Pete ya uchumba

mareche

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
471
95
wana jaimii naombeni mwongozo hivi pete ya uchumba ana vishwa mwanaume na mwanamke au mwanamke tu maana rafiki yangu mmoja anataka kuvishwa na demuwake je hii ni sahihi nawasilisha
 
mwanume kuvaa pete ya uchumba!? kwani mwanaume anachumbiwa au anachumbia?
 
wana jaimii naombeni mwongozo hivi pete ya uchumba ana vishwa mwanaume na mwanamke au mwanamke tu maana rafiki yangu mmoja anataka kuvishwa na demuwake je hii ni sahihi nawasilisha

Hii mpya, sijaiona bado.. nani anamchumbia nani, labda jamaa yako anachumbiwa watch out anakwenda kuolewa huyo. :focus:
 
wana jaimii naombeni mwongozo hivi pete ya uchumba ana vishwa mwanaume na mwanamke au mwanamke tu maana rafiki yangu mmoja anataka kuvishwa na demuwake je hii ni sahihi nawasilisha[
Kama yeye nfo kachumbiwa na anaolewa. Ruksa kuvaa
 
Huu kwetu bongo ni uchuro, ila atakuwa msichana ameona mwanaume hamwambii atamuoa lini na wamekaa kipindi kirefu.wadada tuwe na subira
 
wanaume sijaona kuona wanavalishwa pete ya uchumba,labda huyo dada anamwambia kimafumbo kuwa kama hunivalishi basi mm nakuvalisha.na pete za uchumba wanazovalishwa wanaume zikoje?ila wahindi si nasikia wanawake ndio wanaoa,au huyo dada ana asili ya kihindi?najiuliza tu.
 
nashukuruni wana jf kwa ushauri wenu nitajaribu kushauri huyo my best kama hana wazo la kumvisha japo amgusie aone atachukuliaje :welcome:
 
Ruksa kumvalisha mwanaume pete ya uchumba. Kama hujasikia baso basi mimi nimeshahudhuria nyingi. May God bless them
 
He?? Kweli dunia inaelekea ukingoni duuuhh mwanaume kuvishwa pete ya uchumba?? Mungu tusaidie maana hali ni mbaya humu duniani.

Sasa inakuwa na vitu vya almasi au tanzanite?? Au ndo ikoje???

Mtume yarabi tobaaa aaahhh
 
He?? Kweli dunia inaelekea ukingoni duuuhh mwanaume kuvishwa pete ya uchumba?? Mungu tusaidie maana hali ni mbaya humu duniani.

Sasa inakuwa na vitu vya almasi au tanzanite?? Au ndo ikoje???

Mtume yarabi tobaaa aaahhh

Umeona eeee ni soo
 
Yesu utarudi lini???????????

mwanaume anataka kuvishwa pete ya uchumba lol!! au lbd mwanaume si riziki????????
 
japo siyo ya kuchekesha lakin imenichekesha na kunishangaza kwa wakati mmoja.....hapa tz tangu lini mwanaume akavishwa pete ya uchumba na mwanamke??,,mwanaume kuvishwa pete ya uchumba kunanifanya nikubaliane na elia kuwa huyo mwanaume basi anaenda kuolewa yeye.

huyo kijana kabla hajavishwa pete ya uchumba ahakikishe anajua anapata kufahamu nini maana ya pete ya uchumba na hasa kwa tafsiri ya hapa tz.

vijana jitahidini kujua kila maana ya jambo unalotaka kufanya ili usije kuingia kwenye mkasa kama huu wa kuvishwa pete ya uchumba na mwanamke....lakin pia nalazimika kuamini kuwa nyuma ya pazia huyo binti ana sababu inayomsukuma kumvisha pete mchumba wake huyo.....nijuavyo mimi kila jambo lifanyikalo au litokelo huwa lina sababu yake...
 
Dah brother huyo hicho ni choo cha kike,hamna kitu kama hicho.. Watanzania tumeuacha utanzania na tukaanza kufikiria kwa fikra za kigen.. Huo sio uafrica wetu!
 
Back
Top Bottom