Malengo ya mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo(Comunity Development Catalyst Fund-CDCF)

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Nimetembelea tovuti ya Wizara ya Fedha nikakutana na mgawanyo wa fedha za Majimbo yote. Fedha hizi zinafanya kazi gani majimboni?

Inawezekana kabisa fedha nyingi hapa nchini zinaishia kwenye siasa hizi.

Kwa hali hii kila mtu anaweza kuwa mbunge kwa sababu fedha za kutekeleza ahadi zako tayari zinakuwepo.


------ Tutor B anajibu----

YAFAHAMU MALENGO YA MFUKO WA JIMBO.
Mfuko wa jimbo ni mfuko ulianzishwa kisheria na ulipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na lengo kuu la kupitishwa kwa mfuko huo ni kuchochea na kuongeza kasi katika miradi mbali mbali iliyoanzishwa na wananchi katika majimbo yao (The Constituencies Development Catalyst Fund Act. Na. 16 ya mwaka 2009)

Kama ilivyoahinishwa hapo juu lengo la kuanzishwa kwa mfuko huu ni kuchochea maendeleo katika majimbo ya uchaguzi. Ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo ufanyika kwa juhudi za wananchi wakishirikiana na mbunge wao, pamoja na serikali kuu kama mchochezi mkuu anayetoa pesa husika.

Serikali kupitia bunge tukufu ilifanya hivi hili kurahisisha maendeleo kwa kasi katika majimbo husika; ikiamini kuwa kwa kuwa mbunge yupo karibu na wapiga kura wake itamuwia rahisi kutekeleza maendeleo hayo japo, maskini serikali haikujua kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu wanaishi mbali na sisi na huwa tunaonana nao kipindi cha kuomba tena ridhaa yetu.

Kama wengi wasemavyo kuwa "ukitaka kupima utu wa mtu mwangalie katika mambo mawili PESA na CHAKULA" mara nyingi pesa hizi zimekuwa hazifahamiki matumizi yake hasa baada ya serikali kuzitoa. Kunakuwa hakuna ufuatilia wa kina juu ya matumizi yake; jambo ambalo limekuwa faida kwa wabunge.

Utaratibu unasema kuwa pesa hizi za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDF) hupewa kwa kila mbunge wa jimbo na huwabagua wabunge wa viti maalumu na wale wabunge wa kuteuliwa na Rais.

Mfuko huu hudhibitiwa na kamati maalumu ya watu sita (6) kama sikosei ambao wote huteuliwa na mbunge husika ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa mfuko huo. Kamati hii hukoma pale mbunge husika anapokoma kuwa mbunge kwa kushindwa ubunge, kung'olewa na mahakama au kifo.

Mbunge na kamati yake ndiyo wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya pesa za mfuko huu na si lazima matumizi hayo yaende sambamba au yawiane na vipaumbele vya halmashauri ya mji,wilaya au manispaa.

Wabunge wa viti maalumu wanataka pia kupewa pesa za CDF kwa madai kwamba wana majukumu sawa au hata kupita yale ya wabunge wa majimbo. Kabla ya kufikiria kuwajumuisha wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa na Rais katika kupata fedha za mfuko wa jimbo ni vema ukaguzi na upembuzi ufanyike kwanza ili kubaini manufaa ambayo yameletwa na mfuko huu kama yapo.

Ushirikishwaji wa wananchi katika hili umekuwa haufahamiki, ajabu ukijaribu kuwahoji hata baadhi ya madiwani katika halmashauri zetu mbalimbali hawajui huwepo wa pesa hizi na kama wanajua hawafuatilii matumizi ya pesa hizi.

Miradi mingi ya wananchi inakwama kwasababu ya kukosa kichocheo muhimu kama hichi ambacho serikali iliona umuhimu wake ila ikasahau kufuatilia utekelezaji wake.

Suhala la shule kutokuwa na huduma bora zinazopaswa hupelekea wanafunzi wengi wa sekondari kukata tamaa na kuacha shule kabisa ama kupata matokeo mabaya mwishoni. Lakini ukiwasikiliza watu hawa wana moyo na hali yakujitoa ila support ya viongozi husika inakuwa ndogo! Mfuko wa jimbo na ubunifu wa viongozi wetu ukitumika tunaweza kutatua tatizo hili maana naamini inawezekana sana.

