[Petition]: Tatizo la Umeme (Dr. Wilbroad Slaa amesaini)

BongoTz

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
272
3
Nianze kwa kuwashukuru watanzania wote (ndani na nje ya nchi) ambao tayari mmeitikia wito huu na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa kusaini petition. Sambamba na hilo, napenda pia kuwashukuru wale wote mliokubali kutoa muda wenu kuwapigia simu/andikia email wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaelezea kwa kina umuhimu wa mradi huu (shukrani za pekee kwa Dr. Wilbroad Slaa, mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA 2010, aliyeona umuhimu wa suala hili na kuamua kusaini petition).

Natambua suala hili limechukua muda mrefu sana, but at last, juhudi zetu zinakaribia kuzaa matunda. Hata Kikwete mwenyewe anaonekana sasa kuwa "onboard"--maana ameahidi mwenyewe kuwa--mradi huu utatekelezwa ndani ya kipindi cha mhura wake wa mwisho (2010-2015).

By Rodgers Luhwago
21st November 2010
President Jakaya Kikwete has said the government would start implementing the multibillion power Stigler's Gorge project on Rufiji River in this second term of his government.
Delivering a maiden speech when inaugurating the 10th Parliament in Dodoma on Thursday President Kikwete said the Stigler's Gorge Power Project would generate 2100 MW upon completion.
The President was outlining strategies by his government of alleviating shortage of power in the country. "I have been informed that this project will take nine years before the power is switched on. I hope to start implementing the project within the period of five years," he promised.
The project is located at a narrow gorge on the Rufiji River, some 230 kilomitres upstream from the Indian Ocean and it is some 374kilometres away from Dar es Salaam by road. The distance will be 165kilometres from Chalinze after construction.
This project was studied in 1978-80 by M/s Norplan / Hafslund who were commissioned by Rufiji Basin Development Authority (RUBADA). The capital cost is estimated at about US$1,200 million at 1985 prices.
According to the President, in the past five years the government succeeded to add 145 MW onto the national grid from natural gas. He said that plans to add another 100 MW from natural gas are complete. He said in the next five years the government expects to generate 640 MW from natural gas, hydro and coal.
He said the government would speed up the exercise of connecting more customers to power, adding that the target is to connect 30 percent of Tanzanians to electricity from the current 14 percent.
On education, Kikwete said in the past five years the government succeeded to expand education opportunities for children, adding that the efforts would be carried out during his second term. Education would continue to get the lion's share of the national budget every year, he said.
In the next five years the government would continue improving teachers' welfare and the working environment, including building teachers' houses across the country.
He also promised to continue building vocational training centers in each district. As for higher education, the president said he would implement a higher education programme that, among other things, aims at improving its quality to meet the standards needed by the local labour market, within East Africa region as well as internationally.
Construction of University of Dodoma would be finalised in this second term of President Kikwete's government, to be followed by the construction of Mwalimu Nyerere University of Agriculture at Butiama.
SOURCE: GUARDIAN ON SUNDAY
Please endeleeni kusaini petition/sambaza ujumbe kwa wabongo wengine ili tuzidi kuibana serikali itekeleze ahadi hii ndani ya kipindi cha miaka mitano, kama Rais alivyoahidi mwenyewe.

Petition inapatikana hapa: TATIZO LA UMEME: TUPATIENI 'STIEGLERS GORGE' Petition

P.S. Kama unawafahamu watu wengine ambao wangependa kusaini hii petition lakini hawana access ya Internet; basi naomba tuwasiliane ili nikutumie petition zilizochapwa (print version).

Thank you!
 
Thanks, VoiveOfReason! Petition ya katiba mpya ipo, Nitai-post in the next few days.
Thanks tuko pamoja, pia post hard copy ili watu watoe photocopies na wawape jamaa zao wengine wasaini cha muhimu ni kuwapa address ya wapi wasikusanye wakishazisaini I am sure by february we might have more than 8 million signatures
 
Thanks tuko pamoja, pia post hard copy ili watu watoe photocopies na wawape jamaa zao wengine wasaini cha muhimu ni kuwapa address ya wapi wasikusanye wakishazisaini I am sure by february we might have more than 8 million signatures
Wazo zuri. Ok, nita post hard copy.
 
