hivyo ni lazima tushambulie sana lakini tukicheza kwa tahadhari wenzetu wasipate bao, kwa ujumla itabidi tucheze kitimu hasa ukizingatia pale mbele nao wako vizuri.

"Si mechi rahisi kama wengi wanavyofikiria muhimu ni kujipanga na kuhakikisha hatupotezi nafasi kama ilivyotokea katika mchezo wa awali," alisema Phiri.

Aidha aliwataka viongozi, wachezaji na wanachama wa klabu hiyo kuongeza umoja na mshikamano na kuachana na mambo ambayo yanaweza kuwadhoofisha na hatimaye wakashindwa kutimiza malengo yao.

"Nasisitiza suala la umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi, mashabiki na wanachama hasa kipindi hiki tunachokabiliwa na mchezo mgumu mambo ambayo hayaweza kutudhoofisha tuachane nayo badala yake tuelekeze akili zetu Jumapili," alisema Phiri.

Katika hatua nyingine daktari wa Simba, Cosmas Kapinga alisema kuwa hali za wachezaji Abdulhalim Humoud, Hilary Echesa na Uhuru Selemani ambao wamekuwa majeruhi kwa kipindi mrefu zinaendelea vizuri.

Hata hivyo, Kapinga alisema beki Joseph Owino ambaye ni majeruhi wa muda mrefu atalamizika kwenda kupata matibabu zaidi nchini India kutokana na tatizo kuonekana kuwakubwa.

"Humoud anaendelea vizuri na matibabu ya goti wakati Echessa tulimpeleka Hospitali ya Agha Khan kwa ajili ya vipimo zaidi na tatizo lake limeonekana linaweza kutibika hapa nchini lakini Owino tatizo lake kubwa na linafanana na lile la Uhuru hivyo mipango ikikamilika atakwenda kutibiwa India,"alisema Kapinga.
 
Naamini kabisa kama wachezaji watajituma basi lazima mnyama mmtafune mtu..uwezekano wa history kujirudia upo, kikubwa ni mshkamano ..waling'oka waarabu hata wakongo watang'oka tu.
 
hahaaaaaa tuombe shetani asiingilie kati
Naamini kabisa kama wachezaji watajituma basi lazima mnyama mmtafune mtu..uwezekano wa history kujirudia upo, kikubwa ni mshkamano ..waling'oka waarabu hata wakongo watang'oka tu.
 
Hii michezo ya kwenye media ndo inatupeleka kaburini kabisa...kandanda ni uwanjani bwana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom