Peter Noni na Rostam - The EPA Connection

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Peter Noni na Rostam ni wabia wa biashara (Vodacom). Peter Noni ni shahidi wa serikali katika kesi za EPA zinazoendelea. Alikuwa ni bosi wa kina Imani Mwakosya, Esther Komu na Bosco Kimola. Katika ushahidi wake mwanzoni mwa mwaka huu aliiambia mahakama kuwa malipo ya EPA yalifanyika kwa idhini na ujuzi wa moja kwa moja wa Gav. Ballali. Alishuhudia mwenyewe kuwa taarifa zilitoka kwa Gavana kuja kwake, na baadaye kwenda kwa kina Imani.

Niliandika kwenye kijarida cha Cheche wakati nazungumzia mafisadi (mwishoni mwa mwaka jana) kuwa Peter anatakiwa kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa wizi huu lakini nilielewa kwanini asingeweza kusimamishwa kizimbani - kwa sababu ni mtu mmoja ambaye anajua connection ya Rostam.

Mfanyakazi wa BOT ambaye ana uwezo na fedha ya kuanzisha kampuni ya Planetel (ningependa kweli kujua kampuni hii ilianzishwa lini na wana hisa wake!) na kuwa na hisa kubwa tu kule Vodacom ambazo walikuwa waziuze (sijui kama tayari wameziuza) kwa kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na Rostam!

Mpango huo ulifanikiwa kwa ushirikiano mkubwa na usaidizi wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge.

Well.. je waridi likiwa na rangi nyingine laweza kuwa si waridi?
 
Mimi nimechoka kabisa yaani natamani niendelee kukaa ughaibuni mpaka hali ya mambo itulie nyumbani kwani nina ghadhabu sana naweza kukamatwa kwa kutukana au kuatarisha usalama sioni nchi inaelekea wapi maana kila kitu kinafall apart.

Hivi serikali inafaidika na nini kuhusu marumbano yanayoendelea sasa, kwanini haingilii kati na kuyasimamisha au kuchukua hatua za kushitaki wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kwanini maswali yanayoulizwa kila siku serikali haiwezi kuyatafutia suruhisho la kudumu badala ya kuyahailisha.

Sina haja ya kumtetea mtu lakini kama RA nafikiri hakuna cha maana anachotafuta kwani kana alikuwa na ushaidi kwanini alisubiri Mengi aseme na yeye ndio aseme wakati anajua yeye ni kiongozi wa taifa.

Inawezekana huu ni mpango wa serikali wa kumshughulikia Mengi, kwani hatuelezwi Kagoda mwisho wake nini, je nini mwisho wa uhusiano wa RA na RDC and DOWANS, nini mwisho wa ufisadi nani atafungwa kwa sababu ya ufisadi?

Tireeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeed
 
hivi hii Vodacom ndiyo inatumiwa kama front company ya kufyatua watu mbalimbali wanahusishwa na ufisadi? Au ni nini... ?
 
Mimi nimechoka kabisa yaani natamani niendelee kukaa ughaibuni mpaka hali ya mambo itulie nyumbani kwani nina ghadhabu sana naweza kukamatwa kwa kutukana au kuatarisha usalama sioni nchi inaelekea wapi maana kila kitu kinafall apart.

Kama unafikiri Kukaa Ughaibuni ndio suluhisho la matizo ya Tanzania wewe ni fisadi wa Uzalendo, huna tofauti na mafisadi wengine
 
hivi hii Vodacom ndiyo inatumiwa kama front company ya kufyatua watu mbalimbali wanahusishwa na ufisadi? Au ni nini... ?

Katika Uchunguzi wangu wa Kina, nimegundua kuwa Tatizo sio Vodacom Hapa, Tatizo ni UKABILA NA UKANDA ndio unatusumbua kwa sasa.

Wachaga walikuwa very influencial katika siasa za Tanzania, but they lost that status as the time was passing on. Ukiangalia utawala wa Mkapa uliwanufaisha sana wachaga, which has lost in Kikwete leadership. On other hand kwa Kuangalia political Map Rostam Aziz ni influential kwasababu alikuwa na good ties with the lake zone which politically always is a very big decider of Tanzania politics.

Ndio maana ukianza kutaja majina yote ya watu ambao wako associated na Rostam Aziz na VodaCom wote wanatoka kanda ya ziwa, mpaka unakuta hata Lipumba hawezi kuongea against RA

Rostam Aziz ni mnyamwezi, ukiangalia Tabora, Mwanza na Shinyanga mpaka Musoma ukweli ni kwamba kuna waarabu wengi sana ambao ni wafanyabiashara maarufu katika maeneo yao and they have helped those communities for many years.

Why Rostam Aziz ana kiburi? Rostam had legitimate business for so long and if you look back at Mirambo Holdings is one of very reputable investment company in Tanzania for so long.

Kilichoenda kombo ni kwamba Rostam alikuwa ni njia tu ya ku-justify uchotaji wa fedha za CCM ,

why KIKWETE YUKO KIMYA?

Since he drugged RA in this shit hawezi kumsaliti, COST ya yeye kumsaliti is equal to the lose of political map. RA anafahamika Mwanza, Shinyanga, Tabora na Musoma and he is very influential there, calculation ni kura za NEC Mzee, na kanda ya ziwa ndio imempa JK ushindi.

MENGI

Tatizo la Mengi ni kwamba he have been a big fish for so long, akiangalia mwelekeo wa biashara na political influence ilivyopotea kwa wachaga anaogopa. But he has legitimate claims panapoharibika ni kwamba waarabu wengi wenye ugomvi na Mengi ni kutoka kanda ya ziwa, wanajiita wasukuma. So Mengi is in battle to retain his powership/chaga but at the same time anasidia kupambana na ufisadi

Mwisho tulipofika sasa:-

- JK Anaangalia his political future.
- Wasukuma wameshikilia justice department
- Wasukuma,wanyamwezi hawawezi kumwachia RA afe maji
- JK hawezi kuwatosa wasukuma
- Wachaga, they see it is the time for them to gain their political influence
- Wasukuma wanawafunga mafisadi wachaga

NGOMA NZITO MZEE MWANAKIJIJI
 
Duu bongo politiks ni balaa kuelekeo 2010....tuone mwisho wake.
 
Kama unafikiri Kukaa Ughaibuni ndio suluhisho la matizo ya Tanzania wewe ni fisadi wa Uzalendo,huna tofauti na mafisadi wengine

Wewe umenena.Kama watu kama Dr. Slaa na Kina Mwakyembe wangeamua kukimbilia ugenini ingekuwaje?

Tusichoke iko siku moja Tanzania itakuwa huru.
 
Mwisho tulipofika sasa:-

- JK Anaangalia his political future.
- Wasukuma wameshikilia justice department
- Wasukuma,wanyamwezi hawawezi kumwachia RA afe maji
- JK hawezi kuwatosa wasukuma
- Wachaga, they see it is the time for them to gain their political influence
- Wasukuma wanawafunga mafisadi wachaga

Then mkuu hii ni vita ya kikabila kati ya wasukuma na wachaga!?

Inawezekana maana wengi waliopo mahakamani ni kina Kweka, Komu, Mramba, Mgonja nk
 
LeoKweli na Limbani msitupotoshe!

Hapa tunazungumzia vita dhidi ya ufisadi. It is a war between PATRIOTIC TANZANIANS against BOISTEROUS CORRUPT PEOPLE.

Hata humu jamvini ukifuatilia utaona kabisa kuna pande mbili. Wapo watetezi wa mafisadi ambao wanatoa hoja za kuharibu michomo dhidi ya mafisadi. Na wapo ambao wanajadili ufisadi kwa uchungu mkubwa wakinuia kuuondoa kabisa ili kuinusuru nchi na watu wake.

Hapa jamvini tuwatendee haki watanzania kwa kujadili kile ambacho kitaokoa uhai wa watanzania, kuyaboresha maisha yao na kuondoa umasikini unaowakabili.

Nchi hii ni tajiri sana. Lakini kutokana na tamaa ya baadhi ya watu ambao wana nafasi kubwa serikalini, wameamua kuuweka mfumo in such a way that watakula wao na marafiki zao na kuwaacha watanzania hoi kwa dhiki.

Huu ni unyama, upumbavu, uroho na ushetani ambao lazima tujenge utamaduni wa kuukemea bila soni hata moja usoni. Wanaotaka kuungana nami katika hili wajitokeze bila hofu.

Naipenda Tanzania
Nawapenda watanzania
 
naogopa kabisa kufikiria hoja ya kikabila.. kwa sababu in that case watu wa magharibi watashinda hands down! Hapana.. hii ni kati ya watu wanaoamini kuwa utajiri wa nchi ni wa kwao peke yao na wale ambao wanataka tugawane utajiri huo.

Hivyo Vodacom naamini ni mahali kama pa recruitment.. haiwezekani:

Dr. Idris
Ngeleja
Noni
Rostam
n.k something is very wrong.. kama RA ameweza kukuamini kwenye Vodacom.. you have passed the test
 
Kuna mahali nimesikia kuwa Rostam kakabidhi vielelezo vya ufisadi wa Mengi kwa Takukuru. Ni Takukuru walewale waliosema kuwa richmond haikuwa imeisababishia serikali hasara yoyote. Kwa Rostam ninayemfahamu, tusijeshangaa Mengi akitumukia kifungo baada ya kutiwa hatiani. Mkono wa Rostam upo hadi Judiciary!
 
Ole wao Takukuru nasema ole wao Takukuru waanze na Mengi wakati hawajamaliza ya KAGODA, MEREMETA, Richmond na zile kesi kubwa kubwa. Kwanza ili sisi yaani sisi nataka atuambie kuwa zile docs za Mengi ni zakuforge ndo waanze utafiti.
 
Peter Noni na Rostam ni wabia wa biashara (Vodacom). Peter Noni ni shahidi wa serikali katika kesi za EPA zinazoendelea. Alikuwa ni bosi wa kina Imani Mwakosya, Esther Komu na Bosco Kimola. Katika ushahidi wake mwanzoni mwa mwaka huu aliiambia mahakama kuwa malipo ya EPA yalifanyika kwa idhini na ujuzi wa moja kwa moja wa Gav. Ballali. Alishuhudia mwenyewe kuwa taarifa zilitoka kwa Gavana kuja kwake, na baadaye kwenda kwa kina Imani.

Niliandika kwenye kijarida cha Cheche wakati nazungumzia mafisadi (mwishoni mwa mwaka jana) kuwa Peter anatakiwa kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa wizi huu lakini nilielewa kwanini asingeweza kusimamishwa kizimbani - kwa sababu ni mtu mmoja ambaye anajua connection ya Rostam.

Mfanyakazi wa BOT ambaye ana uwezo na fedha ya kuanzisha kampuni ya Planetel (ningependa kweli kujua kampuni hii ilianzishwa lini na wana hisa wake!) na kuwa na hisa kubwa tu kule Vodacom ambazo walikuwa waziuze (sijui kama tayari wameziuza) kwa kampuni ya Mirambo inayomilikiwa na Rostam!

Mpango huo ulifanikiwa kwa ushirikiano mkubwa na usaidizi wa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge.

Well.. je waridi likiwa na rangi nyingine laweza kuwa si waridi?
mkjj..

utafiti wa ndani wa karibuni unaonyesha dk balali alikuwa very clean akazungukwa na watu (noni, RA, CCM leaders) wenye mbinu chafu kufanikisha ufalme wao...

wafanyakazi wa BOT walioshatakiwa kwenye kesi ya EPA wanamatumaini makubwa kusafishwa na wakuu wao kupitia mahakama...
 
