Pesa ya school fees... Ada.

sarikoki

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
1,194
721
Hii pesa ina balaa,ni tamu ajabu na huwa hairudishiki...wakati nasoma mambo ya kulipia bank yalikua bado hayajaanza. Ilikua shule zikifunguliwa tunakutana pale Moshi mjini maana wanafunzi wanaotoka Dar lazima walale town kesho yake ndo tunaenda kijijini shule.
Balaaa linakuja unaanza kuonyesha ufahari.... yaani pocket money inaisha kabla hujafika shule... then unaamia kwenye ada... kudadadeki ukifika shule unamsomesha basa ,unamwambia baba amesema ataleta.... siku zinaenda , mambo yanakua sio mambo pale asubui moja mko parade ghafla unaona basa anakuja na karatasi la majina ya wanaodaiwa, pembeni kuna mwalimu wa zamu na viranja wa mabweni. Yaani mliotajwa baada ya hapo mnasindikizwa kuchukua mabegi alafu home no discussion.

Alalfu mara nyingi demu uliyekula naye maisha na pesa ya ada yeye jina lake halitajwi,....... mara ya mwisho nakumbuka nilizingizia pochi imedondoka chooni......aisee.
 
he hee heee mimi nilikuwa nafanya kusudi sichukui home school fees ili ikitokea amri ya kurudishwa home
nirudi home kula vinono
siku moja ile kurudi home tu ijumaa kujifanya nimerudishwa kwa ada
nikafikiri nitakaa hadi jumapili ndo niondeke
duh..jumamosi nikafurumushwa na kupewa ada nikalipe lol
 
asante nilizaliwa bibi kizee, marfuku kugusa ada.

Na ole mwanangu ale ada, itamtandika kama NSSR walokula NSSF yangu.
 
du mie dingi alikuwa nuksi, nikiwa o levo day, dingi akikupa ada jion anadai risit.

nikiwa f 2 nikadokoa na kununua unyunyu, dingi alipodai risit jion nikasingizia vitabu vya risit vimeisha so wakinunua watanipa risiti, so basa karekodi kwenye likitabu lake, dingi akasema poa uwakumbushe wasije wakasahau.

dingi usiku akachezwa na machale, kesho yake katinga skull bila mie kujua, ghafla nasikia unaitwa kwa hedmasta,

Naingia hamadi mdingi huyu, yaani ile kuniona tu, nilikula makofi ya kufa mtu bila hata kupewa nafasi ya kutoa maelezo.

H/masta alikuwa mnoko kinoma, ila kwa kile kichapo alilazimika kuokoa jahazi, pale dingi kwa hasira akalipa pesa ingine bila kudai ile alionipa jana yake (30,000)

Akaaga tutaonana home akaondoka, headmaster alishindwa kuniadhibu baada ya yale makofi ya fastafasta ya mdingi.

Jion yaliyo nikuta home nayajua mie.
 
Du kuna mitambo humu duniani...sijawahi wala kufikiria kwamba ada huliwa...
 
Me ada sikuwahi kulipa (kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo siyo ujanja,namshukuru H/master Mr.Mwasha) si unajua boarding halafu special school kitu 70,000, parefu bado unatoka mbali kwa treni,tulikuwa tulizungushana nimelipa wakati nachukua cheti,......MUNGU AMBARIKI SANA HUYU H/MASTER MANAKE ANGEKOMAA DU NDOTO ZANGU ZINGEYEYUKO HATA JF SIJUI KAMA NINGEIJUA
 
he hee heee mimi nilikuwa nafanya kusudi sichukui home school fees ili ikitokea amri ya kurudishwa home
nirudi home kula vinono
siku moja ile kurudi home tu ijumaa kujifanya nimerudishwa kwa ada
nikafikiri nitakaa hadi jumapili ndo niondeke
duh..jumamosi nikafurumushwa na kupewa ada nikalipe lol

Hehehe.. alafu mara nyingi unachelewa kufika nyumbani.... unakuta umerudisha toka asubuhi uzurura mjini ikifika jioni kali ndo unaingia home.... maana unaogopa ukiwahi unaweza pewa siku hiyohiyo ugeuze school...... Mimi nilikua naendaga kwa bibi alafu natinga home Jumamosi mchana....kwa hiyo ngoma jumatatu hiyo. Du...!
 
Me ada sikuwahi kulipa (kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo siyo ujanja,namshukuru H/master Mr.Mwasha) si unajua boarding halafu special school kitu 70,000, parefu bado unatoka mbali kwa treni,tulikuwa tulizungushana nimelipa wakati nachukua cheti,......MUNGU AMBARIKI SANA HUYU H/MASTER MANAKE ANGEKOMAA DU NDOTO ZANGU ZINGEYEYUKO HATA JF SIJUI KAMA NINGEIJUA

Von huyu Mr Mwasha sio wa ile shule kule mwika?
 
du mie dingi alikuwa nuksi, nikiwa o levo day, dingi akikupa ada jion anadai risit.

nikiwa f 2 nikadokoa na kununua unyunyu, dingi alipodai risit jion nikasingizia vitabu vya risit vimeisha so wakinunua watanipa risiti, so basa karekodi kwenye likitabu lake, dingi akasema poa uwakumbushe wasije wakasahau.

dingi usiku akachezwa na machale, kesho yake katinga skull bila mie kujua, ghafla nasikia unaitwa kwa hedmasta,

Naingia hamadi mdingi huyu, yaani ile kuniona tu, nilikula makofi ya kufa mtu bila hata kupewa nafasi ya kutoa maelezo.

H/masta alikuwa mnoko kinoma, ila kwa kile kichapo alilazimika kuokoa jahazi, pale dingi kwa hasira akalipa pesa ingine bila kudai ile alionipa jana yake (30,000)

Akaaga tutaonana home akaondoka, headmaster alishindwa kuniadhibu baada ya yale makofi ya fastafasta ya mdingi.

Jion yaliyo nikuta home nayajua mie.

Hehehhehe..alafu ukitoka hapo unaenda chooni kunawa uso ili watu wasishtukie....ukirudi class unajichekesha chekesha...ehehehhe.. Nakumbuka mshua alikua akiitwa school anakuja na fimbo zake ..... hakuulizi yeye anachosikiliza ni maelezo ya headmaster tu...baada ya hapo anatoa saa, miwani na pakiti yake ya sigara maranyingi inakuaga mfuko wa shati...then anaanza shughuli..bila walimu kuingilia hakuachii.. ila namshukuru sana.
 
Back
Top Bottom