Wabunge wengi wa majimbo ukitaka kugombana nao wahulize kuhusu pesa za mfuko wa jimbo. Kijana mmoja aliwahi kumhoji mbunge wake lakini alichojibiwa hakikuwa kizuri kwa ustawi wa uwajibikaji kwa wananchi waliomchagua.

Mara nyingi wabunge wetu wakitumia pesa za jimbo katika shughuli ndogo za kijamii ujinasibu kuwa hizo ni pesa zao wenyewe toka mfukoni mwao, wanatumia mihanya hiyo ya wananchi kutojua ukweli wa jambo hili.

Hivyo uzitumia pesa husika kujihimarisha kisiasa, ndiyo maana wanaharakati wengi wamekuwa wakiishauri serikali kufuta sheria hiyo na kuondosha hii mifuko ya jimbo kwani imeonekana ilianzishwa kwa lengo zuri ila usimamizi na utekelezaji wake hauleti hali chanya kwa walengwa.

Ukiangalia kwa mfano Mgawanyo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo 2010/2011 majimbo kama kielelezo kwenye picha kinavyoonesha yalipata pesa nyingi tu lakini nani anaweza kujua zilitumikaje katika majimbo yetu?

WITO WANGU KWA WANANCHI, baada ya kutambua matumizi na malengo ya pesa za jimbo tuanzishe miradi mbalimbali na tuwashirikishe wabunge wetu na wakigoma kutusupport tuwahoji hizi pesa zilitumika kwa matumizi gani?


Yamkini viongozi wetu (wabunge) wamejisahau sasa tuwakumbushe kwa kuanzisha miradi mbalimbali na kutaka mchango wao toka mfuko wa jimbo.

ANDIKO HILI LINALENGA KUEMILIKISHA JAMII JUU YA SHERIA YA MFUKO WA JIMBO NA MALENGO YAKE.

-----

Pia soma
>Mfuko wa Jimbo kupingwa mahakamani - JamiiForums
>Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF - JamiiForums
 

Attachments

  • JIMBO.pdf
    55.3 KB · Views: 124
Kwa wale wenye ujuzi na mambo haya naomba nifahamishwe hili fungu linalotolewa kwa minajili ya kuendeleza jimbo (constituency development fund) huwa linatumikaje na ni kiasi gani kwa jimbo?

Maana sijawahi kuona hata kitu kimoja kimendelezwa jimboni mwangu; mfano barabara, zahanati au shule na ikadaiwa ni kutoka fungu hili.

Mara nyingi utasikia mbunge kajitolea kununua madawati, kakarabati zahanati au kanunua madawati kwa shule fulani na utakuta anadai ametumia labda pato lake binafsi na mifano mingine mingi tu.

Je, hii CDF hutumika wapi na ni kiasi gani?
 
Hivi walipewa wabunge wote au ni wale wa kuchaguliwa majimboni tu?

Kuanza kuhoji wamezitumiaje kutaibua mjadala mpya.
 
Waliopewa ni wale wa kuchaguliwa majimboni. Kuhusu matumizi yake wanaojua ni waheshimiwa wabunge. Nafikiri ni posho nyingine ya waheshimiwa wabunge.
 
Ndugu Wabunge wa Bunge la JF;

Mimi binafsi huwa nashindwa kuelewa kuhusu MFUKO WA JIMBO, ambao kwa maelezo ni kwamba kila Jimbo la Uchaguzi kuna mfuko kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Jimbo husika. Kipindi cha Kampeni mwaka 2010 ulikuwa ndio kauli mbiu ya Wagombea wengi kuwa "Wakichaguliwa watasimamia mfuko huu ili ufanye kazi" walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa "Ni pesa nyingi sana Serikali inatoa katika Mfuko wa Jimbo na wajanja wachache wanakula hizo pesa, hivyo tuwachague ili wakazisimamie"

Ni mwaka mmoja na nusu sasa toka tufanye uchaguzi; na baadhi wale wale waliokuwa wanasema haya maneno wapo madarakani, lakini sijajua au kupata tetesi zozote kuhusu ule wimbo wa "MFUKO WA JIMBO" maana umekuwa kimya.

Je, Wabunge JF, kuna anayeelewa kuhusu Mfuko wa Jimbo au mfano ni Majimbo yepi yanayonufaka na mfuko wa Jimbo??? NAOMBA ANIJUZE TAFADHARI!!!


