Pesa za deci zimeenda wapi jamani

Gomezi Richard

New Member
Oct 26, 2010
3
0
Ndugu Watanzania inauma sanatena sana na tena inatia uchungu , ni miaka 2 sasa tangu serikali iliyopo madarakani iliposema inaingilia kati suala la DECI ili kuharakisha Watanzania kupata haki yao, lakini kilichotokea wtanzania hawa waliohidiwa maisha bora kwa kila Mtanzania hali wasiyaone wakaamua kujitosa huko DECI ndipo walipoyaona maisha bora lakini hadi leo hii bilioni 14 za wana DECI walizoahidiwa kuzipata wamejikuta kesi ikiwa mahakamani kwa muda wa miaka 2 sasa, kwani watanzania hawa wamekosa nini wengi wao wakiwa ni watumishi wa Mungu na wanyonge wasio na hatia hadi leo hawana matumaini juu ya mabilioni hayo ya fedha, huku wakiwa wamepigwa mkwala kutokujikusanya makundi makundi kuongelea swala hili, jamani ni kesi gani hiyo isiyo isha watu wakapewa haki yao, uonevu huu unasikitisha sana watanzania wengine waliuza nyumba zao wakajiunga na DECI mmewaambia DECI haikusajiliwa sawa wamekubali ila pesa zao zipo wapi? Dr.Slaa ameliongelea hili na tuna imani naye akiishinda watazirudisha pesa za Watanzania ambao waliuza mbuzi, kondooo, mavuno ya shambani kwao, nyumba, wengine wafanyakazi wa ndani wakadunduliza, wengine mishahara yao, wengine walikopa, Dr.Slaa wewe ndio MTANZANIA Halisi ambaye tuna imani utawatoa Watanzania kwenye mateso ya miaka mingi , maonevu, dhuluma, ujeeuri na rushwa iliyo kisiri na ufisadi , tunahitaji kuona pesa hizi zinarudi hawajaiba hawa watanzania, na bado mioyo yao ina uchungu hadi leo wengine wamekufa hawajapata haki yao, Dr.Slaa Mungu yu pamoja nawe jipe moyo mkuu tumechoka sisi watanzania
 
Pesa haziwezi kurudi! Wanazitumia kwenye mambo yao - mwisho wa siku watakwambia watu wa DECI walizipoteza na serikali haina hizo pesa. Si unajua usanii wa viongozi wetu? Sasa hivi watu wanatafuna faida na interest!
 
Dah hii deci wangeirudisha ikae hata sita Tu, naamini vyuma vingelegea. Watu walitajirika sana kwa kweli
 
Back
Top Bottom