Pete katika ndoa

Hah hapo ameondoka nyumbani kanuniwa....hahah maisha ya ndoa mwe acheni tu!

Mie nilikuwa nikitoka nje ya nyumba bila nayo yaani nakosa amani sasa najiuliza kwa nini nakosa amani sipati jibu!! maana kama kusahau si nimesahau na hakuna kitu kibaya unafanya........mwe vifungo vingine ni kujipa jakamoyo tu!

Hapo kwenye Blue.............Naomba nitume application LOL.
Waiting na kikombe changu cha kahawa naangalia Coming to America LOL

LOL...mwj1 huna hata haja ya kutuma application...nakukabidhi wizara zote na umakamu wa raisi.
Pete haikuchubui weye?...Mie nakusudia pete ijayo niimezee na maji ikajivishe moyoni.
 
Hiyo kali Mbu......uimeze na maji mwe!!

Lakini tukirudi nyuma mie ninafahamu wasabato huwa hawavishani pete wanapooana ingawa wengi wamekuwa wakizivaa baadae! So kwangu mie nahisi umaana wa pete kwa watu kama hawa uko zaidi kwenye definition inayowekwa na jamii zaidi kuliko kulinganishwa na maandiko au uaminifu wa ndoa zao kinje: Pete zao wanazivaa mioyoni!

Ila sasa na wewe na hii thread yako usijewapa watu kisingizio......sivai pete kwa kuwa nimeivaa moyoni mwe!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

na kweli, si unaona Data alivyoandika hapa...;

mie naona ni fasheni tu...

...yaani itabakia ina maana kwa wenye kujua na kuithamini maana tu.
mnh, ama kweli hii taasisi inahitaji ufunuo mpya...yu wapi The Finest atuletee somo?
 
with_this_ring2.jpg
...pamoja na tafsiri zote, kuvishwa PETE na umpendae ni the best feeling ever!
 
Kwa wanandoa inamaanisha kuwa ninyi ni wenzi halali kwa kipindi chote mtakapokuwa pamoja. Uhalali huu hutakiwa kwenda sambamba na kiapo cha uaminifu mlichokitoa na kuhakikisha mnakifuata.Kwa wanajamii- Ina maanisha kuwa fulani (mwenye pete) hayuko available ni mali ya mtu tayari na hivyo vishanshuda na mangurumbene wakae mbali na kifaa hicho.
Ndugu naomba kujua majina hayo penye nyekundu na blue ni ya jinsi gani na nini maana yake?
 
Hahaaaaaa hukuiweka rehani baada ya kukosa hela ya malipo acha kutuzuga bwana...........Halafu siku hizi watu hawazivui ,tena unakuta pete limejaa nusu kidole mkono huo huo umekumbatia guberi...........zamani kidogo mtu akifanya upuuzi wake anaiweka mfukoni akikaribia kimlango cha home inarudishwa kulikuwa na kauoga fulani nafikiri.
mtoto taratibu aisee... majina gani hayo unaita waume za watu??
 
mi naamini kuwa pete ni kwaajili ya zile promise zote mlizopeana wakati na kabla ya kuoana, ikiwemo suala la kucheat n.k kama heshima haitakuwepo ndani ya ndoa hata kama hakuna cheating hapa maana yake ndoa imeshavunjika. Kwa kawaida anaevaa pete anajisikia furaha kuivaa, kama mke/mume ni kero pete unaivaa ya nini? Haina maana.
 
Nyie wenzangu pete mwavaa na kuvua daily?? Mimi toka nivishwe siku ya harusi nilivua once tu kwani gold ni ngangari sioni sababu ya kuvua. Nadhani kama wavua ukienda kuoga kuna uwezekano mkubwa sana wa kuipoteza.

Kuhusu walioachana; ni kweli mimi nawajua kama mtu tatu wame divorce lakini hawataki kuvua pete. Nadhani wanahofia maswali kwani kama mmoja huyo yeye hajawahi mwambia mtu kuwa the marriage is over ila washikaji tunajua na tuna pretend not to know.
Si unajua waswahili na kupenda kuhoji; ndiyo maana watu wanajiamulia kuendelea kuvaa.

Ila mimi sijali watu wanasemaje aisee. Niliwahi gombana na hubby pete nikazivua na nikawa nadunda bila pete.