Ukiona hivyo ujue watu wanaitaka haraka. Asante kwa kuahidi kwamba inakuja soon. Tunaisubiri kwa hamu.
 
Watu wengine ni waajabu sana, Rais kisha amuwa na kishatangaza umeme huu wa Rufiji utapatina na utaanza kutekelzwa within his tenure, sasa petition ya kushinikiza nini?
 
Watu wengine ni waajabu sana, Rais kisha amuwa na kishatangaza umeme huu wa Rufiji utapatina na utaanza kutekelzwa within his tenure, sasa petition ya kushinikiza nini?
Kwasababu mwaka 2005 aliahidi the same thing lakini hakutekeleza. That's why we diceded to start a petition this time so we can push him to keep his promise. Enough is enough. Tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo.
 
TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KUSINI KUHUSU MGOGORO WA NISHATI YA UMEME NA KUSUDIO LA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI

JUMAPILI, DISEMBA05, 2010
Dar es Salaam.


UTANGULIZI
Karibuni wanahabari. Leo nimeamua kuwaomba kama wanahabari na watanzania wazalendo tujadili hatma ya Taifa letu ambalo utaratibu wa kuingizwa gizani na mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya watanzania.

Kwanza nipende kuwakumbusha tu kwamba tukiwa na nusu karne tangu tupate uhuru ni asilimia 14 tu ya watanzania ambao wanapata huduma ya umeme, kiwango ambacho ni sawa kabisa na takwimu za huduma hii kabla ya Uhuru takribani nusu karne iliyopita.Kwa vijijini kama jimboni kwangu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla hali ni mbaya zaidi kwani kwa takwimu za sasa, ni asilimia 2 tu za watanzania vijijini wanaopata huduma ya umeme.

Lakini pia, tukumbuke kwamba bila nishati ya umeme ya uhakika hatuwezi kutekeleza MKUKUTA, hatuwezi kufikia MALENGO YA MILENIA, hatuwezi kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ama ya uchumi wala ya huduma. Takwimu mbalimbali na hata zile za Benki ya dunia zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya uchumi duniani inategema nishati ya umeme.

Hapa Tanzania, kwa kasi ya ukuaji wa uchumi ya sasa ya takribani asilimia 7 kwa mwaka, uzalishaji wa Umeme unapaswa kukua kwa zaidi ya asilimia 15 kwa mwaka. Mahitaji ya Umeme nchini ni zaidi ya 1500 MW kwa mwaka, uwezo wetu ni kuzalisha 1034 MW lakini kiasi kinacho zalishwa ni 690MW tu kwa sasa kutokana na uchakavu wa mitambo na kupotea kwa umeme mwingi kwenye njia za kusafirisha. Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi na inahitaji mikakati ya lazima kushughulikia.

Nikatika misingi hii watanzania tunawajibika kuwa wakali inapotokeo watu tuliowapa madaraka kutuongoza wanashindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu masuala nyeti kama umeme.

Msingi mkubwa wa tatizo la umeme Tanzania ni serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hili na badala yake imebaki inasimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo kwa miaka sasa, tangu IPTL mwaka 1994 hadi Agreko, Songas, Richmond, Dowans imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa. Asilimia 86 ya mapato ya TANESCO yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote. Hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba wake. TANESCO wanailipa kampuni ya Songas takribani shilingi 266m kila siku kwa kununua 186MW za umeme. Mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa TANESCO wanailipa kampuni hii shilingi 300m kila siku! Itakumbukwa kuwa TANESCO walikuwa wanapaswa kuilipa kampuni ya RICHMOND/DOWANS shilingi 152m kila siku kwa kununua 100MW za umeme.

Tangu mwaka 2006, serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo hili la mgawo wa umeme. Viongozi wakuu wa serikali na hasa Waziri wa Nishati na Madini mara kadhaa wamekuwa akipotosha watanzania kuwa serikali inashughulikia kwamba mgawo wa umeme utakuwa historia lakini siku hadi siku sekta ya umeme imevuka upeo wa viongozi hawa kiasi cha kauli zao kupoteza imani kwa watanzania.

