Pesa wanazolipwa Wabunge ni rushwa?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Pesa wanazolipwa Wabunge ni rushwa wanayopewa na Serikali ili waburuzwe kwa hiari yao bila ya kupinga kitu. Ndio maana utaona Mbunge kasimama anaibwatukia Serikali lakini mwisho anamalizia kwa kusema, "Naunga mkono hoja mia kwa mia".

Ndio maana Mwaka jana, Wabunge wote pamoja na Wapinzani walimvamia Dr. Wilbroad Slaa, MP Karatu (CHADEMA), alipotoa hoja ya kuwa Mishahara ya Wabunge ipunguzwe waongezewe wafanyakazi. Hii ni State Corruption.

Penye njaa, demokrasi ina kazi kusimama na Serikali inajua hivyo na inaitumia hio hali to their advantage. Tanzania kama Nchi si maskini, watu wake ndio maskini. Hapa hapana demokrasi bali domokrasi na tumbokrasi tu.

Je Unajua kuwa
kuna Nchi inayoitwa Somaliland .Hio haina Support ya Budget kutoka UNDP au IDB wala EEC lakini GNP yake ni kubwa kuliko sisi ,Howu comes ?
 
Mwiba,
haya ndio maswali mazito wanayoshindwa watu kuelewa. Na hakika ndio kitu hujiuliza kwa nnini tunafanya uchaguzi hali tukijua kwamba Wabunge wengi wanatafuta nafasi ya kuwakilisha matumbo yao. Ndio lugha ya mjini kila mtu kaingia siasa kwa sababu ya uwezekano wa kuvuta...
Mishahara ya Wabunge na posho zao ni kubwa kupita kiasi, pengine kwa ujumla wake malipo ya mishahara na posho za serikali yetu ni mikubwa kuliko ile ya nchi tajiri wakati uzalishaji wetu ni chini mara 10 ya nchi hizo hizo.
Tatizo letu sisi ni Ujinga na Ulimbukeni, hiyo njaa ni matokeo ya watu hawa.
 
We si umeona hata wabunge wa upinzani wakishaingia kwenye kamati za bunge wanakua mabubu na kutoa kauli za kisiasa zaidi??? naamini kwa wao ni ubinafsi kuliko njaa kwani pesa ya kula wengi wao wanayo!!!
 
Mkuu Mwiba unapotea sana ukiibuka unakuja na kitu kama suprise vile...ila usahau kuwa waswahili wanasema 'penye fungu ndipo penye nyongeza'.
 
We si umeona hata wabunge wa upinzani wakishaingia kwenye kamati za bunge wanakua mabubu na kutoa kauli za kisiasa zaidi??? naamini kwa wao ni ubinafsi kuliko njaa kwani pesa ya kula wengi wao wanayo!!!

Ni ukweli tena ulio wazi. Mishahara, posho za vikao, Mikopo ya magari, nyumba Dodoma, nk vyote vyatumika kuwaziba midomo wabunge. Na uwaziri ndo ziba domo jumla kwa mbunge wa CCM alokwishaonekana akihoji mambo kwa undani. Hayo ndo yalomkuta P. Marmo na wengine.
Pendekezo langu Uwaziri na Ubunge vyapaswa kutenganishwa ili Serikali iwe kweli yawajibika kwa Bunge. Haiingii akilini kuwa Waziri atajihoji mwenyewe kwa kutumia kofia ya Ubunge pale utendaji wake serikalini unapokuwa mbovu. Na akijisahau akahoji ya waziri mwenzake ndo anatimuliwa jumla. Yalimkuta Mrema kwenye kesi ya Chavda!
 
Kichekesho sasa uwakute kwenye mijadala yao ya Kamati za bunge hasa pale wanapokutana na wakuu wa taasisi ambazo Kamati zao zinazizimamia. Kwanza wengi wanaonyesha kuwa na upeo finyu wa mambo mengi sana yenye maslahi kwa nchi na ambayo wao wanayasimamia. Mpaka wakati mwingine unajiuliza kama wabunge hawa wanaangalia zile sessions za kamati za senate kula marekani wanavyokata nondo mpaka White House inatingishika.

Kubwa ni vile wanavyohangaika kulazimisha wakuu wa taasisi wakitoa presentation, hasa kwenye power popoint ziwe semina kusudi tu wapate posho y a semina kwa wakuu wa taasisi wakati wanalipwa posho kwa kila sitting kutoka kwa Katibu wa Bunge. Kuna wengine kila ukikutana nao wako broke!
 
Nashangaa ulikuwa hujui kama pesa hizo ni rushwa tu.

naambiwa hata kama waziri anatoa majibu ya hovyo"kusema pamoja na majibu yako mazuri mh waziri ni KANUNI inawezekana kupanda mzuka na kuishia kuunga mkono hoja ni kanuni kama sio hivyo ni RUSHWA
 
Mishahara ya Wabunge na posho zao ni kubwa kupita kiasi, pengine kwa ujumla wake malipo ya mishahara na posho za serikali yetu ni mikubwa kuliko ile ya nchi tajiri

Mkandara umetamka kweli sema kwa uhakika badala ya pengine "malipo ya wabunge wa Tanzania ni mkubwa kuliko wa wale wa nchi tajiri kwa tarakimu na kimaisha"

Mishahara hii ni rushwa tu haina maelezo mengine. Kwanza sirikali inatumia kuwa tawala wabunge, wanashindwa kuwa waledi katika kazi yao kwa ajili yake. Pili malipo hayo inasadikiwa watumie sehemu kuhonga wanachi ili warudi bungeni, serikali ikidai wanaleta maendeleo. Niambieni ni lini mtumishi akatumia mshahara wake awaletee maendleo wananchi? Wizi mptupu. Hii ni sawa na wachimbaji wa madini eti wajenge zahanati na shule! Je kazi ya serikali ni nini? Naona aibu kuendelea kwani ninapata kichefu chefu na serikali yangu
 
Back
Top Bottom