Pete kwa wanawake ina raha yake. Inapunguza maswali yale ya umeolewa au uko single. Na wanaume wengi wenye akili timamu wanaheshimu sana wadada wenye pete kwa hiyo tunaepuka usumbufu wa hapa na pale.

...hhahha,...Ikunda usishtuke bana, ndio hali ya dunia na mapito yake,
ila hapo kwenye ubuluu, umenichekesha sana...wengi hujifanya wameisahau juu ya dressing table
Halafu upo kazini unashtukia simu/sms ..."umeiachia nini pete nyumbani?"---Problem Solved.

Dawa tosha hiyo saa ingine.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kweli mimi nikiachika cha kwanza kufanya ni kuvua pete. Si kwamba na advertise kuwa niko single ila naona kama ntakuwa nampa bichwa mtalaka wangu kwa kuendelea kuvaa pete "yake"
mi naamini kuwa pete ni kwaajili ya zile promise zote mlizopeana wakati na kabla ya kuoana, ikiwemo suala la kucheat n.k kama heshima haitakuwepo ndani ya ndoa hata kama hakuna cheating hapa maana yake ndoa imeshavunjika. Kwa kawaida anaevaa pete anajisikia furaha kuivaa, kama mke/mume ni kero pete unaivaa ya nini? Haina maana.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Ila mabinti wa siku hizi ni balaa. Enzi za ujana wangu sikuwahi kumpa nafasi mtu mwenye pete aniambie kuwa ananipenda. Kwanza nilikuwa nahoji mpaka jamaa anaona amekutana na padri alomfungisha ndoa. I thank God sijawahi tembea na mume wa mtu mpaka naolewa na sijawahi hata kumtamani. Nikiona pete tu hata uwe handsome vipi nilikuwa nakuona kama kaka yangu. Siku hizi wame za watu ni fashion.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hivi ndoa za kiislamu wana valishana pete?na kiapo chao kinakua wapi?mana ndoa ikifungwa binti anakua hayupo!
 
Waislamu hawavai pete. Ila wa siku hizi naona wanavaa nadhani wanaona zinapendeza kama urembo. Kuna muislamu mmoja alinambia eti vitabu vyao haviruhusu kabisa mwanume kuvaa pete nadhani alisema gold ndiyo marufuku; ila mapedeshee si unajua tena wanavaa tu magold wakati hairuhusiwi kwa mwanaume wa kiislamu. Ngoja wataalamu watatupa majibu.

Hivi ndoa za kiislamu wana valishana pete?na kiapo chao kinakua wapi?mana ndoa ikifungwa binti anakua hayupo!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Pete chanzo chake ni ibada za kishetani(Devil worshiper)kwani ni moja ya kanuni zao na anaevaa anakuwa anafanya ibada hiyo,hawa Devil worshiper wana kanuni 3,moja alama,pili ishara na tatu ni hesabu,pete au ring ni symbol ya Lucifer ikiwakilisha jua kwa alama ya mviringo au circle,alama ya jua(circle)inatokana na maana ya neno Lucifer yaani "mwenye nuru"au "mtoa nuru"na hata walioanzisha illuminati linawakilisha maana hiyohiyo,pete sio alama wala ishara ya upendo kwa mkeo au mumeo,bali upendo wako na mshikamano wako kwa Lucifer,lakini waabudu shetani hawa wanaamini circle au duara pamoja na triangle(pembe tatu) ni alama ya uumbaji wa Lucifer,wanaamini Lucifer ndiye muumbaji,alipomaliza akaweka alama hizo kama ishara ya mwanzo wa uhai,mfano uzazi wa mwanadamu,uke unawakilishwa na circle na uume unawakilishwa na triangle(tazama kuanzia kwenye kichwa mpaka karibu na wanaposhonea wakati wa circamsition mwisho wa kichwa,inafanana na pyramid au triangle)kumumbuka Mungu amekataza ibada ya ishara au alama alisema"wamuabuduo Mungu halisi watamuabudu katika roho na kweli"pia pete ziko kwenye maandiko gani?
 