Leo tukiwa tunazungumza mgawo wa umeme, pembeni tunakabiliwa na deni la zaidi ya billioni 185 ambazo kwa uamuzi wa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa (ICC) tunapaswa kuilipa kampuni ya Dowans, ambayo mpaka sasa serikali imekosa ujasiri kusema mmiliki wake ni nani lakini imekiri kushindwa kesi mahakama ya kimataifa.

Kwamba serikali isiyomjua wala kutambua uhalali wa mmiliki wa kampuni ya Dowans iko tayari kukiri kwa watanzania kuwa kampuni hiyo isiyojulikana mmiliki wake imeshinda kesi? Ni dhahiri kuwa Mahakama ya kimataifa yenye kuheshimika duniani kote haiwezi kukaa na kushiriki katika shauri ambalo Kampuni inayoshitaki haijulikani . Suala la umiliki wa Kampuni ya Dowans limekuwa likichezewa tu kwa maslahi ya makambi ya kisiasa ndani ya chama tawala.

Itakumbukwa pia kuwa mkataba ule ulikuwa ni wa miezi 24 na wenye thamani ya shs 172bn. Lakini kwa ukosefu wa uongozi na siasa duni ndani ya mfumo wa utawala wetu tunalipia shs 185bn tena bila kupata umeme. Billioni 185 zingetosha kuongeza 200MW za Umeme kwenye grid ya Taifa lakini sasa zinakwenda kulipwa kizembe. Huu ni unyama usio vumilika kwa watanzania maskini. Na ni unyama zaidii kwa watanzania masikini wa vijijini ambao asilimia 98 hawajui radha ya umeme lakini kodi zao sasa zinakwenda kutumika kijinga kabisa! Haiwezekani.

Mwanzoni mwa mwaka 2009 kulikuwa kuna mgogoro kuhusiana na ama TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya kampuni hii iliyotushinda kesi. Kundi moja la wabunge likisema isinunuliwe kwani itakuwa ni kukiuka sheria ya manunuzi (hakuna aliyethubutu kusema ni kifungu gani cha sheria ya manunuzi) na utata kuhusu mkataba wa Dowans(Hii ndio hoja ya msingi).

Kundi lingine lilikuwa likijenga hoja ya kununuliwa kwa mitambo ile ili kuepusha mgawo na vile vile iwe ni fursa ya kufuta kesi ambayo DOWANS waliifungulia TANESCO (mitambo ile ilikuwa inunuliwe kwa thamani ya shs 70bn). Kwa uamuzi tuliouchukua kama Taifa wa kutonunua mitambo ile, tunapaswa kulipa 185bn shs, mitambo wamebaki nayo na wataiuza watakapo baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kitengo cha Biashara kuamuru tarehe 22.10.2010 kuwa zuio la TANESCO dhidi ya Dowans kubeba mitambo ile lilikuwa batili. Mbaya zaidi Mgawo bado unaendelea na kuunyonya uchumi wa Taifa letu (bleeding the economy). Kinachosumbua hapa ni kwamba inawezekanaje serikali kushindwa kesi na kampuni ambayo tulielezwa mkataba wake ni batili( hapa ndio kuna siri nzito ndani ya serikali na chama tawala na ni siri hiyo nzito inayoendelea kukamua watanzania masikini mabilioni ya fedha ambayo yangepelekwa kwenye huduma za maji, Afya na Elimu).

