Philemon Luhanjo: Ni nini kazi yake? Mbona hastaafu?

Kama alistaafu nakuongezewa mkataba alifuata ule utaratibu wa wengi wakuenda likizo la kustaafu halafu baada ya hapo anapewa mkataba? ama yeye ni exceptional kwenye sheria zetu hizi?
 
Hata mimi nashangaa kwani jana nimeona yuko pale kilimanjaro kempinsky akiwaaga makatibu wakuu wengine sasa nikajiuliza hivi yeye ni vipi..

Kikwete anadhambi nyingi sana na huyu jamaa ndiye anayemsaidia kuficha huo uchafu.. Kama hamjui hicho cheo chake hakipo kwenye vyeo vya serikali... Na pia jamaa ana nguvu sasa kwenye mawaziri...

Wakati wa kikao baraza la mawaziri, rais ndiye mwenyekiti na yeye ndiye katibu wa baraza la mawaziri.

Ila mwisho wa siku atastahafu na pia tutamfunga kwa sababu ya utumbo wa serikali hii mbovu..
 
Wakati wa sakata la Jairo tuliambiwa kuwa Luhanjo angestaafu tarehe 09/ 12/ 11 baada ya kufanikisha sherehe za miaka 50 ya uhuru. Juzi juzi nimemsikia akitaja majina ya mabalozi wapya walioteuliwa kuchukua kazi kwenye nchi mbalimbali. Leo hii bado siku 6 tumalize mwaka. Je huyu Luhanjo ajira yake haina kikomo?
 
Mnalalamikia ajira wakati mababu zenu kibao wapo makazini kwa mikataba.Ni hofu ya kustaafuna sio utaalamu ingekuwa utaalamu vijana wapo wengi, maana mtaani stamina au la inakula kwako!
 
Wakati wa sakata la Jairo tuliambiwa kuwa Luhanjo angestaafu tarehe 09/ 12/ 11 baada ya kufanikisha sherehe za miaka 50 ya uhuru. Juzi juzi nimemsikia akitaja majina ya mabalozi wapya walioteuliwa kuchukua kazi kwenye nchi mbalimbali. Leo hii bado siku 6 tumalize mwaka. Je huyu Luhanjo ajira yake haina kikomo?
na nimemuona kwenye picha akisimamia uapishwaji wa hao mabalozi juzi Ikulu. hata kama wamemwongezea muda si watanzania tunapaswa kufahamishwa?
 
Nadhani mtoa mada swali lake lipo justified.

Justified how,naomba udadavuzi mkuu.Samahani lakini.Maana tumeshazoea kusikia mtu amefikisha umri wa kustaafu kwa lazima lakini utasikia amekuwa akifanya kazi kwa mkataba au alikuwa kwenye mkataba miaka 2 au 3 n.k wakati vijana na watu wa rika la kati wapo.
 
Ndiyo fringe benefits za kusikilizana na mwenye nchi jamani!...kama kuna missions uncomplited mnataka walete kimeo mpya aje azitibue?
 
Kama kuna tija kutoka kwa mtumishi aliyefikisha umri au kama taaluma yake ni nadra kuipata katika soko la ajira kama vile madaktari wa binadamu then kuna kila sababu kwa mwajiri ku renew mkataba. Kwa upande wa huyu Philemon nafikiri ameweka historia yavkuwa KMK kiongozi wa kwanza kulalamikiwa sana na jamii, wanasiasa pamoja na wana harakati. Vilevile kitaaluma ni mtu wa Public Administration au HR kwa hiyo hainiingii akilini kwa nini huyu kiumbe bado yupo pale pamoja na kudhalilisha utumishi wa juu katika taifa
 
Kwani si kina yale mapendekezo ya kamati maalum iliyoundwa kuchunguza sakata la Jairo si ilionyesha kuwa naye ana hatia! Sasa hiyo siyo sababu tosha ya kum-sideline?
 
Kwani si kina yale mapendekezo ya kamati maalum iliyoundwa kuchunguza sakata la Jairo si ilionyesha kuwa naye ana hatia! Sasa hiyo siyo sababu tosha ya kum-sideline?

Mzee wenye nji hii hawakawii kukujibu kuwa una wivu wa kike! Kwao wala hiyo report bado haijawafikia, ni kama haipo, bado anakabidhi kwa miaka mingine mitatu, zile ni ofisi Zenye majukumu mazito, huwezi kuacha kienyeji tu, eti kwa kuwa muda umefika wa kustaafu kwa mujibu wa sheria,sawa?
 
Back
Top Bottom