Mh. Hapo unatuchanganya

Pete chanzo chake ni ibada za kishetani(Devil worshiper)kwani ni moja ya kanuni zao na anaevaa anakuwa anafanya ibada hiyo,hawa Devil worshiper wana kanuni 3,moja alama,pili ishara na tatu ni hesabu,pete au ring ni symbol ya Lucifer ikiwakilisha jua kwa alama ya mviringo au circle,alama ya jua(circle)inatokana na maana ya neno Lucifer yaani "mwenye nuru"au "mtoa nuru"na hata walioanzisha illuminati linawakilisha maana hiyohiyo,pete sio alama wala ishara ya upendo kwa mkeo au mumeo,bali upendo wako na mshikamano wako kwa Lucifer,lakini waabudu shetani hawa wanaamini circle au duara pamoja na triangle(pembe tatu) ni alama ya uumbaji wa Lucifer,wanaamini Lucifer ndiye muumbaji,alipomaliza akaweka alama hizo kama ishara ya mwanzo wa uhai,mfano uzazi wa mwanadamu,uke unawakilishwa na circle na uume unawakilishwa na triangle(tazama kuanzia kwenye kichwa mpaka karibu na wanaposhonea wakati wa circamsition mwisho wa kichwa,inafanana na pyramid au triangle)kumumbuka Mungu amekataza ibada ya ishara au alama alisema"wamuabuduo Mungu halisi watamuabudu katika roho na kweli"pia pete ziko kwenye maandiko gani?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kweli mimi nikiachika cha kwanza kufanya ni kuvua pete. Si kwamba na advertise kuwa niko single ila naona kama ntakuwa nampa bichwa mtalaka wangu kwa kuendelea kuvaa pete "yake"

...hivi, kurudishiwa pete, au kunyang'anywa pete ipi ina uchungu zaidi?
hili swali linahusu wa'wake na kwa wa'ume..maana nishayashuhudia haya.

140906-425x282-Return-Engagement-Ring.jpg

Japo Kuna wengine huzitupa kabisa...
 
Swahiba mbu... salaam sana kutoka Quito, jiji tamu lenye kila ladha ya latinas na latinos....

Nimejaribu kuiba muda na kupitia hii mada yako lakini to be honest nakosa nguvu kubwa ya kuchangia kwani kwa baadhi yetu hii pete haina maana tena. Tunaitumia tu kama ID ya kuonyesha your civil status basi, majority ya "akina sie" tuliowahi kutoka nje ya reli unakuta hata hukumbuki kwamba you are wearing a thing, waweza kukumbuka kwamba umevaa soksi, saa, chain etc lakini si hiyo kitu

Pia kuna wengine (men or women) wanavaa tu hata kama ndoa zao zilishakwenda marikiti, na pia kuna wasiovaa ingawa wana ndoa very strong

Anyway sijui tuiwekeje but mimi nimewakilisha kundi "dogo" lililopoteza thamani ya pete kama ishara ya upendo

Mapenzi ya siku hizi ni "umjuaye na umpendaye" kama alivyosema Rashid Majaliwa kwenye riwaya ya Kuli.... mimi natafsiri kwamba we love two types umjuaye (aweza kuwa yoyote) na umpendaye (pia aweza kuwa yoyote) na hilo tayari linafifisha maana ya pete
 
Dahhh,....kamanda umeninyong'onyesha sana swahiba yangu.
Kwa maandiko tu nimehisi ni kwa jinsi gani unavyoungulia hali iliyopo.
Umegusia jambo la maana sana kwamba kuna wengine mmeishia kuivalia mazoea tu.

Dahhh, ...sina hata la kuongeza bro...inauma sana.
Pete hizi...kuna mengi yamejificha nyuma yake.
 
we acha tu, i dont know why lakini kuna ka upepo kamepita imefikia kila kitu tunafanya kama fasheni... siku hizi hata kuwa na mpango wa kando ni sunna, inauma sana uchungu lakini kwa wengi tunaoishi Dar tunayaona, sijui mikoani au nje hali ikoje lakini kwa dar ni balaa

Kuna siku (kama alivyotoa mfano chauro) nilikuta dada ana peke kama nusu kilo hivi ya ndoa na nyingine ya engagement... lakini alivyokua amekaa chobingo na jinsi alivyokua amekula chicha na mambo aliyokua anayafanya huwezi kuamini

I think there is a need for a social campaign kuhamasisha jamii kuamka na hali iliyopo..............
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hivi ndoa za kiislamu wana valishana pete?na kiapo chao kinakua wapi?mana ndoa ikifungwa binti anakua hayupo!
Usiandike usichokijua bwana. Bint wa kiislamu huwa anaulizwa naye na huyo sheikh anayefungisha ndoa na ndoa haifungwi mpaka akubali. Ukisikia vigelegele ujue kakubali.
 
Back
Top Bottom