Peter Tosh's Family

Nimemuulizia baadhi ya mabredren toka Jah Make Yah (Jamaica) wanadai jamaa aliuwawa kwa kisasi na Dennis "Leppo" Lobban baada ya kushindwa kutimiza ahadi ya kusaidia familia ya Lobban wakati alipotumikia kifungo kirefu gerezani. Inasemekana Leppo alikubali kwenda gerezani muda mrefu kumsaidia Tosh a.k.a Bush Doctor/Mystic Man/ The Toughest aepuke gereza kutokana sababu alikuwa ana kesi ambayo angehukumiwa Tosh angesota gerezani muda mrefu na ingelikuwa mwisho wa career yake ya music, sasa alitakiwa aisidie familia wakati bredren leppo alipokuwa jela kitu ambacho Tosh hakutimiza .
 
Thanks Mkuu XRasta,nimeiangalia Bush Doctor,kama sikosei ndiyo ilibeba jina la Album ile
 
Bush Doctor ni moja ya track ambayo iko kwenye album ya Bush Doctor iliyotolewa mwaka 1978. Peter Tosh alitoa album zifuatazo: Legalize It 1976; Equal Rights 1977; Bush Doctor 1978; Mystic Man 1979; Wanted Dread and Alive 1981; Mama Africa 1983 na No Nuclear War 1987( hii album aliifyatua majuma machache kabla ya kuuwawa na Lobban). Live in Boston 1976 ilikuwa tour mahususi kuitambulisha album ya Legalize It kama solo baada ya kujiondoa the wailers kutokana na kutofautiana na Marley kwa upande mmoja na Chris Blackwell ( mmiliki wa Island Records) katikati ya miaka 1970.
 
Bush Doctor ni moja ya track ambayo iko kwenye album ya Bush Doctor iliyotolewa mwaka 1978. Peter Tosh alitoa album zifuatazo: Legalize It 1976; Equal Rights 1977; Bush Doctor 1978; Mystic Man 1979; Wanted Dread and Alive 1981; Mama Africa 1983 na No Nuclear War 1987( hii album aliifyatua majuma machache kabla ya kuuwawa na Lobban). Live in Boston 1976 ilikuwa tour mahususi kuitambulisha album ya Legalize It kama solo baada ya kujiondoa the wailers kutokana na kutofautiana na Marley kwa upande mmoja na Chris Blackwell ( mmiliki wa Island Records) katikati ya miaka 1970.

Yeah,,inadaiwa tofauti hizo ndo hata zilimpelekea kutohudhuria mazishi when Bob died! na alibaki na bifu naye since!
 
Namkubali winston hubert macntosh, mauzimia, pamoja na nyimbo nyingine ni ,here comes the judge, huu wimbo wazungu hawataki hata watu wengine wausikie! R.I.P PETER
 
Namkubali winston hubert macntosh, mauzimia, pamoja na nyimbo nyingine ni ,here comes the judge, huu wimbo wazungu hawataki hata watu wengine wausikie! R.I.P PETER

Mkuu salute! wimbo huu upo album ipi? tafadhali, ila jamaa alikuwa mkali!
 
Burial ni wimbo ambao uko kwenye albamu ya Legalize It. Nyimbo kama Here Comes The Judge, Maga Dog alizifyatua mwishoni wa miaka 1960 na mwanzoni wa miaka 1970 kabla hajajitoa THE WAILERS pamoja na Neville O'Rilley Livingstone a.k.a Bunny Wailer/Jah B/The Blackheart Man. Sababu iliyopelekea Wailers kusambaratika moja wapo ni Chris Blackwell mmiliki wa Island Records alikuwa anamsukuma Marley kama the main guy at the expense ya Tosh na Wailer. sababu nyingine ni kwamba nyimbo nyingi zilizokuwa zinaappear kwenye album za Catch a Fire and Burning zilikuwa zinatambulishwa kama mtunzi ni Marley pekee bila kushirikisha mchango wa Tosh na Wailer, vile vile Marley alikuwa anachukua lead vocals kwenye nyimbo nyingi za album tajwa tofauti na wenzake, nyimbo chache kama stop the train, 400 years and you can't blame the youth, Tosh alikuwa lead vocals na Bunny alikuwa lead vocal kwenye Haleluyah Time. Baada ya Tour ya UK, Bunny Wailer alikataa kutour USA ambapo nafasi yake ilizibwa na Marehemu Joseph (Joe) Higgs, sababu iliyotolewa wakati huo inasemakana alikuwa anaogopa kupanda ndege, ila kuna interview aliulizwa alidai alikataa kutour sababu aliona Blackwell/ Whitewell/ Whiteworst anawapeleka siko ana alifikiri Bob na Peter watamuunga kwa msimamo huo ila wenzake hawakufanya hivyo. Tosh alikuwa anataka kutoa single zake kupitia Island lakini Whiteworst alimgomea na ukizangitia uhusiano wake na Marley pamoja Whiteworst ulizorota mno akaamua kujiondoa. Walikuja kuperform pamoja kwenye concert 1974 na Marvin Gaye na ya mwisho kuperform pamoja ilikuwa kwenye concert ya wonder dream concert for the benefit of blind ambapo headliner alikuwa Steve Wonder.
 
Mkuu naomba nikusahihishe, mama yake Andrew anaitwa Shirley ambaye alikuwa dada yake Bunny Wailer. Pearl Livingstone ambaye ambaye anachangia mama na Bob na baba na Bunny alizaliwa mwanzoni mwa miaka 1960 kwahiyo ni vigumu kumzaa Andrew Tosh ambaye alizaliwa mwaka 1967.
 
Kama umeusikiliza wimbo burrial utakuwa na nafasi ya kelewa idea za tosh, huwezi laumu

Kuna interview Bob (Robert Nesta Marley) alifanyiwa na sikumbuki mwandishi gani,kuna mahala (kutokana na bifu hilo) alimuuliza Bob ikiwa atashindana/toa kibao kuijibu ile ya Tosh (I'm the Toughest) lkn Bob shortly alikataa na kusema"I dont compete,I dont compete": jibu linalotajwa kujaa busara!
 
Kama umeusikiliza wimbo burrial utakuwa na nafasi ya kelewa idea za tosh, huwezi laumu

Mkuu,nimeisikiliza "burial",Tosh ameongea mengi sana kumhusu Chris Blackwell,,,"The richman's heaven is the poor man's hell......,,Carrying people's bussines on your head....." Kimsingi alimtarget yeye kama Promota akizungumzia unyonyaji wa watu wanaoitwa promoters, Offcourse hii inatokea hata leo TZ, wasanii wengi wanalalamika kupunjwa/nyonywa na Promoters wao. Sijaona alipomgusa Bob,chuki yake kwa Marley hadi kususia mazishi ilitokana na "kijiba cha roho tu" nadhani?
 
Mkuu,wimbo mkali sana huu full philosophical! Kiufupi Tosh nae alikuwa mkali

Kitu sijajua ni Tosh alikuwa anachukuliaje dini/imani,katika baadhi ya nyimbo zake kama John Be.Goode anaimba akiwa kavaa joho kama la maaskofu/wachungaji,anashika msalaba mkono wa kulia kichwani kavaaa/zungushia kitambaa na kukifunga namna waislamu wanavaaa
 
Back
Top Bottom