Kwanini Peter Noni hakushtakiwa pamoja na wengine wakati yeye ndiye alikuwa kati ya Ballali na kina Mwakosya? Yawezekana kwa sababu ya uhusiano wake na RA na hivyo wakamchukua kuwa shahidi?
 
Mwisho tulipofika sasa:-

- JK Anaangalia his political future.
- Wasukuma wameshikilia justice department
- Wasukuma,wanyamwezi hawawezi kumwachia RA afe maji
- JK hawezi kuwatosa wasukuma
- Wachaga, they see it is the time for them to gain their political influence
- Wasukuma wanawafunga mafisadi wachaga
Too simplistic! Mzee Mwanakijiji kwa nini umeshukuru hii post? does'nt make sense to me at all.
 
Then mkuu hii ni vita ya kikabila kati ya wasukuma na wachaga!?

Inawezekana maana wengi waliopo mahakamani ni kina Kweka, Komu, Mramba, Mgonja nk
Na Maranda, Mahalu na Mwakosya ni wachaga? No way, la ukabila katika kushtakiana sikubaliani nalo!
 
naogopa kabisa kufikiria hoja ya kikabila.. kwa sababu in that case watu wa magharibi watashinda hands down! Hapana.. hii ni kati ya watu wanaoamini kuwa utajiri wa nchi ni wa kwao peke yao na wale ambao wanataka tugawane utajiri huo.

Hivyo Vodacom naamini ni mahali kama pa recruitment.. haiwezekani:

Dr. Idris
Ngeleja
Noni
Rostam
n.k something is very wrong.. kama RA ameweza kukuamini kwenye Vodacom.. you have passed the test
Usiogope sana kufikiria ukabila kwa sababu humo ndimo kunaweza kuwa na suluhisho la haya yanayoendelea hivi sasa.

If you check recent history, kuna mtu aliwahi kuwa mbunge wa Shinyanga mjini akiitwa Derefa. Katika kikao kimoja cha bunge aliwahi kitamka kuwa watawala wasipoangalia, kanda ya ziwa wanaweza kumega nchi yao. Alikuwa ni mtu wa masihara na watu wengi hawakuuchukulia msemo huo kwa uzito, lakini kumbe alikuwa anafikisha ujumbe fulani na tangu wakati huo, harakati zikaanza na hakuna hadi hii leo anayehusisha mambo hayo na ku-gain nguvu kwa watu wa kanda ya ziwa na kupoteza kwa wa kanda ya kaskazini as far as political power is concerned.

Hii vita ni zaidi ya ufisadi! Kwa wenye malengo yao, ufisadi unatumika kudhoofisha upande mwingine, lakini si lengo kuu la vita inayoendelea hivi sasa nchini
 
Inasikitisha watu wachache wajanja wanavyojitahidi kutuhadaa kwa mbinu zile za kizamani. Nijuavyo kuna mambo ukifanya kama huyaombei msamaha wa dhati, huwa yana namna ya kutafuta nafasi ya kukulipizia kisasi.Kinachotia moyo ni ujasiri wa kuweka wazi haya ambayo watu wachache wanaojidanganya kwamba wanaweza kufanya lolote bila kupata madhara yoyote. Ninahisi haya madhambi hata kama itachukua miaka mingi kuyapatia ufumbuzi, iko siku watanzania watawaamkia wote wanayoyatenda na kudai haki itendeke. Tatizo hili si la ukabila wala rangi. Ni tatizo la watu wachache kutaka kusambaratisha Taifa zima kwa ajiri ya kujilimbikizia isivyo halali utajiri wa nchi yetu. Watanzania hawa ninao waona mimi si wajinga tena vile tunavyowafikiria.Naona dola inapata kigugumizi kufanyia kazi matatizo yaliyopo. Inawezekana ni kwasababu dola pia ni sehemu ya tatizo.Ipo siku wataamua mana uongozi na madaraka ni dhamana wanayoitoa wao kwa wale wanaotaka wawaongoze. Tuombe mungu atujarie busara zaidi ila naona tunavyoenda sivyo kabisaaa
 
Back
Top Bottom