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Wakuu kuna hili suala la mfuko wa maendeleo ya jimbo(CDF) ambao umeanza yapata miaka miwili sasa, sina hakika ni kwa kiasi gani mfuko huu unatimiza malengo yake.

Pesa hizi za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDF) hupewa kwa kila mbunge wa jimbo na hubagua wabunge wa viti maalumu na wale wabunge wa kuteuliwa na Rais. Mfuko huu hudhibitiwa na kamati maalumu ya watu sita kama sikosei ambao wote huteuliwa na mbunge husika ambaye pia ndiye mwenyekiti wa mfuko huo. Kamati hii hukoma pale mbunge husika anapokoma kuwa mbunge kwa kushindwa ubunge, kung'olewa na mahakama au kifo. Mbunge na kamati yake ndiyo wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya pesa za mfuko huu na si lazima matumizi hayo yaende sambamba au yawiane na vipaumbele vya halmashauri ya mji,wilaya au manispaa.

Wabunge wa viti maalumu wanataka pia kupewa pesa za CDF kwa madai kwamba wana majukumu sawa au hata kupita yale ya wabunge wa majimbo. Kabla ya kufikiria kuwajumuisha wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa na Rais katika kupata fedha za mfuko wa jimbo ni vema ukaguzi na upembuzi ufanyike kwanza ili kubaini manufaa ambayo yameletwa na mfuko huu kama yapo.
 
Wakuu kuna hili suala la mfuko wa maendeleo ya jimbo(CDF) ambao umeanza yapata miaka miwili sasa, sina hakika ni kwa kiasi gani mfuko huu unatimiza malengo yake.

Pesa hizi za mfuko wa maendeleo ya jimbo (CDF) hupewa kwa kila mbunge wa jimbo na hubagua wabunge wa viti maalumu na wale wabunge wa kuteuliwa na Rais. Mfuko huu hudhibitiwa na kamati maalumu ya watu sita kama sikosei ambao wote huteuliwa na mbunge husika ambaye pia ndiye mwenyekiti wa mfuko huo. Kamati hii hukoma pale mbunge husika anapokoma kuwa mbunge kwa kushindwa ubunge, kung'olewa na mahakama au kifo. Mbunge na kamati yake ndiyo wenye kauli ya mwisho juu ya matumizi ya pesa za mfuko huu na si lazima matumizi hayo yaende sambamba au yawiane na vipaumbele vya halmashauri ya mji,wilaya au manispaa.

Wabunge wa viti maalumu wanataka pia kupewa pesa za CDF kwa madai kwamba wana majukumu sawa au hata kupita yale ya wabunge wa majimbo. Kabla ya kufikiria kuwajumuisha wabunge wa viti maalumu na wale wa kuteuliwa na Rais katika kupata fedha za mfuko wa jimbo ni vema ukaguzi na upembuzi ufanyike kwanza ili kubaini manufaa ambayo yameletwa na mfuko huu kama yapo.

well said mkuu, naungana nawe 100% mfuko huu ni unneccessary cost center na hauna maana yoyote zaidi ya duplication of efforts with costs. Nimeshitushwa kuwa mbunge ndiyo anateua kamati ya mfuko, noma!!
 
Jamani nijuzeni hivi mfuko wa jimbo mali ya nani manake hata sijui unatumikaje na nani anatoa maamuzi ya matumizi ya fedha yake.
 
Huo ni mfuko wa Jimbo kusaidia maendeleo ya Jimbo,na mwenyekiti wa mfuko huo ni Mbunge wa Jimbo,kamati ya Maendeleo ya Jimbo inatakiwa kutoa maamuzi ya matumizi.Tatizo kama kamati inavilaza wengi basi mbunge anadominate maamuzi yote!!!
 
Jamani hivi jamani wabunge wa viti malumu huwa wanapewa hela za majimbo? ni sh ngapi? je wabunge wa majimbo huwa wanapewa sh ngapi kwa ajiri ya majimbo yao? mwenye kujua haya naomba anijuze jamani,sababu nimeona wabunge huwa wanatumia hela hizi kwa manufaa yao tu.Asanteni.
 
unatakiwa kwanza utuambie mbunge wako wa jimbo anaitwa nani ilitukupe majibu fanya ivo tupe jina kwanza tukupe majibu mbwana mdogo sawa
 
mawio.PNG
Tafuta gazeti hili, Toleo la Alhamisi 3/10/2013. Maslahi ya Wabunge, mishahara, posho za aina mbalimbali zilichambuliwa vizuri sana.
 