MADHARA YA MGAWO

  • Uzalishaji viwandani : Shirikisho la wenye Viwanda nchini mara kwa mara limekuwa likieleza namna ambavyo wanachama wake wanaathirika na mgawo wa umeme. Mifano ya viwanda vya simenti imekuwa ikitolewa ambapo mgawo wa umeme unaongeza gharama za kuzalisha Simenti kwa kiwango cha dola za marekani 10 kwa kila mfuko wa kilo 50 wa Simenti na hivyo kuongeza gharama, kupata hasara na kushindwa kulipa kodi Serikalini.
  • Gharama za uzalishaji kuongezeka: Vijana wanaojishughulisha na kunyoa nywele jijini Dar es Salaam hupoteza zaidi ya asilimia 45 ya Mapato yao kutokana na kutumia majanereta ili kupata umeme wa kutoa huduma kwa wateja wao (REPOA report on electricity access for job creation 2010).
  • Bei za bidhaa kupanda kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka. Wafanyabiashara hujaribu kusukuma kuongezeka kwa gharama kwa walaji wa kawaida na hivyo kumdidimiza mwananchi wa kawaida. Maeneo ya vijijini ambapo hutegemea umeme kusaga nafaka zao kama Mahindi na Mpunga huathirika sana unapotokea mgawo kwa kutembea umbali mrefu kusaga nafaka na kwa gharama kubwa kutokana na gharama za mafuta ya kuendeshea majenereta kuwa kubwa.
  • Kusimama kwa shughuli nyingi za huduma kama benki, hospitali, vyuo na shule, na hata vyombo vya habari katika utendaji wake.


HATUA ZA KUCHUKULIWA.

    1. Serikali ione kwamba suala la mgawo wa umeme linaathiri maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi, hivyo ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa uhakika, kwa mfano Stigler’s gorge (2000MW), Mnazi Bay 300MW na kufufua KIWIRA 200MW. Miradi yote hii inaweza kuendeshwa na sekta Binafsi iwapo tutaweka mazingira mazuri ya uwezekezaji. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa iachane na kujenga majengo na ijielekeze kwenye uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme nchini kwetu.
    2. Kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza TANESCO iingie mkataba na RICHMOND na baadae kuuhamisha mkataba kwa kampuni ya DOWANS. Vile vile kwa kuwa BUNGE ndio lililotoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na TANESCO kufanya hivy; Hivyo basi TANESCO wasibebeshwe chembe ya lawama katika suala hili. Mzigo huu ni mzigo wa Serikali unaotokana na ukosefu wa umakini, woga na kutowajibika kiuongozi kwa viongozi wa Serikali. Serikali haipaswi kujitenga na gharama zitokanazo na madhaifu ya TANESCO katika hatua zote kwani serikali ndio msingi wa matatizo yote ya TANESCO na hivyo inawajibika kubeba deni lote.
    3. Kwa kuwa Serikali itapaswa kulipa deni hili kutoka katika fedha za walipa kodi wa Tanzania na kwamba fedha hizi zitaondolewa katika bajeti ya Elimu, Afya na kadhalika, ni lazima Serikali itoe maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufika tulipofikia. Haiwezekani serikali itumie kodi ya wananchi kulipa deni la mabilioni ya fedha kwa kampuni ambayo serikali imeshindwa kuthibitisha uhalali wake na hata kutaja mmiliki wake.

    1. Kwakuwa Taifa linaingia hasara kubwa ya mabilioni haya ya fedha kutokana na udhaifu wa serikali kusimamia mikataba na mpango mzima wa nishati, nakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni katika Bunge la Februari ya KWANINI SERIKALI ISIWAJIBIKE KWA KULINGIZA TAIFA HASARA KWENYE SEKTA YA UMEME.


    1. Pamoja na mambo mengine na vile Bunge litaona inafaa, nitalitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati, na Mpango Kabambe wa usambazaji umeme (Power System Master Plan) na hivyo kusimamia migawo 3 ya umeme ndani ya miaka 2 ya uongozi wake.

Asanteni kwa kunisikiliza
Limetolewa na kusainiwa na;


David Zacharia Kafulila
Mbunge Jimbo la Kigoma Kusini
0716 42 62 20
 
Angalieni kwa umakini ili hii petition isije ikachakachuliwa. Maana hiyo ni muhimu sana. Leteni petition ya katiba kama mlivyoahidi
 
Angalieni kwa umakini ili hii petition isije ikachakachuliwa. Maana hiyo ni muhimu sana. Leteni petition ya katiba kama mlivyoahidi
Mams, usiwe na shaka. Hii petition haiwezi ikachakachuliwa (kuna "super commandos" wanaoilinda). Plus, petition a katiba inapaikana hapa (ingia usaini kama ulikuwa bado hujaanya hivyo): TUNAHIHITAJI KATIBA MPYA Petition
 
Back
Top Bottom