ufahamishwe wewe kama nani?
Justified how,naomba udadavuzi mkuu.Samahani lakini.Maana tumeshazoea kusikia mtu amefikisha umri wa kustaafu kwa lazima lakini utasikia amekuwa akifanya kazi kwa mkataba au alikuwa kwenye mkataba miaka 2 au 3 n.k wakati vijana na watu wa rika la kati wapo.
ufahamishwe wewe kama nani?
inaonekana ni kisiki cha mpingo.Wakati wa sakata la Jairo tuliambiwa kuwa Luhanjo angestaafu tarehe 09/ 12/ 11 baada ya kufanikisha sherehe za miaka 50 ya uhuru. Juzi juzi nimemsikia akitaja majina ya mabalozi wapya walioteuliwa kuchukua kazi kwenye nchi mbalimbali. Leo hii bado siku 6 tumalize mwaka. Je huyu Luhanjo ajira yake haina kikomo?
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) hustaafu kama viongozi wengine, mfano makatibu na manaibu katibu wakuu wa Wizara. KMK hayuko katika kundi la viongozi wa kisiasa ambao hawana suala la kustaafu kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa nk.
Kweli muda wake wa kustaafu ulifika, lakini akaongezewa muda. Hilo la kuongezewa muda liko Serikalini kama wanaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.