Mkuu fedha za mfuko wa Jimbo ie Constituency Catalyst Development Fund hutolewa kwa wabunge wa kuchaguliwa tu. Na fedha hizi huingizwa kwenye akaunti ya Development ya halmashauri.Kwa mujibu wa sheria ya mfuko huo fedha hizi zinatakiwa zisitumike bila kupitiswa na kamati ya mfuko wa jimbo iliyoko kisheria, na pia miradi itakayopangiwa fedha hizo ni lazima iwe imeibuliwa na wananchi wa eneo husika. Sasa kwa kuwa mbunge ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko wa jimbo ndo maana ama anakula hela au anapeleka kata ambazo ana maslahi nazo. Kwa kweli madiwani wa CDM fedha hizi zinawapitia hewani tu. Mfano jibunge kama Mwigulu lilianzisha ligi ya mpira kupitia hizi hizi hela, wakati takwimu za mapungufu mbalimbali katika sekta ya elimu inasikitisha
 
Watu mnaharibu kiswahili siku hiza yani mnakera mpaka basi! Kwani si wanafundisha darasa la kwanza mwandiko?
 
Ndugu wadau;

Tukiwa tunaelekea kipindi kingin cha Uchaguzi kwa kuingiza madarakani Serikali ya awamu ya Tano.

Ni vyema kama endapo Wabunge na wahusika watatuwekea hadharani matumizi ya Mfuko wa jimbo lake ili wananchi tuweze kupima na kuangalia ni maendeleo kiasi gani yamefanyika katika maeneo yetu kwa kutumia fedha hii, kwani bila shaka inatuhusu wananchi wote.

Nawaomba Wah. Wabunge na wale wanaohusika katika kila jimbo watuwekee hadharani hata ikiwezekana hapa ili tuelewe kabla ya Uchaguzi ujao.

Nawasilisha


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Sioni kama kuna umuhimu wa kuendelea kutoa fedha za mfuko wa jimbo kwa kila jimbo hapa Tanzania. Fedha hizi zimekuwa zikitumiwa vibaya sana na wabunge wetu, na hazifuati mfumo wa fedha za ruzuku za maendeleo.

Pia sioni sababu ya kuendelea kutolewa maana moja ya ahadi za mh Magufuli ni kila kijiji kitapata milioni 50 , pia bado kila kijiji upata pesa za ruzuku za maendeleo.

Moja ya mapungufu ya sheria hiyo ni kumweka mbunge kuwa mwenyekiti wa kamati hy ya mfuko wa jimbo hali inayopelekea kushindwa kumwajibisha mbunge.
 
Habari waTZ wenzangu,

Leo kumetokea mvutano bungeni baada ya mbunge mmoja kutaka wabunge wasio na majimbo nao wapewe fedha za mfuko wa jimbo wakati akijua hana jimbo.Hoja hiyo imenipa mawazo mengi kwamba hizo fedha huenda zina kwapuriwa tu na wabunge bila kufika kwa wananchi.Baadhi ya wabunge walifika mbali wakipendekeza bora hiyo iachwe kutolewa.

Je huko jimboni kwako hiyo fedha unajua ilifanya nini na wapi?

Je sheria hiyo ya mfuko wa jimbo ikifutwa kuna madhara yeyote kwa wananchi?

Je Rais aache kutoa hiyo fedha kwa kuwa inasababisha ugomvi kati ya wabunge wenye majimbo na wale wasio na majimbo?

Je Kwanini wabunge wasio na majimbo nao wanang'ang'ania wapewe fedha hizo wakati hawana majimbo?
 
Hizi nafasi za ubunge wa upendeleo huwa nazichukia sana maana hazina faida kwa taifa zaidi ya hasara, hizi nafasi zinapaswa zifutiliwe mbali kabisa na katiba ya nchi maana ni upuuzi mtupu
 
Tatizo huwa tunawaumiza wabunge kwa kuomba watoe fedha kwa ajili ya maendeleo badala ya kuhamasisha maendeleo na shughuli nyingine za kibunge ndio maana na wabunge wa viti maalumu wanaomba fedha za mifuko ya jimbo ili wakifika majumbani (wanakotoka) wasikose cha kutoa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom