Peter Serukamba: Kukataa Posho ni Unafiki

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho lilikuwa ni unafiki. Serukamba aliyasema hayo katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kupitia Magic FM.

Fina aliuliza moja ya swali kutoka kwa wasilizaji ambapo alisema biashara ya kukataa posho ni unafiki tu huku akimwambia Fina ataje Mbunge gani karudisha au kukataa posho, alisema, “Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa vingine tumechukua, hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa confirmed wengine wakaanza kukopa,” huku akisema hakuna umuhimu wa kupinga posho za wabunge badala yake wabunge waombe Serikali iwaongezee posho na watumishi wengine.

Alipoulizwa kwa nini wasiiombe Serikali ianze na sehemu nyingine kabla ya kuwaongezea mshahara Wabunge akitolea mfano wa Shirika la Ndege la Taifa ATCL, Serukamba alijibu kuwa siku zote binadamu anaanza na “mimi” kabla hujawafikiria wengine akikumbushia siku alivyopendekeza kama Bunge lifungwe kama watu hawataki Wabunge wapokee posho na kuishia kushambuliwa kupitia mitandao ya kijamii.

Serukamba aliongezea kusema kuwa bunge la Tanzania ni kati ya Mabunge yanayolipa hela ndogo sana watumishi wake ambazo ni milioni mbili tu kwa mwezi bila posho na kusema wanazidiwa na Bunge la nchi ya Burundi wanaolipwa dola 4,500 za Marekani.

Alimalizia kwa kusema jukumu la wabunge libaki kuwa kutekeleza wajibu wao wa kibunge ambao ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali itekeleze wajibu wake.

Source: Peter @Serukamba (Mb)*@MakutanoShow:*Kukataa posho ni unafiki - wavuti.com
 
SERUKAMBA AMECHOKA, AJIANDAE KUNG'OLEWA ALIKUWA ANABEBWA NA MAKAMBA BABU, SASA HAYUPO TENA ASIPONG'OLEWA NDANI YA CHAMA UPINZANI JIMBO WATABEBA.jianda baba mm mwenyewe nimeshatangaza nia endelea kulopoka ili unilainishie njia
 
Hiyo akili ya huyo serukamba ina-reflect akili za wana ccm na matumizi ya rushwa, ina maana hicho (posho) ni chanzo cha mapato kutunisha mifuko ya wahongaji, wananchi tunakataa wao wanaona na kutuona sisi ni wanafiki, Kwa taarifa yao aliye mnafiki ni jk anayekiri hadharani kuwa chaguzi za ccm zimegubikwa na rushwa akiwa na maana wagombea ndio wametoa rushwa na wajumbe/wapiga kura wamepokea na kukamilisha ufahamu kuwa aliyeshinda/kuchaguliwa ni zao la rushwa, MWENYEKITI WA CCM ANATUONYESHA "DENTO FOMULA" kuonyesha alivyoridhiiiiiiiiiiiiiika. Angalau wenzao CHADEMA "mainaz shibuda" wanakataa hiyo posho na wako tayari ifutwe hata leo, wao ccm wanatumia nguvu zote kupinga moja ya chanzo chao cha mapato ya kutunisha mifuko na mifumo ya rushwa kisiguswe kwa namna yoyote kwa lengo la kufutwa isipokuwa kwa KUBORESHWA!!!!!
kwa jinsi hii, Serukamba naamini hana uwezo wa kuwaongoza hata nyumbu kule ngorongoro.
 
Nipeni nukuu hivi ni lini bunge letu limetunga sheria. mimi huona wakipitisha sheria zilizotungwa na serikali kwa maslahi ya waserikali, nani anabisha.
 
Ale tu maana ndio kipindi cha lala salama. Baada ya 2015 atakuwa anaingia bungeni kama wageni wengine.
 
"Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa vingine tumechukua, hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa confirmed wengine wakaanza kukopa,"
[/QUOTE]

Hapa kuna hoja, sema alisahau na wengine walikataa magari mbele ya waandishi wa habari kisha wakayachukua kinyemela!!!!
 
huyo ni kibaraka, kazi kufuata vigogo nyuma nyuma kama mkia. Tabia zake zinashangaza mno kama....
 
kama hayo ndio mawazo yenu, saaa za ukombozi kwa mtazania zinakaribia........ hivi unajua maana ya kupinga kitu? unasema hivyo na watu wote wanakuangalia unafanya hivyo, lakini kama mfumo unakataaa, lazima unde nao mpaka utakapopata nafasi ya kuuhodhi na ndio utabadilisha kama unavyotaka

"Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa vingine tumechukua, hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa confirmed wengine wakaanza kukopa,"
[/QUOTE]

Hapa kuna hoja, sema alisahau na wengine walikataa magari mbele ya waandishi wa habari kisha wakayachukua kinyemela!!!!
 
hivi hao akina serukamba ndio humo raisi anaweza kupata mawaziri?....kuna haja sasa ya bubadilisha huo utaratibu, maana ndani ya CCM hakuna tena wabunge weledi.......
 
suala siyo nchi gani inawalipa vipi wabunge wake,suala ni nchi husika ina mapato kiasi gani?kama mnafisidi mapato ya serikali halafu bado mnataka mlipwe kama wenzenu wanaosimamia vizuri mapato yao shame.
nyinyi watetea ufisadi ndiyo wenye serikali,wafanya maamuzi ila tumeishawajua kuwa nyinyi ni wachumia matumbo wabunge wote wa ccm
 
Hata wale wa upinzani wanachukuwa posho.
 
KWA NINI USIWASEME WALE WENYE MAMLAKA YA KUPITISHA NA KUTOA POSHO?tunataka mfumo ambao utaweza kuwawajibisha wale wafujaji wa pesa za umma kwa sababu ameumbwa na tamaa,sasa ukiwatetea wanaolazimisha na madaraka ya kujilipa haitosaidia
 
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia CCM Mhe Peter Serukamba amesema suala la baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupinga posho lilikuwa ni unafiki.

Serukamba aliyasema hayo katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango kupitia Magic FM.

Fina aliuliza moja ya swali kutoka kwa wasilizaji ambapo alisema biashara ya kukataa posho ni unafiki tu huku akimwambia Fina ataje Mbunge gani karudisha au kukataa posho, alisema, “Tumeongezewa mafuta tumechukua, tumeongezewa vingine tumechukua, hakuna ambaye amerudisha na next day ilipokuwa confirmed wengine wakaanza kukopa,” huku akisema hakuna umuhimu wa kupinga posho za wabunge badala yake wabunge waombe Serikali iwaongezee posho na watumishi wengine.

Alipoulizwa kwa nini wasiiombe Serikali ianze na sehemu nyingine kabla ya kuwaongezea mshahara Wabunge akitolea mfano wa Shirika la Ndege la Taifa ATCL, Serukamba alijibu kuwa siku zote binadamu anaanza na “mimi” kabla hujawafikiria wengine akikumbushia siku alivyopendekeza kama Bunge lifungwe kama watu hawataki Wabunge wapokee posho na kuishia kushambuliwa kupitia mitandao ya kijamii.

Serukamba aliongezea kusema kuwa bunge la Tanzania ni kati ya Mabunge yanayolipa hela ndogo sana watumishi wake ambazo ni milioni mbili tu kwa mwezi bila posho na kusema wanazidiwa na Bunge la nchi ya Burundi wanaolipwa dola 4,500 za Marekani.

Alimalizia kwa kusema jukumu la wabunge libaki kuwa kutekeleza wajibu wao wa kibunge ambao ni kutunga sheria na kuisimamia Serikali itekeleze wajibu wake.
 
...Haya ndo yale yale ya yule mnafiki mwingine. Akiwa bongo kelele mingiii...oh ufisadi, ohh uwajibikaji lkn akiwa nje au na shida ya fweza, anakwenda kupiga mizinga kwa hao hao mafisadi. Yeye na yule mwenye afya ya kucheka cheka na kuanguka ni kitu kimoja na wana ufisadi sawa kabisa... ! Mmoja akiwa nje ya mipaka, wanawasiliana sana na ..i missi yuu broda au dogo ni mingi saana... au pia mukuba naomba dora kazaa nipo huku nimekwama kidogo na nitarudisha nikirudi!!! Anapewa chap chap na kupewa maagizo ya nini ya kusema akirudi in exchange of the msaada.... na ndiyo unasikia kuwa kweri mimi ni chijana na naipenda sana CDM kama mkate wa kumimina rakini sitajari utaratibu wao mie ntagombea ulaisi kivyangu-vyangu na hizo M4C sitashiriki kabisa !!!
 
bora kasema ukweli lakini....watu wanakimbilia ubunge kwa sababu ya pesa/posho/marupurupu hakuna kingine....
 
Back
Top Bottom